Shirikisho
la Kimataifa la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea Hati ya
Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa wachezaji 11 wa nje kati ya 14
walioombea usajili na klabu mbalimbali za Ligi Kuu.
Wachezaji
walioombewa usajili Yanga na tayari ITC zao zimepatikana ni Nizar
Khalfan kutoka Vancouver Whitecaps ya Canada, Didier Kavumbagu (Atletico
Olympic- Burundi) na Mbuyu Twite kutoka FC Lupopo ya Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo (DRC).
Kwa
upande wa Simba ni Musa Mude (Sofapaka, Kenya) na Daniel Akuffor
(Stella Abidjan, Ivory Coast) wakati Mtibwa Sugar ni Shabani Kisiga timu
ya El Itihad ya Oman.
Waliopata
ITC kwa upande wa Kagera Sugar ni Wilfred Ojodale Ame na Benjamin Efe
Ofuyah wote kutoka FC Abuja ya Nigeria. Wengine ni Deangelis Silva
kutoka New Road ya Nepal kwenda Coastal Union, George Odhiambo kutoka
Randers FC ya Denmark kwenda Mtibwa Sugar na Jerry Santo kutoka Tusker,
Kenya kwenda Coastal Union.
Wachezaji
ambao wameombewa usajili na ITC zao bado hazijapatikana ni Salum Kinje
na Pascal Ochieng wa AFC Leopards, Kenya kwenda Simba na Ayoub Hassan
Isiko kutoka Bull FC, Uganda kwenda Mtibwa Sugar.
Bado
klabu ambazo hazijakamilisha usajili na kupata ITC zina fursa ya
kufanya hivyo hadi Septemba 4 mwaka huu ambapo dirisha litafungwa.
Pia
TFF imetoa ITC kwa wachezaji wanane walioombewa kwenda kucheza mpira
wa miguu katika nchi za Kenya na Msumbiji kutoka katika klabu
mbalimbali za hapa nchini.
Wachezaji
hao na klabu wanazokwenda katika mabano ni Abdallah Ally Abdallah (CD
Madchegde, Msumbiji), Almasi Khatib Mkinda (Ferroviario da Beira,
Msumbiji), David Naftali (Bandari, Kenya) na Hassan Hassan Mustafa (CD
Madchegde, Msumbiji).
Wengine
ni Meshack Abel (Bandari, Mombasa), Mohamed Banka (Bandari, Kenya),
Thobias Davis Silas (CD Madchegde, Msumbiji) na Thomas Maurice (Bandari,
Kenya).
0 comments:
Post a Comment