Friday, August 17, 2012

Waandamanaji wauawa Afrika Kusini


Policemen give instructions to an injured miner after the striking miners were shot outside a South African mine in Rustenburg, 100 kilometres northwest of Johannesburg, August 16, 2012.
                                  
Polisi nchini Afrika Kusini wamewaua wachimba migodi kadhaa na kuwajeruhi wengine wengi katika juhudi za kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wakilalamikia mishahara duni.
Mwandishi mmoja aliyekuwepo nje ya mgodi wa Lonmin Platinum wa Marikana aliambia BBC kuwa polisi walionekana kushambulia mfano wa siku za ubaguzi wa rangi.
Waliojeruhiwa walisafirishwa kwa helikopta hadi hospitalini.
Waandamanaji hao, wachimba migodi, walikuwa wakidai nyongeza ya mshahara wa Dola 1,500 kwa mwezi.
Polisi walisema mashauriano kati ya wawakilishi wa wafanyakazi wa Association of Mine Workers and Construction (AMCU) yalikwama na ikalizimika kuwatimua wafanyakazi hao kutoka mahali pale kwa nguvu.
Polisi walikuwa wakifanya maamuzi wakati ambapo wachimba migodi walikuwa wameshika mikononi silaha za kitamaduni na bunduki.
Rais Zuma amenukuliwa akisema kuwa amesikitishwa sana na mauaji hayo yasiyokuwa na maana. Chama cha upinzani cha upinzani cha Democratic Alliance limetoa wito Serikali kuunda tume ya kuchunguza kilichosababisha mauaji hayo.
Ghasia zilianza mapema juma hili baada ya makundi mawili ya kuwakilisha wachimba migodi kupigana na kusababisha vifo vya watu kumi, kukiwemo maafisa wawilai wa polisi.
Afrka Kusini ni taifa linalozalisha madini aina ya Platinum kwa wingi zaidi duniani.

Waziri Mkuu Asema Sheria Iliyotumika Kufunga Mwanahalisi Ni Halali.

NA: MAGRETH KINABO – MAELEZO, DODOMA
Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema kwamba mtu yoyote ambaye anona hakutendewa haki kuhusu kufungiwa kwa Gazeti la Mwanahalisi anaweza kufafuta utaratibu mwingine wa kwenda mahakamani.

Kauli hiyo ilitolewa leo Bungeni na Waziri Mkuu Pinda wakati akijibu swali la Kiongozi wa Kambi ya Upinzania Bungeni , Freeman Mbowe lililouliza kuwa Julai 30, mwaka huu, Serikali ililifungua gazeti la Mwanahalisi kwa muda usiojulikana kwa kutumia sheria ya magazeti ya mwaka 1976.

Maadam katika siku za hivi karibuni serikali imetambua umuhimu wa mahakama ni

Kwanini wamelifungua gazeti hili badala ya kulipeleka mahakamani na wahusika wapate nafasi ya kujitetea kabla ya kuhukumiwa?

Akijibu swali hilo , Waziri Mkuu Pinda alisema "ni kweli serikali imechukua hatua hiyo, lakini imechukua hatua hiyo kwa kuzingatia sheria na taratibu za nchi na mtu yoyote kwa msingi wa sheria hiyo kama anaona hajatendewa haki ni juu yake kutafuta utaratibu mwingine wa kwenda mahakamani,” alisema Waziri Mkuu Pinda.

Katika swali lake la nyongeza la kiongozi huyo lililouliza kuwa Sheria iliyotumika imekuwa ikilalamikiwa na wadau wengi na vyombo vya habari kwa muda mrefu . Je wewe huamini kwa kutumia sheria hiyo ni kunyima haki na ni msisitizo wa utawala usio bora?

Akijibu swali hilo Waziri Mkuu Pinda alisema “ Mimi siamini hivyo kwa sababu sheria hiyo imetungwa na Bunge tukufu na kuwa bado inatumia ni sheria halali, sisi tutaendelea kuitumia mpaka hapo itakapobadilishwa.

IJUMAA YA LEO KATIKA MAGAZETI


















Thursday, August 16, 2012

Majambazi wapora Sh. milioni 65 Dar

 
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela
Watu wanne wanaodaiwa kuwa ni majambazi wamepora Sh. milioni 65 kwenye kiwanda cha kutengeneza kinywaji cha Sayona, kilichopo eneo la Mwenge, jijini Dar es Salaam.
Tukio hilo lilitokea saa 8:00 machana baada ya majambazi hao kufyatua  risasi mara tatu hewani mfululizo kwa wakiwa wamesimama mbele gari la kiwanda  kiwanda hicho lililokuwa likitoka nje kupeleka pesa hizo kwa mhasibu wa kampuni ya M.M inayoshughulika na utengenezaji wa vifaa vya ujenzi.
Meneja masoko wa kampuni hiyo, Ragu Gadabi, alisema walinzi wake walimfungulia geti na kutoka nje ili kuwahisha pesa hizo. Alisema kuwa hatua chache nje ya geti, gari lenye  namba T640 MBZ aina ya RAV4 lilisimama mbele yake na kisha mtu mmoja alishuka na kugonga dirisha la gari lake.
“Sikuweza kufungua dirisha, lakini nilisikia milio ya risasi ikishambulia gari hilo, nilifanikiwa kutoka kwenye gari na kurudi kiwandani, lakini pesa na Laptop zote zimechukuliwa,” alisema na kuongeza: “Nilirudi kiwandani haraka kunusuru maisha yangu la sivyo wangepoteza uhai wangu, kitendo kilikuwa cha haraka mno yaani kufumba na kufumbua,” alisema Ragu.
Shuhuda ambaye hakupenda kutaja jina lake liandikwe gazetini, alisema majambazi hao walitokea barabara ya ITV na mara walipofika karibu na kiwanda hicho walisimama. Alisema muda mfupi baadaye aliliona gari likitoka kiwandani na kisha gari lililokuwa limesimama likalikinga gari hilo na kuanza kufyatua risasi na kufanikiwa kuchukua pesa na kompyuta ndogo.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwa Jeshi la Polisi linaedelea kulifanyia kazi.
“Nimepata taarifa hizo, lakini kwa sasa nipo nyumbani kwani hali yangu siyo nzuri kiafya, lakini vijana wangu wa kazi wanaedelea kuifanyakazi hiyo,” alisema.
CHANZO: NIPASHE

Benki Ya KCB Yatoa Msaada Wa Madawati Kwa Shule Ya msingi Ujirani Manispaa Ya Morogoro



Meneja wa Benki ya KCB Tanzania tawi la Morogoro, Carlos akiteta jambo na wazazi wa wanafunzi wa  shule ya msingi Ujirani iliyopo kijiji cha  Kienge B katika Kata ya Mkundi Manispaa ya Morogoro,baada ya kukabidhiwa msaada wa madawati 80 yenye thamani ya shilingi milioni 4.8.

Meneja wa Benki ya KCB Tanzania tawi la Morogoro, Carlos akiteta jambo na wazazi wa wanafunzi wa  shule ya msingi Ujirani iliyopo kijiji cha  Kienge B katika Kata ya Mkundi Manispaa ya Morogoro,baada ya kukabidhiwa msaada wa madawati 80 yenye thamani ya shilingi milioni 4.8.
Meneja wa Benki ya KCB Tanzania tawi la Morogoro, Carlos Msigwa wa pili kutoka (kulia) akipongezwa na Mkuu wa shule ya msingi ya Ujirani Philemon Kibuja, iliyopo kijiji cha  Kienge B katika Kata ya Mkundi Manispaa ya Morogoro,baada ya kukabidhiwa msaada wa madawati 80 yenye thamani ya shilingi milioni4.8. na benki ya KCB Tanzania,wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Mshauri wa shule Godfrey Tairo na Mwalimu wa kujitolea Lazaro Isondo.

Meneja wa Benki ya KCB Tanzania tawi la Morogoro, Carlos Msigwa akisalimiana na mmoja wa wanafunzi wa wanafunzi wa shule ya msingi ya Ujirani iliyopo kijiji cha  Kienge B katika Kata ya Mkundi, Manispaa ya Morogoro,baada ya kukabidhi msaada wa madawati 80 yenyethamani ya shilingi milioni4.8 kwa shule hiyo.
Meneja wa Benki ya KCB Tanzania tawi la Morogoro Tanzania , Carlos Msigwa akipongezwa na Diwani wa kata ya Mkundi Emelda Chambo, baada ya kumkabidhi  msaada wa madawati 80 yenye thamani ya shilingi milioni 4,8  kwa ajiri ya shule ya msingi ya Ujirani iliyopo kijiji cha  Kienge B, Manispaa ya Morogoro.
Afisa Masoko wa Benki ya KCB Tanzania tawi la Morogoro,Herieth Mwakifulefule akimsaidia kumvisha kiatu Kulwa Mussa, ambaye ni Mwanafunzi wa darasa la Tatu katika shule ya msingi ya Ujirani ya jamii ya wamasai iliyopo katika kijiji cha Kienge B, baada ya benki hiyo kutoa msaada wa madawati 80 yenye thamani ya shilingi milioni4.8. mtoto huyo tangu darasa la kwanza amekuwa akishika nafasi ya kwanza katika darasa lao.

BENKI ya KCB Tanzania imetoa msaada wa madawati 80 yenye thamani ya shilingi milioni nne na laki nane (4.8m) kwa shule ya msingi Ujirani iliyopo katika kata ya Mkundi manispaa ya Morogoro.

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya madawati hayo, Meneja wa KCB Tawi la Morogoro Carlos Msigwa alisema kuwa lengo la msaada huo lilikuwa kusaidia upungufu wa madawati katika shule hiyo na hivyo kuwawezesha wanafunzi kusoma vizuri

Meneja huo alisema kuwa Benki ya KCB inatambua umuhimu wa elimu bora katika maendeleo ya taifa na ndiyo maana haikusita kuelekeza msaada huo katika sekta ya elimu.

Akipokea msaada huo, diwani wa kata ya Mkundi Emelda Chambo aliishukuru Banki ya KCB kwa kutoa msaada na kusema kuwa utakuwa chachu kubwa katika maendeleo ya elimu katika shule hiyo ambayo inakabiliwa na upungufu mkubwa wa madawati.

Tuaishukuru sana KCB kwani wamekuwa kama walezi kwa shule yetu. Hii ni mara ya tatu kupokea msaada baada ya ule wa miti ya kivuli pamoja na vitabu.Tunaahidi kuyatunza madawati haya ili mtakaporudi tena myakute katika hali nzuri.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo Philemon Kibuja shule hiyo yenye wanafunzi 400 imekuwa ikikabiliwa na changamoto nyingi ikiwamo ukosefu mkubwa wa madawati.

“Mimi ndiyo mwalimu mkuu na mwalimu pekee katika shule hii. Nafundisha kuanzia darasa la kwanza hadi la saba. Shule hii kabla ya kupata msaada huu kutoka KCB haikuwa na dawati hata moja. Wanafunzi walilazimika kukaa chini, kwenye magogo na kwenye mabenchi,’ alisema

Mwalimu huyo aliishukuru Benki ya KCB na kuomba serikali pamoja na makampuni binafsi kuidia shule hiyo ambayo wanafunzi wengi wanatoka katika jamii za wafugaji.

“Shule hii yenye wanafunzi 400 ina madarasa matatu tu na mwalimu ni mimi peke yangu. Pamoja na jitihada kubwa ya kuomba msaada serikalini, serikali haijaweza kutusaidia. Tunaomba mashirika mbalimbali kujitikeza kutusaidia,” alisema
chanzo: Mjengwa

Bus La Muhamed Trans Lapata Ajali Km 15 Kutoka Bukoba Mjini


RPC Kelenge kulia akijadili jambo na RTO  Willy eneo la tukio
     Bus la muhamed trans lenye nambari  T884 likiwa limepinduka
Lori lenye nambari  T814 liliokua baada ya kugongwa na bus kwa kutokea nyuma.


Ajali hii imetokea asubuhi ya leo majira ya saa moja kasoro ni eneo la kyetema km 5 kabla ya kifika kemondo na ni umbali wa km 15 kutoka bukob mjini. Baada kwa kuligonga lori la mchanga  bus hilo lilikua likisafiri kutoka bukoba mjini kuelekea Mwanza, na abiria wote wamenusurika!

Picha kwa hisani ya:-
Bukobawadau
P. O.Box 316,
Bukoba – TANZANIA
Mobile:MC BARAKA GALIATANO +255 715 505043,
 SIR.LOOM   GALIATANO   +255 768 397241

WAPENZI WA ARSENAL WAKILIA NA KUSAGA MENO, KWA HASIRA WAFANYA HAYA


Muda mchache baada ya vilabu vya Arsenal na Man United kuthibitisha kwamba vimekubalina ada ya uhamisho wa mchezaji RobinVan Persie kujiunga na mashetani wekundu - baadhi ya mashabiki wa Arsenal wamekuwa wakipost picha mitandaoni kuonyesha namna walivyopokea taarifa za nahodha wao kwenda Old Traford. Wapenzi wa Arsenal vipi? KAMA YOYOTE AMBAYE ANATAKA KUONYESHA HASIRA ZAKE KAMA HAWA ATUME PICHA AU MAONI KWENYE EMAIL HII - shaffidauda@gmail.com

Chanjo ya Ebola huenda isipatikane


Virusi vya Ebola

Virusi vya Ebola
Wanasayansi wanaoendesha utafiti kuhusu virusi vinavyosababisha ugonga wa Ebola, wameiambia BBC kuwa, chanjo inayoweza kutumiwa kuzuia maambukizi ya virusi hivyo huenda isifumbuliwe.
Wiki chahche zilizopita idara ya ulinzi ya Marekani, Pentagon, ilisitisha ufadhili wake kwa kampuni mbili ambazo zilikuwa zikiendesha utafiti huo.
Mmoja wa wataalamu katika jopo hilo amesema kuna uwezekano mkubwa wa chanjo hiyo itakayotumiwa kuzuia mkurupuko wa ugonjwa wa Ebola haitatumika.
Ugonjwa wa Ebola umetajwa kama moja ya magonjwa hatari na ya kuogofya zaidi ulimwenguni.
Virusi hivyo vinasababisha homa kali ambayo hufanya mtu kuvuja damu katika viungo vya ndani na hata kupitia sehemu zingine kama vile masikio, mapua na hata ngozi.
Wataalamu wanasema virusi hivyo ambavyo hushambulia chembe chembe nyeupe na mishipa ya damu na kusababisha mwasho wa ngozi, macho mekundu, kutapika na mauimivu ya viungo.
Katika miezi ya hivi karibuni watu 16, waliaga dunia Magharibi mwa Uganda, kutokana na ugonjwa huo.
Kufikia sasa hakuna tiba kamili ya ugonjwa huo ambao unaweza kusababisha vifo kwa asilimia 90 ya watu walioambukizwa virusi hivyo.
Mikakati ya kujaribu kufumbua chanjo ya kutibu na kuzuia virusi vya Ebola imefadhiliwa na Idara ya Ulinzi na Taasisi ya Kitaifa ya Afya nchini Marekani NIH.
Idara hizo mbili zimewekeza mamilioni ya dola kwa utafiti huku zikiwa na wasi wasi kuwa virusi hivyo vinaweza kutumiwa kama silaha za kibiolojia.
Kutokana na ufadhili huo, chanjo kadhaa zimefumbuliwa na tayari zimefanyiwa majaribio kwa wanyama na matokeo yake yamekuwa ya kuridhisha.
Kampuni mbili Sarepta na Tekmira tayari zimeanzisha majaribio ya tiba hiyo kwa binadamu.
Lakini kampuni hizo zimefahamaishwa na Idara ya Ulinzi ya Marekani kusitisha utafiti huo mwa muda kutokana na ukosefu wa fedha.
Uamuzi wa mwisho kuhusu ikiwa ufadhili huo utarejelewa tena utatolewa mwezi ujao.

Syria yaondolewa kama mwanachama wa OIC


Ekmeledin Ihsanoglu wa OIC

Ekmeledin Ihsanoglu wa OIC
Jumuiya ya muungano wa nchi za Kiislamu (OIC) imesimamisha uanachama wa Syria katika muungano huo.
Baada ya kumalizika kwa mkutano wa viongozi wa Kiislamu uliofanyika mjini Mecca, katibu mkuu wa Muungano huo, Ekmeleddin Ihsa-noglu, alisema muungano huo wa mataifa ya kiislamu hauna nafasi kwa taifa ambalo serikali yake inawaua raia wake.
Hatua hiyo imesababisha kutengwa zaidi kwa Rais Bashar al-Assad baada ya jumuiya ya mataifa ya ki-arabu kuitimua mnamo mwezi Novemba.

Koffi Olomide ashitakiwa kwa kupigana



Koffi Olomide ashitakiwa kwa kupigana
Koffi Olomide, ambaye ni mwanamuziki mashuhuri barani Afrika ameshitakiwa kwa kumpiga Mtayarishaji wake wa muziki.
Mwanamuziki huyo alikamatwa na kufungiwa katika kituo cha polisi na kufikishwa mahakamani jumatano.
Koffi alikamatwa kufuatia vurugu katika hoteli moja mjini Kinshasa.
Waandishi wa habari wanasema mahakama hiyo ya Kinishasa ilifurika kutokana na watu wengi kuja kumuona kiongozi huyo wa bendi ya Quartier Latin akiwa kizimbani.
Kesi hiyo iliharishwa hadi Alhamisi asubuhi wakati atakaposhitakiwa rasmi.
Wakati wa kesi hiyo hapo jana Koffi Olomide aliwakilishwa na mawakili 10.
Ugomvi kati ya mwanamuziki huyo na mtayarishi wake Bwana , Diego Lubaki, ni kuhusu pesa dola $3,680.
Hakimu alimfahamisha mwanamuziki huyo ikiwa atapatikana na hatia huenda akafungwa jela miezi sita.
Olomide ni gwiji wa muziki aina ya "soukous", mtindo ulitokana na jina la kifaransa "secouer", lenye maana ya kujitikisa au kujinengua ,na wachezaji wake vile vile wanatambulika kwa kunengua maungo.