Mabaki ya Helikopta mbili za Uganda ambazo ziliripotiwa kutoweka siku ya Jumapili zimepatikana mashambani nchini kenya.
Kanali Cyrus Oguna ambae ni msemaji wa jeshi la Kenya amesema hatma ya watu 14 waliokuwemo ndani ya chombo hicho haijulikani.
Ndege
hizo mbili zilikuwa ni sehemu ya vifaa vilivyokuwa vikipelekwa nchini
Somalia kuongezea nguvu kikosi cha umoja wa Afrika kilichoko huko.
Helikopta ya tatu ambayo pia ilikuwa katika msafari huo ilitua kwa ghafla katika eneo la mlima Kenya siku ya Jumapili.
Kanali Oguna amesema wote waliokuwa katika helikopta hiyo ya tatu waliokolewa.
Ni helikopta moja peke yake ndio faulu kutua vizuri na kuongeza mafuta katika mji wa Garissa ulioiko kaskzzini mwa Kenya.
Helikopta
hizo nne ambazo zimetengezezwa Urusi ziliondoka siku ya Jumapili Uganda
zikelekea Somalia kabla ya kukumbwa na mkasa huo.
Masalia
ya helikopta hizo mbili ambazo awali ziliripotiwa kutoweka zilionekana
juu ya mlima Kenya na maafisa wa Shirika la Wanyama pori, limeripoti
gazeti la Daily Nation la Kenya.
Msemaji
wa jeshi Kanali Oguna ameimbia BBC kwamba kikosi cha jeshi la Kenya
linaelekea katika eneo hilo la Mlima Kenya , ambao ndio mlima wapili kwa
urefu ,afrika.
Afisa huyo amefafanua kwamba moja ya helikopta hizo imeharibika kabisa ilhali ya pili imeharibika kiasi.
Helikpta
hizo zilikuwa zinaelekea nchini Somalia kuongezea nguvu vikosi vya
Umoja wa Afrika ambavyo vinajitayarisha kuvamia mji wa Kismayo na
kuwafurusha wapiganaji wa Al Shabaab toka mji huo ambyo ndio ngome yao
kuu.
Chanzo: http://www.bbc.co.uk/swahili
0 comments:
Post a Comment