Saturday, November 3, 2012

Jeshi latuhumiwa na mauaji ya vijana


Jeshi la Nigeria
Jeshi la Nigeria
Raia wameiambia BBC kuwa, vijana kadhaa wameuawa kwa kupigwa na wanajeshi wa serikali mjini Maiduguri, Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo.
Imamu mmoja ameiambia BBC kuwa vijana 11 kutoka mtaa anaoishi, wameuawa vijana wanne kati yao wakiwa wanawe wa kiume.
Mauaji hayo yanayodaiwa kufanywa na wanajeshi wa serikali, yametokea ambapo shirika la kutetea haki za kibinadam la Amnesty International, limeshutumu maafisa wa ulinzi wa serikali kwa kuwanyanyasa raia wakati walipowasaka wanamgambo wa Kiislamu.
Lakini msemaji wa jeshi katika eneo hilo la Maiduguri amekanusha madai hayo na kusema hana taarifa kuhusu tukio hilo.
Hata hivyo Luteni Kanali Sagir Musa, ameiambia BBC kuwa uchunguzi utaanzishwa kufuatia madai hayo.
Maiduguri ni ngome ya wapiganaji wa Kiislamu wa Boko Haram, ambao wanapambana na jeshi la serikali wakitaka sheria za Kiislamu maarufu kama sharia kutumika nchini humo.
Mamia ya watu wameuawa katika maeneo ya Kaskazini na Kusini mwa Nigeria, katika mashambulio yanayosadikika kutekelezwa na kundi hilo katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.
Ripoti ya shirika la Amnesty International iliyochapishwa hiyo jana, imesema kuwa wanajeshi hao wa serikali walihusika na visa vingi vya ukiukwaji wa haki za kibinadam, wakati wa operesheni zao za kuthibiti wapiganaji hao wa Boko Haram.
Malam Aji Mustapha, ambaye ni Imamu katika msikiti mmoja mjini Maiduguri, amesema, baada ya maombi ya Alhamisi asubuhi, wanajeshi walimkamata na kumpeleka pamoja na watoto wake hadi uwanja mmoja ambako watu wengine wanaendelea kuzuiliwa.
Amesema walipofika kwenye uwanja huo waliamriwa kulala chini huku maafisa hao, wakiwafanyia uchunguzi mmoja baada ya mwingine.

Bondia wa Tanzania abwagwa Afghanistan

  • Hamid Rahimi wa Afghanistan alishinda mchuano wa kwanza wa bondia wa kulipwa kuwahi kufanyika nchini humo

JUMAMOSI YA LEO KATIKA MAGAZETI

Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete: Azindua Taasisi Sayansi Na Teknolojia Ya Chuo Kikuu Cha Nelson Mandela Arusha

Rais Jakaya Kikwete, akikata utepe kuweka jiwe la Msingi ikiwa ni ishara ya kuzindua rasmi Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Chuo cha Kikuu cha Nelson Mandera, jijini Arusha, Novemba 02, 2012. Kushoto kwake ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mkuu wa Chuo hicho, Dkt. DMohammed Gharib Bilal. Kushoto ni Makamu wa Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Burton Mwamila
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mkuu wa Chuo cha Nelson Mandera, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti wa kumbukumbu wakati wa hafla ya uzinduzi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Chuo cha Kikuu cha Nelson Mandera, jijini Arusha , Novemba 02, 2012. Kulia ni Rais Jakaya Kikwete, aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo

 Rais Jakaya Kikwete, akifunua kitambaa ikiwa ni ishara ya kuzindua rasmi Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Chuo cha Kikuu cha Nelson Mandera, jijini Arusha, Novemba 02, 2012. Kulia kwake ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mkuu wa Chuo hicho, Dkt. DMohammed Gharib Bilal. Kulia ni Makamu wa Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Burton Mwamila.
 Rais Jakaya Kikwete, akipokea zawadi ya picha kutoka kwa Makamu wake na Mkuu wa Chuo cha Nelson Mandera, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Burton Mwamila, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Chuo cha Kikuu cha Nelson Mandera, jijini Arusha
                       
                                     Picha na OMR

Wednesday, October 24, 2012

MAGAZETI JUMATANO YA LEO











Foleni Ya Tazara Nusura Ilete Maafa

Kwenye mapishano ya barabara na reli TAZARA Dar es salaam,wakati treni linakaribia kukatisha barabara,foleni ikawa haitembei.hii ilitokea juzi jumatatu