skip to main |
skip to sidebar
HIVI NDIVYO VIWANGO VYA UBORA WA SOKA VYA FIFA - SPAIN KILELENI - ENGLAND YA TATU - BRAZIL YAZIDI KUSHUKA - TANZANIA NAFASI MOJA CHINI
Timu ya Taifa ya Spain imeendelea
kukalia kiti cha uongozi wa ubora wa soka kwa mujibu wa viwango vya
FIFA. Mabingwa ha wa dunia na ulaya wameshikilia uongozi huo wakiwa na
pointi 1605, nafasi ya pili imekamatwa na Ujerumani, England wameendelea
kupanda ubora kwenye rank hizo za FIFA bada ya mwezi uliopita kushika
nafasi ya nne.
Brazil mabingwa wa mara tano wa dunia
wameendelea kuweka rekodi, baada ya kushika nafasi ya chini zaidi katika
historia yake, wakikamata nafasi 13, ikiwa ni mara ya kwanza kushuka
kwa namna hiyo.
Ivory coast ndio pekee ya kiafrika
kuwemo ndani ya 20 bora, wakishika nafasi ya 16. Timu ya taifa ya
Tanzania imeshuka kwa nafasi moja kutoka nafasi ya 127 mpaka 128.
0 comments:
Post a Comment