Meneja
wa Benki ya KCB Tanzania tawi la Morogoro, Carlos akiteta jambo na
wazazi wa wanafunzi wa shule ya msingi Ujirani iliyopo kijiji cha
Kienge B katika Kata ya Mkundi Manispaa ya Morogoro,baada ya kukabidhiwa
msaada wa madawati 80 yenye thamani ya shilingi milioni 4.8.
Meneja
wa Benki ya KCB Tanzania tawi la Morogoro, Carlos akiteta jambo na
wazazi wa wanafunzi wa shule ya msingi Ujirani iliyopo kijiji cha
Kienge B katika Kata ya Mkundi Manispaa ya Morogoro,baada ya kukabidhiwa
msaada wa madawati 80 yenye thamani ya shilingi milioni 4.8.
Meneja
wa Benki ya KCB Tanzania tawi la Morogoro, Carlos Msigwa wa pili kutoka
(kulia) akipongezwa na Mkuu wa shule ya msingi ya Ujirani Philemon
Kibuja, iliyopo kijiji cha Kienge B katika Kata ya Mkundi Manispaa ya
Morogoro,baada ya kukabidhiwa msaada wa madawati 80 yenye thamani ya
shilingi milioni4.8. na benki ya KCB Tanzania,wanaoshuhudia kutoka
kushoto ni Mshauri wa shule Godfrey Tairo na Mwalimu wa kujitolea Lazaro
Isondo.
Meneja
wa Benki ya KCB Tanzania tawi la Morogoro, Carlos Msigwa akisalimiana
na mmoja wa wanafunzi wa wanafunzi wa shule ya msingi ya Ujirani iliyopo
kijiji cha Kienge B katika Kata ya Mkundi, Manispaa ya Morogoro,baada
ya kukabidhi msaada wa madawati 80 yenyethamani ya shilingi milioni4.8
kwa shule hiyo.
Meneja
wa Benki ya KCB Tanzania tawi la Morogoro Tanzania , Carlos Msigwa
akipongezwa na Diwani wa kata ya Mkundi Emelda Chambo, baada ya
kumkabidhi msaada wa madawati 80 yenye thamani ya shilingi milioni 4,8
kwa ajiri ya shule ya msingi ya Ujirani iliyopo kijiji cha Kienge B,
Manispaa ya Morogoro.
Afisa
Masoko wa Benki ya KCB Tanzania tawi la Morogoro,Herieth Mwakifulefule
akimsaidia kumvisha kiatu Kulwa Mussa, ambaye ni Mwanafunzi wa darasa la
Tatu katika shule ya msingi ya Ujirani ya jamii ya wamasai iliyopo
katika kijiji cha Kienge B, baada ya benki hiyo kutoa msaada wa madawati
80 yenye thamani ya shilingi milioni4.8. mtoto huyo tangu darasa la
kwanza amekuwa akishika nafasi ya kwanza katika darasa lao.
BENKI
ya KCB Tanzania imetoa msaada wa madawati 80 yenye thamani ya shilingi
milioni nne na laki nane (4.8m) kwa shule ya msingi Ujirani iliyopo
katika kata ya Mkundi manispaa ya Morogoro.
Akizungumza
katika hafla ya makabidhiano ya madawati hayo, Meneja wa KCB Tawi la
Morogoro Carlos Msigwa alisema kuwa lengo la msaada huo lilikuwa
kusaidia upungufu wa madawati katika shule hiyo na hivyo kuwawezesha
wanafunzi kusoma vizuri
Meneja
huo alisema kuwa Benki ya KCB inatambua umuhimu wa elimu bora katika
maendeleo ya taifa na ndiyo maana haikusita kuelekeza msaada huo katika
sekta ya elimu.
Akipokea
msaada huo, diwani wa kata ya Mkundi Emelda Chambo aliishukuru Banki ya
KCB kwa kutoa msaada na kusema kuwa utakuwa chachu kubwa katika
maendeleo ya elimu katika shule hiyo ambayo inakabiliwa na upungufu
mkubwa wa madawati.
Tuaishukuru
sana KCB kwani wamekuwa kama walezi kwa shule yetu. Hii ni mara ya tatu
kupokea msaada baada ya ule wa miti ya kivuli pamoja na
vitabu.Tunaahidi kuyatunza madawati haya ili mtakaporudi tena myakute
katika hali nzuri.
Mwalimu
mkuu wa shule hiyo Philemon Kibuja shule hiyo yenye wanafunzi 400
imekuwa ikikabiliwa na changamoto nyingi ikiwamo ukosefu mkubwa wa
madawati.
“Mimi
ndiyo mwalimu mkuu na mwalimu pekee katika shule hii. Nafundisha
kuanzia darasa la kwanza hadi la saba. Shule hii kabla ya kupata msaada
huu kutoka KCB haikuwa na dawati hata moja. Wanafunzi walilazimika kukaa
chini, kwenye magogo na kwenye mabenchi,’ alisema
Mwalimu
huyo aliishukuru Benki ya KCB na kuomba serikali pamoja na makampuni
binafsi kuidia shule hiyo ambayo wanafunzi wengi wanatoka katika jamii
za wafugaji.
“Shule
hii yenye wanafunzi 400 ina madarasa matatu tu na mwalimu ni mimi peke
yangu. Pamoja na jitihada kubwa ya kuomba msaada serikalini, serikali
haijaweza kutusaidia. Tunaomba mashirika mbalimbali kujitikeza
kutusaidia,” alisema
chanzo: Mjengwa
0 comments:
Post a Comment