Idadi ya watu waliokufa kwenye
mitetemeko miwili ya ardhi nchini Iran inazidi kuongezeka, na sasa
inajulikana kuwa watu kama 250 wamekufa.
Waokozaji wanawatafuta manusura kwenye kifusi cha majengo yaliyoporomoka katika miji na vijiji kwenye eno la mji wa Tabriz, kaskazini-magharibi mwa nchi.
Shirika la Mwezi Mwekundu la Iran limechukua uwanja wa mpira kuwapa hifadhi watu waliopoteza makaazi yao, au wanaogopa kurudi nyumbani.
Shirika hilo limetoa mahema, mablanketi na chakula.
Shirika la Mwezi Mwekundu la Uturuki, limesema linatuma msaada mpakani.
0 comments:
Post a Comment