Wednesday, August 15, 2012

Tyson Chandler Nyota wa Kikapu Nchini USA Atua Jijini Dar es Salaam

 
Picha Juu Tyson akiwa Don Bosco wakati wa mafunzo kwa vijana wadogo/watoto wa mitaani na picha nyingine ni Mkurugenzi wa Michezo na Ushirikiano wa UNICEF USA akiwa na Magesa/TBF-VP.
---
Nyota wa Kikapu, Tyson Chandler Mchezaji mahiri wa kikapu toka Marekani anayechezea timu ya New York Knicks kama "center" na pia anachezea timu ya Taifa ya Marekani yuko jijini Dar Es Salaam kwa ziara maalumu.

Tyson yumo kwenye timu ya Taifa ya Marekani iliyotwaa medali ya dhahabu katika mashindano ya Olimpiki ya 2012 yaliyomalizika London na alicheza michezo yote.


Tyson ambaye msimu huu wa ligi ya NBA iliyoisha alichaguliwa kuwa mchezaji bora  mzuiaji/Mlinzi (NBA Defensive Player of the year) pia ni balozi wa heshima wa UNICEF.


Katika ziara ya Dar amefanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo kutoa mafunzo ya kikapu kwa vijana wadogo/ watoto wa mitaani katika viwanja vya Don Bosco.


Tunamshukuru sana Tyson na pia tunawashukuru UNICEF kwa ushirikiano wao.


Phares Magesa

Makamu wa Rais,
Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania(TBF).

Kwetu Pazuri: Haya ndio Maeneo ya kupumzikia jijini Dodoma


Eneo la mzunguko,lina mandhari nzuri sana hasa kupigia picha za aina mbalimbali.
Nyerere square ni sehemu maarufu watu wanapumzika na kupiga picha za aina Mbalimbali,jijini Dodoma.
Watu wakipumzika na kutafakari maisha mazuri ya Kitanzania.
Huu ndio mnara wa sanamu ya Baba wa Taifa la Tanzania , Mwalimu Julius Kambarage Nyerere uliopo jijini Dodoma.

RAISI DR. JAKAYA KIKWETE AZINDUA AWAMU YA TATU YA TASAF JIJINI DODOMA LEO.


Dr. Jakaya Kikwete akikagua mabanda ya TASAF,katika uzinduzi wa awamu ya tatu ya TASAF yenye kauli mbio “Mpango wa Kunusuru kaya maskini zilizo katika mazingira hatarishi” Jijini Dodoma leo.
Dr. Jakaya Kikwete akikagua na kupata maelezo katika mabanda ya TASAF,katika uzinduzi wa awamu ya tatu ya TASAF yenye kauli mbio “Mpango wa Kunusuru kaya maskini zilizo katika mazingira hatarishi” Jijini Dodoma leo.
Dr. Jakaya Kikwete akikagua mabanda ya TASAF, akiongozana na spika wa bunge la Tanzania,Mama Anne Makinda,katika uzinduzi wa awamu ya tatu ya TASAF yenye kauli mbio “Mpango wa Kunusuru kaya maskini zilizo katika mazingira hatarishi” Jijini Dodoma leo.
Dr. Jakaya Kikwete akikagua na kupewa maelezo ya kina kuhusu bidhaa yanayofadhiliwa na TASAF,katika uzinduzi wa awamu ya tatu ya TASAF yenye kauli mbio “Mpango wa Kunusuru kaya maskini zilizo katika mazingira hatarishi” Jijini Dodoma leo.
Dr. Jakaya Kikwete akipewa maelezo ya bidhaa kutoka Unguja katika mabanda ya TASAF,katika uzinduzi wa awamu ya tatu ya TASAF yenye kauli mbio “Mpango wa Kunusuru kaya maskini zilizo katika mazingira hatarishi” Jijini Dodoma leo.
Dr. Jakaya Kikwete akipewa maelzo ya zulia katika mabanda ya TASAF,katika uzinduzi wa awamu ya tatu ya TASAF yenye kauli mbio “Mpango wa Kunusuru kaya maskini zilizo katika mazingira hatarishi” Jijini Dodoma leo.
Dr. Jakaya Kikwete akikagua mabanda ya TASAF,katika uzinduzi wa awamu ya tatu ya TASAF yenye kauli mbio “Mpango wa Kunusuru kaya maskini zilizo katika mazingira hatarishi” Jijini Dodoma leo.
Dr. Jakaya Kikwete akikagua mabanda ya TASAF,katika uzinduzi wa awamu ya tatu ya TASAF yenye kauli mbio “Mpango wa Kunusuru kaya maskini zilizo katika mazingira hatarishi” Jijini Dodoma leo.
Dr. Jakaya Kikwete akipata maelezo kutoka kwa mwakilishi wa TASAF katika mabanda ya TASAF,katika uzinduzi wa awamu ya tatu ya TASAF yenye kauli mbio “Mpango wa Kunusuru kaya maskini zilizo katika mazingira hatarishi” Jijini Dodoma leo.

Dr. Jakaya Kikwete akisikiliza kwa kina maelezo kutoka kwa mwakilishi wa TASAF katika mabanda ya TASAF,katika uzinduzi wa awamu ya tatu ya TASAF yenye kauli mbio “Mpango wa Kunusuru kaya maskini zilizo katika mazingira hatarishi” Jijini Dodoma leo.
Dr. Jakaya Kikwete akiangalia mmoja wa wanachama wa TASAF akilipwa mafao yake katika mabanda ya TASAF,katika uzinduzi wa awamu ya tatu ya TASAF yenye kauli mbio “Mpango wa Kunusuru kaya maskini zilizo katika mazingira hatarishi” Jijini Dodoma leo.
Dr. Jakaya Kikwete akimpongeza mmoja wa wanachama mkongwe wa TASAF akilipwa mafao yake katikamabanda ya TASAF,katika uzinduzi wa awamu ya tatu ya TASAF yenye kauli mbio “Mpango wa Kunusuru kaya maskini zilizo katika mazingira hatarishi” Jijini Dodoma leo.
Dr. Jakaya Kikwete akisikiliza maelezo kutoka kwa mwakilishi wa TASAF ,nyuma ni spika wa bunge Mama Anne Makinda,katika uzinduzi wa awamu ya tatu ya TASAF yenye kauli mbio “Mpango wa Kunusuru kaya maskini zilizo katika mazingira hatarishi” Jijini Dodoma leo.
Dr. Jakaya Kikwete akielekea jukwaa kuu,akiongozana na spika wa bunge Mama Anne Makinda, katika uzinduzi wa awamu ya tatu ya TASAF yenye kauli mbio “Mpango wa Kunusuru kaya maskini zilizo katika mazingira hatarishi” Jijini Dodoma leo. 

AKUTWA AMEFARIKI NDANI YA BASI LA UPENDO MOROGORO


Mwandishi wetu, Morogoro Yetu

Abiria mmoja aliyekuwa akisafiri kwa basi la kampuni ya Upendo lililokuwa likitokea jijini Mbeya kuelekea dar es salaam, amegunduliwa kufariki dunia ghafla, baada ya basi hilo kufika mjini Morogoro.

Mwili wa abiria huyo ambaye tiketi aliyokuwa nayo mfukoni imemtambulisha kama Petro Mrenge Sins, anayedaiwa kuwa mwenyeji wa Mkoa wa Tabora, umekutwa umelala katika viti vya chini, nyumba ya basi hilo la abiria, ambapo baada ya upekuzi, amekutwa akiwa na mfuko wa nailoni maarufu kama rambo uliokuwa na nguo zake kadhaa, shilingi elfu nne na tiketi ya basi.

Madereva wa basi hilo la Upendo, Marco Paulo na msaidizi wake Juma Abdul, wamedai wamegundua kufariki kwa abiria huyo, baada ya kufika, kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani cha msamvu mkoani Morogoro, ambapo walitangaza abiria wanaoshuka wafanye hivyo, lakini hakufanya hivyo na kuambiwa abiria huyo alionekana kukosa fahamu, ambapo walitoa taarifa kwa askari waliopo kituoni hapo, na mwili wake kushushwa kituo kikuu cha polisi cha mjini morogoro.

Abiria waliokuwa wakisafiri na mzee huyo aliyepoteza maisha, ambaye kiumri anakadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 60 hadi 70, tangu majira ya saa 12 afajiri kutokea mbeya, Josephat Mahaulane na Winfrida Andrew, wamedai kufahamiana na mzee huyo tangu jumatatu jioni ambapo alisaidiwa kwa kuchangiwa fedha na wauza matunda wa soko kuu la mjini mbeya na abiria waliokuwa kituo kikuu cha mabasi, baada ya kudai hakuwa na uwezo wa kusafiri.

Aidha wamedai abiria huyo alieleza kutaka kuja mjini Morogoro ambako angeweza kuonana na ndugu, jamaa na marafiki zake, ambao wangemuwezesha kuelekea mkoani tabora.

Mwili wa marehemu huyo ambao pia umekutwa na karatasi ya polisi inayoonesha alihitaji kusaidiwa kufika Morogoro, umepelekwa kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, ukisubiri kutambuliwa na taratibu nyingine za kiuchunguzi.

Habari na Morogoro yetu

Operesheni Sangara: CHADEMA Yavuna Wanachama Wapya Ulanga Mashariki.


Wapenzi na Washabiki wa Chadema wakijiandikisha na Kuchukua kadi mpya za uanachama Ulanga Mashariki, Kijiji cha NkonongoPicha Zote na CHADEMA
 Katibu Mkuu wa BAVICHA taifa Bw Deo Munisi akiwa na Mkuu wa shule kijijini Nkonongo wakiangalia hali halisi ya ubora wa shule ilivyo.
Katibu Mkuu wa BAVICHA taifa Bw Deo Munisi akiwa na Mkuu wa shule kijijini Nkonongo wakiangalia hali halisi ya ubora wa shule ilivyo

Picha Zote na CHADEMA

USAJILI TANZANIA: KIJUE KIKOSI CHA MAUAJI CHA YOUNG AFRICANS (YANGA) MSIMU HUU


Young Africans imewasilisha jumla ya majina ya wachezaji  28 kwa shirikisho la soka nchini TFF, kwa ajili ya msimu mpya wa ligi kuu nchini inayotazamiwa kuanza mapema septemba mosi.

Katibu mkuu wa Young Africans Mwesigwa Selestine amesema wamepeleka majina ya wachezaji wote 28 kwa ajili ya msimu mpya wa ligi kuu, na hii ni kutokana na benchi la ufundi kuridhia kuwatumia wachezaji wote.


Aidha katika usajili huo uliowasilishwa leo, umeambatana na usajili wa wachezaji wa timu ya vijana U-20 ambapo majina ya wachezaji mahiri wa timu ya Taifa Saimon Msuva na Frank Domayo.
Usajili  kamili kwa timu ya wakubwa ni kama ifuatavyo:
Walinda Mlango:
Yaw Berko, Ally Mustafa 'Barthez' na Said Mohamed 
Walinzi wa pemebeni:
Shadrack Nsajigwa, Godfrey Taita, Juma Abdul, Oscar Joshua, David Luhende na Stephano Mwasika
Walinzi wa kati:
Nadir Haroub 'Cannavaro', Kelvin Yondan, Mbuyu Twite, Ibrahim Job na Ladislaus Mbogo
Viungo wa ulinzi:
Athuman Idd 'Chuji', Juma Seif Kijiko na Salum Telela
Viungo wa pembeni:
Nizar Khalfani, Shamte Ally, Idrisa Rashid na Omega Seme 
Viungo washambuliaji:
Haruna Niyonzima, Rashid Gumbo na Nurdin Bakari 
Washambuliaji:
Said Bhanaunzi, Hamis Kiiza 'Diego', Didier Kavambagu na Jeryson Tegete

Majina hayo yanakamilisha jumla ya 28 ya wachezaji kwa timu ya wakubwa.
Kikosi cha U-20 kina jumla ya majina 22 ambao ni:
Walinda Mlango: Geofrey Nyalusi na Yusuf Abdul
Walinzi: Said Manduta, Zuberi Juma, Said Mashaka, Benson Michael, Issa Ngao, Rashid Said
Viungo: Frank Domayo, Omary Nasry, Clever Charles, Mwinyi Bakari, Mpenda Abdallah 
Washambuliaji wa pembeni: Abdulahman Ally, Hussein Moshi, Abdallah Salum, Rehani Kibingu
Washambuliaji: Saimon Msuva, George Banda, Notikely Masasi, Suleiman Ussi, Kassim Jongo 
NB: Frank Domayo & Saimon Msuva usajili wao umepelekwa katika usajili wa U-20 lakini wataitumikia timu ya wakubwa 

www.youngafricans.co.tz

Dk. Slaa afanyiwa ‘umafya’

Meneja wa hoteli amnyang`anya chumba

 Umeme wakatika, Tanesco wakana hujuma

 
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibroad Slaa
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibroad Slaa, amefukuzwa katika nyumba ya kulala wageni ndani ya Chuo cha Ufundi Stadi (Veta) Mikumi, Wilaya ya Kilosa, mkoani Morogoro, kwa kile kilichoelezwa kuwa ni sababu za kisiasa ikiambatana na kuzimwa kwa umeme kwa mji mzima kwa saa zaidi ya 12 ili kudhibiti mikutano yake ya hadhara anayoifanya.

Dk. Slaa ambaye aliwasili majira ya saa 8.00 mchana mjini Mikumi akitokea tarafa ya Malinyi, wilayani Ulanga, Morogoro, katika Operesheni ya Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) ikiwa ni mwendelezo wa Operesheni Sangara, alifikwa na udhalilishaji huo baada kuonyeshwa chumba chake lakini baadaye akanyang’anywa.

Baada ya kuwasili hotelini hapo, Dk. Slaa alikabidhiwa funguo ya sehemu ya kufikia kutoka kwa Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare, na kuingia chumbani, muda mfupi baada ya kuingia katika chumba hicho alitokea meneja wa hoteli hiyo, Jacob Sumary, na kumueleza kuwa sehemu hiyo imeshawekewa ‘oda’ na wateja wengine na hivyo kutakiwa kuondoka katika eneo hilo mara moja.

Hata hivyo, Dk. Slaa alihoji sababu za mmoja wa walimu wa Veta kuacha majukumu yake na kujipa jukumu la kuhudumia hoteli kwa kumhudumia eneo lenye vyumba vitatu lenye thamani ya Sh. 75,000 kwa kila chumba kimoja Sh. 25,000.

Meneja huyo alishikilia kumtaka Dk. Slaa aondeke hotelini hapo kwa kuwa yeye hakuwa na taarifa za ujio wake. Dk. Slaa alitii na kuondoka.

Naye Sumary alipofuatwa na NIPASHE jana kwenye hoteli hiyo kuzungumzia kitendo cha kumnyang’anya Dk. Slaa malazi, alikataa kuzngumzia suala hilo.

Awali alisikiliza NIPASHE ikimuuliza juu ya hatua alizochukua na kutaka kujua ni kwa nini, lakini alisema hawezi kuzungumzia suala hilo na kukata simu yake.

Akizungumzia hali hiyo katika mkutano wa hadhara, Dk. Slaa alisema kuna mipango imefanywa kwa nia ya kumdhoofisha katika kampeni za kuwakomboa Watanzania.

“Kama mimi nafanyiwa mambo hayo kwa suala dogo la malazi tu na serikali ya CCM, je nyinyi wengine mtafanyiwaje? Mnapaswa kujifikiria mara mbili,” alisema Dk. Slaa.

Ghafla umeme ulizimwa katika mji wa Mikumi hali iliyotafsiriwa kuwa ni muendelezo wa hujuma zinazofanywa dhidi ya Chadema, kwani wananchi walidai mji huo haukuwa na tatizo la umeme.

“Watanzania wa leo siyo wa jana. Zimeni umeme. Hata mfanye nini tutaendelea na mkutano na wananchi watatusikiliza tu. Lakini nitakula nao sahani moja waliofanya hivi,” alisema Dk. Slaa.

Hata hivyo, kukatika kwa umeme huo kuliongeza mori kwa wakazi wa Mikumi kutokana na kuongezeka kwa wingi katika mkutano huo na kukemea vitendo vilivyofanywa na serikali dhidi ya Dk. Slaa.

Akizungumza kwa njia ya simu na NIPASHE, Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Mkoa wa Morogoro, Deogratius Ndamugaba, alisema kukatika kwa umeme kulitokana na hitilafu za kawaida na siyo hujuma au msukumo wa kisiasa.

“Kukatika kwa umeme Mikumi siyo kwa sababu ya Chadema ila ni feeder ya Mikumi iko nje tangu saa 12.45 jioni. Nguzo imeanguka na inapaswa kubadilishwa na sehemu yenyewe ni porini. Kuna giza na Chui,” alisema Ndamugaba.

Alisema amekuwa akijaribu kuwasiliana na vyombo vya habari ili kuwapa taarifa wananchi wa Mikumi.

Alisema utendaji kazi wa eneo hilo kwa muda huo ulionekana kuwa mgumu na kwamba, tayari mafundi wa Tanesco walikuwa katika eneo la tukio kufanya marekebisho.

chanzo: NIPASHE

BODABODA YAGONGA DALADALA JIJINI DAR ES SALAAM, DEREVA WAKE AFA PAPOHAPO

 
 Baadhi ya watu wakiangalia ajali ya daladala lenye namba za usajili T 871 BGY linalofanya safari zake kati ya Mwenge na Temeke lililogongana na pikipiki katika makutano ya barabara ya Chang’ombe na Nyerere jijini Dar es Salaam leo.Picha Zote na Mdau Francis Dande

SIMBA SC KUWATAMBULISHA PHILIP OCHIENG NA DANIEL AKUFFO KWA WANAHABARI LEO

 

 
Salaam,
Tunawakaribisha kwenye mkutano wa waandishi wa habari leo saa sita kamili mchana kwenye ofisi za Makao Makuu ya Simba Mtaa wa Msimbazi jijini Dar es Salaam.
Dhima Kuu itakuwa ni utambulisho wa wachezaji wetu wapya wawili; Philip Ochieng na Daniel Akuffo.
Msikose tafadhali.
Ezekiel Kamwaga
Ofisa Habari
Simba SC

Special One Mourinho wants to be known as the "Only One"

The 49-year-old tactician revealed he should be called the "Only One" considering the long list of title he has won during his managerial career to date

Jose Mourinho - Real Madrid
 
Jose Mourinho - Real Madrid
Jose Mourinho believes he should be labelled the “Only one” instead of the “Special One”, after becoming the only coach to win the so-called top-three European Leagues.
Speaking to Portuguese television channel SIC on Monday, Mourinho explained that as his managerial career has progressed, he has become less selfish and less focused on individual goals.
"Things have been going well for me, thank God,| he told the station. "I am focused on others much more these days. The pleasure of winning with Inter Milan was seeing a club, which had not won for 50 years, winning again.
"That is what entices me more and more, instead of pursuing individual goals."
Mourinho won La Liga last season with current club Real Madrid, he won Serie A twice with Inter, the Premier League twice with Chelsea and the Portuguese Liga twice with Porto. On top of all that, he also won the Champions League with both Porto and Inter.
"Like me or not, I am the only one who won the world's three most important leagues. So, maybe instead of the 'Special One', people should start calling me the 'Only One'," Mourinho said in the interview that aired on Monday.
The Real Madrid boss was nicknamed “The Special One” during his time in England after calling himself just that during a press conference following his switch from Porto to the Blues in 2004.
Real Madrid kicks off the new campaign with a clash with arch rival Barcelona in the Spanish Super Cup on Aug. 25.

TFF yamkataa Twite Simba, Yanga


 

Na Wilbert Molandi
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limesema halitambui usajili wa beki wa kati wa kimataifa wa Rwanda na APR, Mbuyu Twite (pichani).
Klabu kongwe za Yanga na Simba, hivi sasa zipo kwenye vita kali zikimgombea beki huyo ambaye awali ilidaiwa alisaini Simba kwa dola 30,000 (zaidi ya Sh milioni 45), kisha akapewa dola 50,000 (zaidi ya Sh milioni 75) na kusaini Yanga.
 Vita hiyo hivi sasa imeingia katika sura nyingine baada ya Simba kumwekea mawindo makali beki huyo ikiwemo kutishia kumshitaki kwa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).
Akizungumza na Championi Jumatano, Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah, alisema hadi hivi sasa hawajapokea jina la beki huyo kutoka kwa Simba wala Yanga.
Osiah alisema majina ya usajili waliyoyapokea hadi sasa ni ya Azam FC na Kagera Sugar pekee, hivyo wanashangaa wao TFF kuingizwa kwenye vita hiyo, wakidaiwa wanaihujumu Simba.
Alisema ili usajili ukamilike, lazima TFF ipate orodha ya wachezaji ambao klabu zimewasajili kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
“Ujue sisi tunashindwa kuelewa TFF tunaingizwa vipi katika suala la usajili wa Twite, kazi yetu ni kupokea orodha ya wachezaji ambao klabu imewasajili katika kipindi husika.
“Kama TFF tunasema hatutambui usajili wa Twite, hatujapokea jina lake kutoka kwenye klabu hizo zinazomgombea (Simba na Yanga), timu zilizowasilisha majina ya wachezaji wao ni Azam FC na Kagera Sugar tu,” alisema Osiah.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Mashindano ya TFF, Saad Kawemba, amezitaka klabu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Bara kuwa makini katika suala la usajili.
“Nawakumbusha viongozi wa klabu za ligi kufuata maelekezo ya usajili tuliyowapa katika kozi maalum ya kutumia TMS (mtandao wa usajili).
“Klabu inatakiwa kufanya mazungumzo na timu inayommiliki mchezaji, njia hiyo inasaidia kupata ukweli wa mkataba wake,” alisema Kawemba.

Patachimbika: Simba na Azam ni vita ya kisasi




 

Pichani: Mechi ya robo fainali ya Kombe la Kagame, ambapo Simba ililala 3-1.

Na Lucy Mgina

KLABU ya Mtibwa Sugar leo Jumatano itaingia mzigoni kupambana na Jamhuri ya Zanzibar katika mchezo mkali wa nusu fainali ya michuano ya Super 8, huku Simba ikiivana Azam.

Michezo yote hiyo itapigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam huku ule wa Mtibwa ukitacheza saa nane mchana.

Mashabiki wanasubiri mchezo huu kwa hamu kubwa na wanaamini kuwa utakuwa maalum kwa ajili ya kulipa kisasi cha mabao 3-1 ambacho Simba ilipata kwenye robo fainali ya Kombe la Kagame.

Akizungumza na Championi Jumatano, Meneja wa Mtibwa, David Gboya, alisema mechi hiyo itakuwa ngumu kutokana na kila timu kujiandaa vyema, ikiwa…

Unakumbuka Nini ? ? ?

JUMATANO YA LEO KATIKA MAGAZETI