Mkenya David Lekuta Rudisha
ameibuka kuwa mwanariadha wa kwanza kuandikisha rekodi mpya kwenye
mashindano ya riadha katika michezo ya Olimpiki, inayoendelea jijini
London Uingereza na kisha kushinda medali ya dhahabu katika mbio za mita
mia mbili.
Akiwa anashiriki fainali ya michezo ya Olimpiki
kwa mara kwanza, Rudisha mwenye umri wa miaka 23 alinyakuwa ushindi huo
kwa kuwa mtu wa kwanza kukimbia umbali wa mita mia nane kunako dakika 1,
sekunde 40 nukta 91.Mwariadha wa Botswana Nijel Amos, umri 18, alinyakuwa medali ya fedha huku chipukizi mwingine kutoka Kenya Timothy Kitum, akiridhika na medali ya shaba.
Mwingireza Andrew Osagie alimaliza katika nafasi ya nane lakini akaweza kuandikisha muda bora wa dakika 1:43.77.
Rudisha ambaye ni bingwa wa dunia aliongoza katika mbio hizo tangu mwanzo hadi mwisho na kuwaacha wanariadha wenzake kwa tofauti ya sekunde 49.28. Kisha akafyatuka katika hatua za mwisho mwisho na kuivunja rekodi yake mwenyewe.
Huku kila mwanariadha akiwa na msukumo wa kasi ya rudisha, ni Abubakar Kaki wa Sudan tu ndiye aliyeshindwa kuandikisha muda wake bora licha ya kukamilisha mbio hizo katika nafasi ya saba.
Rudisha ameiambia BBC: "Lo! Nimefurahi sana. Huu ni wakati ambao nimekuwa nikisubiri kwa kipindi kirefu. Kuja hapa na kuivunja rekodi ya dunia ni kitu ambacho bado sijaamini.''
" Nilikuwa nimejiandaa na sikuwa na shaka kwamba nitashinda. Leo, hali ya anga ilikuwa nzuri na niliamua tu kuparamia taji hili."
Ushindi wa Rudisha bila shaka ni habari njema kwa Kenya ambayo kinyume na matarajio, ilikuwa imeandikisha matokeo duni katika michezo hiyo ya Olimpiki kwa kuwa na medali moja pekee ya dhahabu.
0 comments:
Post a Comment