Sunday, August 12, 2012

Kitengo cha dawa asilia Muhimbili chagundua tiba ya Kisukari

Kitengo cha Utafiti wa Dawa Asilia cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, kimegundua dawa za asilia za aina tatu za kutibu magonjwa ya kisukari na kibofu cha mkojo.

Kitengo hicho ambacho kazi yake ni utafiti wa dawa asilia, kimefanikiwa kugundua dawa hizo katika kipindi cha miaka 38 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1974.
Dawa zilizogundulika na kuonyesha mafanikio makubwa ni aina ya Morizela zilizopo kwenye mfumo wa juisi ambazo moja ina sukari na nyingine haina ambazo zimeonyesha mafanikio makubwa katika tiba ya kisukari.
Dawa nyingine ni aina ya Prucan ambayo hutibu wagonjwa wenye matatizo ya kutopata haja ndogo, magonjwa ambayo huwapata zaidi wanaume wazee.
Akizungumza na gazeti hili, Kaimu Mkurugenzi wa kitengo hicho, Dk. Ester Innocent, alisema pamoja na kwamba dawa hizo zimeshaanza kutumika, lakini bado hazijaingia sokoni kwa vile bado ziko kwenye Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA).
Alisema TFDA ikishatoa usajili wake, kitengo hicho kinaweza kuingia mikataba na wenye kampuni za kutengeneza dawa ili zizalishwe kwa wingi na kuwafikia wagonjwa wengi popote walipo.
Alisema kwa sasa dawa hizo zinapatikana kwa uchache sana kutokana na kuzalishwa hospitalini hapo na ikishapata usajili, itapatikana kwa wingi.
Kwa mujibu wa Kaimu Mkurugenzi huyo, pamoja na kitengo hicho kuanza muda mrefu na hatimaye mwaka huu kutoa rasmi dawa hizo, wengi wataona imechukuwa muda mrefu lakini akasisitiza kuwa utafiti kwa kawaida huchukuwa muda mrefu.
Dk. Innocent alisema watafiti mara nyingi ni wepesi kugundua tiba ya dawa, lakini dawa hiyo haiwezekani kutumika bila kujua madhara yake, hivyo wanalazimika kuanza tena utafiti wa kuyajua madhara hayo na kuyadhibiti.
Hata hivyo alisema zipo dawa nyingi za asili zinazofanyiwa utafiti lakini ambazo utafiti wake uko karibuni kukamilika ni za aina 11 zinazotibu magonjwa mbalimbali kama malaria, pumu, tumbo, ngozi na magonjwa nyemelezi ya ukimwi.
Alisema kitengo hicho kinakabiliwa na changamoto nyingi hasa za uhaba wa fedha na hivyo kujikuta kuchelewa kutoa matokeo ya tafiti zao kwa wakati.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

Real Madrid Yaichapa Celtic

Real Madrid finished the World Football Challenge with four straight wins, even collecting a clean sheet against Celtic in Philly.


 Emilio Izaguirre, Celtic; Cristiano Ronaldo, Real Madrid
Drew Hallowell
PHILADELPHIA -- Like it has so many times before, Real Madrid took the field, put on a show and walked away victorious. The opponent didn’t matter, nor did the venue. The result was the same.

A continent away from their homes, families and domestic leagues, the Scottish and Spanish champions met Saturday afternoon in Philadelphia in the final match of this year's World Football Challenge. Celtic was merely the latest victims of Jose Mourinho’s high-priced wrecking ball of talent, falling 2-0 -- although the score belied the match's one-sidedness.

MBUYI TWITE ATUA RASMI YANGA ATIA SAINI MKATABA



Mlinzi wa kati wa timu ya APR kutoka nchini Rwanda Mbuyu Twite amekalisha usajili wake ikiwa ni pamoja na kupata uhamisho wa kimataifa ITC na kuweza kujiunga na mabingwa wa kombe la klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati kombe la Kagame timu ya Young Africans Sports Club.

Mbuyu Twite amabye zoezi lake la usajili lilianza takribani wiki mbili zilizopita limefikia mwisho baada ya klabu ya Young Africans kufanikiwa kupata uhamisho wake wa kimataifa kutoka timu aliyokuwa akiichezea ya APR ambapo awali alikuwa akiichezea timu ya Lumpopo st.

Twite ambaye alingara sana katika mashindano ya Kagame yaliyomalizika hivi karibuni na Young Africans kuibuka mabingwa, amesema anajisikia furaha na mwenye bahati kufanikiwa kujiunga na mabingwa mara mbili mfululizo wa kombe la Kagame.

Usajili wa Twite ulianza takribani wiki mbili zilizopita ambapo mjumbe wa kamati ya Utendaji wa klabu ya Young Africans Abdallah Bin Kleb aliamua kwenda nchini Rwanda kuhakiksiha zoezi hilo linakamilika haraka ipasavyo, ambapo mara baada ya kumalizana na Twite aliendelea kuhakikisha anafuatilia ITC yake.

Akiongea na www.youngafricans.co.tz Bin Kleb amesema, Young Africans ni timu kubwa katika Ukanda huu, Viongozi wake wanafanya mambo yao kwa uhakika zaidi, hivyo hawakutaka kuongelea suala la Twite mpaka watakapoona wamekamilisha zoezi lote'

"Unajua usajili sio mchezaji kusajuli makaratasi ya mkataba tu, kuna kupata barua ya kumruhusu kutoka timu anayotoka, uhamisho wa mchezaji kutoka chama husika cha soka cha nchi, baada ya hapo ndio unaweza kutangaza sasa kwamba ni mchezaji wako halali"alisema Bin Kleb.

Kusajiliwa kwa Mbuyu Twite kunaifanya timu ya Young Africans kuwa na ukuta wa walinzi wa kimataifa akiwemo Kelvin Yondani, Nadir Haroub Cannavaro, Ladislau Mbogo na Ibrahim Job kwa nafasi ya ulinzi wa katikati.

Twite anatarajiwa kuwasili mapema wikii kuungana na wacheji wenzake katika mazoezi ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara inayotarajiwa kuaanza sepetemba mosi. 


Source: http://www.youngafricans.co.tz

Mitetemeko ya Iran yauwa mamia ya watu


Idadi ya watu waliokufa kwenye mitetemeko miwili ya ardhi nchini Iran inazidi kuongezeka, na sasa inajulikana kuwa watu kama 250 wamekufa.
Shughuli za uokozi baada ya mitetemeko ya Iran
Watu wengine 2,000 wamejeruhiwa.
Waokozaji wanawatafuta manusura kwenye kifusi cha majengo yaliyoporomoka katika miji na vijiji kwenye eno la mji wa Tabriz, kaskazini-magharibi mwa nchi.
Shirika la Mwezi Mwekundu la Iran limechukua uwanja wa mpira kuwapa hifadhi watu waliopoteza makaazi yao, au wanaogopa kurudi nyumbani.
Shirika hilo limetoa mahema, mablanketi na chakula.
Shirika la Mwezi Mwekundu la Uturuki, limesema linatuma msaada mpakani.

Lema Amwomba Slaa Agombee Arusha Mjini


MBUNGE wa zamani wa Arusha Mjini, Godless Lema amesema anatamani Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa agombea ubunge wa jimbo hilo akieleza anaamini atatoa mchango mkubwa zaidi kwa chama kabla ya mwaka 2015.Lema alitoa kauli hiyo juzi usiku jijini Dar es Salaam, wakati wa harambee ya kuchangia chama hicho kwenye kampeni yake ya Vuguvugu la Mabadiliko maarufu kama Movement for Change (M4C) mkoa wa Dar es Salaam.

Alisema katika chama hicho kuna watu wengi wanaoweza kuwa wabunge wa jimbo hilo, lakini yeye binafsi angependa Dk Slaa awe mbunge wa Arusha Mjini kwa sababu Katibu Mkuu huyo wa Chadema akiwa bungeni ni moto wa kuotea mbali.

Lema alisema: “Kuhusu ubunge wa Arusha sina hofu, atakuja Dk Slaa au mimi, ingawa sasa napenda aje Dk Slaa.”
Alisema angefurahi kama Dk Slaa angekuwa mbunge wa jimbo hilo hasa katika kipindi hiki cha kutafuta mabadiliko kumpokea wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Lema alisema hivi sasa anafurahia mchango mkubwa anaoutoa katika chama chake akiwa nje ya Bunge.
“ Nahisi kutoa mchango mkubwa katika chama nikiwa nje ya Bunge kuliko nilivyokuwa bungeni kwa sababu nimefanya shughuli nyingi zenye matokeo chanya katika taifa hili,” alisema Lema.

Lema alienguliwa ubunge mwaka huu na Mahakama ya Kuu Kanda ya Arusha kwa kilichoelezwa kuwa alitumia lugha chafu katika kampeni za kuusaka ubunge huo mwaka 2010.

Kuchangia fedha za M4C
Lema alieleza kuwa fedha zitakazopatikana katika harambee hiyo zitatumika kununulia helikopta, magari, pikipiki, baiskeli na matumizi mengine ya Chadema kwa ajili ya kufikisha ujumbe wa ukombozi kwa wananchi.

“Tusifanye siasa ili kutafuta vyeo bali tulenge kuleta mabadiliko chanya katika jamii iliyonyanyasika kwa muda mrefu. Nchi yetu ilipata uhuru, lakini sasa tunahitaji mabadiliko yanayowakomboa wananchi kutoka kwenye umasikini,” alisema Lema.

Kauli ya Mbowe
Akizungumza katika harambee hiyo Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema kuwa, propaganda za ukabila, udini na rangi zinazoenezwa na CCM ni dhaifu na zimeshindwa kuidhoofisha Chadema.

Alisema kuwa wananchi wamezishtukia propaganda hizo na kwamba, wananchi wengi wamehamasika kutaka mabadiliko.
Katika harambee hiyo zaidi ya Sh270 milioni zilipatikana, kati ya hizo Sh250 milioni zikiwa ni ahadi na Sh20 milioni zikiwa ni fedha taslimu.
Kati ya fedha hizo, Sh20 milioni zilichangwa na tawi la Chadema nchini Marekani likiwa na majimbo yake Washington DC, Maryland na Virginia.

Watendaji wa Serikali
Kivutio kikubwa kilikuwa kwa baadhi ya watendaji wa Serikali kuchangia katika harambee hiyo na kutaka waitwe Wasamaria wema bila kutaja majina yao.

Mbowe alisema: “Kwa kuwa wananchi wametuamini, tumeacha njia ya maandamano na sasa tunataka kufika kila kata ya nchi hii ili kufikisha ujumbe wa mabadiliko kwa wananchi. "

Alisema kuwa wamekubaliana baada ya kumalizika kwa kikao cha Bunge wabunge wote wa Chadema watasambaa nchi nzima kueneza Vuguvugu la Mabadiliko.
Mwenyekiti huyo wa Chadema alisema kuwa mbali ya kufika kwenye kila kata chama hicho pia kimejipanga kufikisha ujumbe huo katika nchi zote ambako kuna Watanzania.

“ Hatuna mchezo sasa, tumejipanga kuchukua dola ifikapo 2015, hawa CCM sasa ni kama wanaweweseka hawajui wanalolifanya, tutawang’oa tu, ” alisema Mbowe.

Alisema kuwa chama hicho kikifanikiwa kuchukua dola, kipaumbele kikubwa kitakuwa ni kuboresha elimu ambayo ni sekta muhimu kwa maendeleo ya taifa.

“ Kipaumbele namba moja, mbili hadi tatu kitakuwa ni elimu. Tutawekeza zaidi kwenye elimu ili kuwawezesha wananchi kuhimili changamoto za dunia ya sasa hasa katika usimamizi wa rasilimali zao,” alisisitiza Mbowe.
Aliwahimiza watu wanaokichangia chama hicho kwa kuficha majina yao kuacha hofu akisema: “Jitokezeni hadharani, hamna sababu ya kuhofu kama kweli mnahitaji mabadiliko. Tumepuuzwa, tumenyanyaswa na tumedhalilishwa kiasi cha kutosha, sasa basi tuache woga.”

Alisema kuwa, CCM imeshindwa kuwasikiliza madaktari, walimu na wafanyakazi wengine lakini Chadema inaahidi kushughulikia matatizo ya makundi hayo.
Akizungumzia umuhimu wa harambee hiyo, Mbowe alisema mabadiliko yana gharama zake na kwamba wadau ndiyo wanapaswa kuchangia chama hicho.
Mbowe aliomba kila mpenda mabadiliko kuchangia kwa kadri ya uwezo wake na kwamba fedha zake zitailetea mabadiliko nchi hii.

Vyeo
Akizungumzia suala la nafasi za uongozi ndani ya chama hicho, Mbowe alisema kuwa, huu si wakati wa kugawana vyeo wala kutangaza nafasi za kugombea bali kukiimarisha chama ili kiweze kuwa na nguvu zaidi.
Naye Mwenyekiti wa M4C, Mkoa wa Dar es Salaam, Alex Mayunga alisema harambee hiyo ilikuwa na lengo la kukusanya Sh5 bilioni katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Alisema katika hafla ya jana walipanga kupata Sh500 milioni, lakini hazikutimia kutokana na msongamano wa wananchi waliokuwa wakituma fedha kwa njia ya simu za mkononi.

“Tunadhani hadi kesho (leo) kiasi hicho kitatimia kwa sababu wananchi wengi wametuma fedha lakini bado hazijatufikia,” alisema Mayunga.
Aliwataka wananchi kutuma fedha kwa kutumia njia ya simu za mkononi kwa sababu hiyo ndiyo njia rahisi. 

                      Chanzo.www. mwananchi.co.tz