Kabla
ya kuanza kwa mgomo wa walimu, Mwenyekiti wa Tume ya Sensa na Makazi
aliwatangazia watanzania kuwa jumla ya walimu 150,000 sawa na asilimia
75 ya walimu wote watashiriki katika zoezi la sensa ya watu na makazi.
Kutokana
na mgomo wa walimu baadhi ya wakuu wa mikoa na wilaya wamewaondoa
walimu kwenye zoezi la sense kwa kile kinachoonekana kuwa ni maagizo
kutoka ofisi ya Waziri Mkuu.
Kwa
mujibu wa taarifa ya rais wa CWT Mwl. Gratian Mukoba, serikali
iliorodhesha majina ya walimu waliogoma na viongozi wa CWT kwa maelekezo
yanayodaiwa kutolewa na Kaimu Katibu Mkuu TAMISEMI Mwl. Jumanne
Sagiti.
Kutokana
na hatua hiyo, Chama kinawaomba wanachama wake waliogoma na kuondolewa
kwenye sensa kutokata tamaa kwa kukosa pesa ambazo zingewasaidia kwa
muda wa wiki moja tu.
Badala yake wajitambue kuwa uboreshaji wa maslahi yao utatokana na wao wenyewe.
0 comments:
Post a Comment