Ndugu Mwenyekiti,
Gazeti la KISIWA la Ijumaa ya tar; 17 August lenye kichwa cha habari: MFUNGO WAISHA NA MIUJIZA MIKUBWA.
Mwanzo kabisa baada ya kuziangalia picha hizo nilidhani ni gazeti la
Aprili Mosi ile siku ya wajinga, la hasha ni la leo na ni habari kama
habari zingine za kina.
Mwenyekiti naomba uiweke hii kwenye ukurasa wako wa mbele kwa faida ya
wengi - maana si wote wanaosoma maoni, ila ikiwa hapo juu mbele watu
wote wataona uozo huu wa kuweka habari bila chunguzi za kina.
Maoni yangu kwa wizara ya habari isiishie tu kufungia magazeti
yanayowachachafya wanasiasa, hata haya yanayopotosha umma kwa malengo ya
kuuza kupitia imani za watu ni kebehi na hayatufai. Watuombe radhi
ukurasa wa mbele kama yalivyoweka habari katika ukurasa huo, nina imani
watauza pia.
Picha iliyopo ni ya mtindo unaoitwa wa "multimedia", hivyo ni ya kutengeneza.
Tafakari;
(1) watu waliouwawa na joka hili la kutisha ni wengi kiasi cha kuashiria
uwepo wa watu wengi katika eneo hilo, lakini cha kushangaza hakuna watu
wa kulishangaa na kusherehea kuuwawa kwaa joka katika mji huu
uliopoteza watu wengi. Pata picha sawaka limeuwawa Nyeregete kule
kijijini kwa Mwenyekiti halafu umeamua kupiga picha, sidhani kama
kutakosa watu wa kulishangaa.
(2) Hili ni joka kubwa sana, la miujiza ya kipekee, limepoteza maisha ya
watu wengi sana, haiingii akilini kwamba walimuua hawakuwa na shauku ya
kuweka kumbukumbu kwa kupiga picha ya pamoja na joka hili
tutakaloliingiza kwenye kitabu cha rekodi za dunia cha Guinnes, kama
zipo mtuzodoe kwa kuziweka hewani tuzione, naahidi kuomba radhi, kufuta
kauli na kuwasifu kwa kazi nzuri.
Picha yenyewe;
(1) Angalia kwa umakini gari lilobeba nyoka, kwa waliokuwa na wazazi
wenye nafuu walipata kuendesha magari haya wakati wa kuchezea ya
plastiki, nakumbuka jirani yangu walikuwa na tipa la kubinua mchanga, la
njano kwa kumbukumbu nzuri, sisi tulindesha ya mbao yakiwa na matairi
tulikata kwenye malapa ya umoja, wengine waliendesha ya mabati ya korie
na wengine ya kukata maboksi ya biskuti. Hata askari aliyekalia nyoka
naye ni wa plastiki.
Yaani iko hivi, nyoka wa kweli kwenye gari la plastiki (trick of the
eye), halafu ikafanyiwa editing kidogo kwa kompyuta kuongezea
background.
Kiufupi ni kwamba, habari ni ya kutengeneza na picha ni ya kutengeneza kwa ufundi mbovu.
Ndugu zangu wa gazeti la KISIWA mtuombe radhi, hapa hakuna Elimu, hakuna Maarifa wala Habari.
Mwenyekiti nitakushukuru kama hautaiweka hii nyuma ya pazia la
"comments" na badala yake uiweke usoni ili wengi wapate kuiona na
kuisoma ili wachangie katika hili.
Inakera kuona baadhi ya wanataaluma ya habari kutofanya tafiti za kina kabla kutujuza vinavyojiri kama habari.
Mdau - Hussein
Mungu Ibariki Tanzania na watu wake.
Mjumbe mwingine: Mfungo waisha na miujiza mikubwa, gazeti KISIWA.
Maoni yangu kwa wizara ya habari isiishie tu kufungia magazeti
yanayowachachafya wanasiasa, hata haya yanayopotosha umma kwa malengo ya
kuuza kupitia imani za watu ni kebehi na hayatufai mtaani. Watuombe
radhi ukurasa wa mbele kama yalivyoweka habari katika ukurasa huo,
watauza pia.
Picha iliyopo ni ya mtindo wa "multimedia",hivyo ni ya kutengeneza.
Tafakari; (1) watu waliouwawa na joka hili la kutisha ni wengi kiasi cha
kuashiria uwepo wa watu wengi katika eneo hili, lakini cha kushangaza
hakuna watu wa kulishangaa katika mji wa watu wengi. Pata picha sawaka
limeuwawa Nyeregete kule kijijini kwa Mwenyekiti halafu umeamua kupiga
picha, sidhani kama kutakosa watu wa kulishangaa. (2) Hili ni joka kubwa
sana, la miujiza ya kipekee, limepoteza maisha ya watu wengi sana,
haiingii akilini kwamba walimuua hawakuwa na shauku ya kuweka kumbukumbu
kwa kupiga picha joka hili, kama zipo mtuzodoe kwa kuziweka hewani
tuzione na tuwasifu kwa kazi nzuri.
Picha yenyewe; (1) Angalia kwa umakini gari lilobeba nyoka, kwa
waliokuwa na wazazi wenye nafuu walipata kuendesha magari haya wakati wa
kucheza, sisi tulindesha ya mbao, mabati na ya kukata maboksi. Hata
askari aliyekalia nyoka naye ni wa plastiki. Yaani iko hivi, nyoka wa
kweli kwenye gari la plastiki (trick of the eye), halafu ikafanyiwa
editing kwa kompyuta POORLY.
Kiufupi ni kwamba, habari ni ya kutengeneza na picha ni ya kutengeneza kwa ufundi mbovu.
Ndugu zangu wa gazeti la KISIWA mtuombe radhi, hapa hakuna Elimu, hakuna Maarifa wala Habari.
Source: Mjengwa