Friday, August 24, 2012

Viwanjani Leo Ijumaa-Yanga Kucheza Na Rayon ya Rwanda Leo


Rais Paul Kagame katika picha ya pamoja na Yanga. (Picha  na Saleh Ally wa gazeti la Champion).
Mabingwa wa Kombe la Kagame klabu ya Dar Young Africans  leo watashuka dimbani kuivaa Rayon Sports ya Rwanda kwenye Uwanja wa Amaholo jijini Kigali.

Ufafanuzi Oparesheni Ya Kuwaondoa Wavamizi Wa Ardhi Eneo La Madale Na Zoezi La Sensa Jijini Dar Watolewa.


Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kufafanua oparesheni ya kuwaondoa wavamizi wa ardhi katika eneo la Madale na zoezi la Sensa ya watu na makazi leo jijini Dar es salaam.

Na. Aron Msigwa –MAELEZO.
 
Serikali imesema kuwa haitayavumilia makundi ya watu wanaovunja sheria za nchi kwa kuendesha vitendo vya wizi, uvunjaji wa nyumba, uporaji na uuzaji wa ardhi kinyume cha sheria katika maeneo yanayomilikiwa kihalali jijini Dar es salaam.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Bw. Saidi Meck Sadiki ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es salaam kufuatia vurugu zilizotokea katika eneo la Madale nje kidogo ya jiji la Dar es salaam kutokana na uamuzi wa serikali kuwaondoa kwa nguvu wananchi waliovamia maeneo hilo.
Amesema kuwa serikali haikukurupuka kuchukua hatua hiyo na kuongeza kuwa hatua zilizochukuliwa zimezingatia kanuni na taratibu za kisheria zikiwemo baraka za kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa.
“ Kufanyika kwa zoezi hili si kwamba serikali ya Kinondoni imekurupuka, hata kidogo haijafanya hivyo, zoezi hili limefuata kanuni na taratibu zote za kisheria ikiwemo uamuzi wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Dar es salaam na amri ya Mahakama”
Amefafanua kuwa matukio yaliyotokea hivi karibuni katika maeneo hayo kwa baadhi ya makundi ya wananchi hasa vijana waliobeba silaha za jadi kuwashambulia, kuwajeruhi na kuharibu mali za wananchi wanaoishi katika eneo la Madale kihalali kwa lengo la kuwaondoa kwa nguvu na kuyatwaa maeneo yao ni jambo lisilokubalika nchini.
Amesema kuwa licha ya jambo hilo kuwa la muda mrefu na serikali kuchukua hatua za kuhakikisha kuwa wananchi wanaoishi katika maeneo hayo kihalali wanafanya shughuli zao bila kusumbuliwa baadhi ya wananchi wamekuwa hawakubaliani na jambo hilo na hatimaye kuanza kuyavamia maeneo ya wazi ambayo mengine yanamilikiwa na taasisi na makampuni.
Ameongeza kuwa zoezi hilo la kuwaondoa wananchi waliovamia maeneo hayo lilizingatia taratibu zote ikiwemo hatua ya serikali kuwapa taarifa wahusika wote waliovamia maeneo hayo kuondoka wenyewe jambo ambalo hawakulifanya.
“Kabla ya kutumia nguvu kuwaondoa wananchi hao serikali iliwapatia taarifa ya kuwataka kuondoka wenyewe jambo ambalo walilikaidi na kuendelea kukalia maeneo hayo kinyume cha sheria.
“ Bado naendelea kusisitiza kuwa serikali ilifuata taratibu zote, kwanza tuliwashauri wamiliki halali kwenda mahakamani kisha mahakama ikatoa amri ya wavamizi hao kuondolewa na zaidi ya hapo walipewa taarifa ya kuondoka wao wenyewe jambo ambalo hawakulifanya na hii inaashria kudharau amri ya mahakama” amesisitiza Bw. Sadiki.
Aidha Bw. Saidi Meck Sadiki amesema kuwa imebainika kuwa baadhi ya wananchi wanaoendesha vitendo hivyo vya kihalifu sio raia wa Tanzania na kukongeza kuwa tayari vyombo vya dola vinavyohusika vinaendelea na uchunguzi wa suala hilo na tayari vinawashikilia watu 68 kwa kuhusika na vurugu hizo.
Pia ameonyeshwa kusikitishwa na baadhi ya watendaji wachache wa serikali na viongozi wa siasa wanaoshabikia na kuhamasisha suala hilo na kuongeza kuwa serikali inaendelea na uchunguzi wa suala hilo na ikibainika hathua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Katika hatua nyingine mkuu wa mkoa wa Dar es salaam amevipongeza vyombo mbalimbali vya habari vinavyoendelea kuwahamasisha wananchi kushiriki katika zoezi la Sensa ya watu na makazi na kuongeza kuwa hivi sasa wananchi wana uelewa mkubwa juu ya zoezi hilo na wako tayari kuhesabiwa.
“Navishukuru sana vyombo vya habari kwa kazi nzuri za uhamasishaji wa watu kushiriki katika Sensa ya watu na Makazi japo vipo vichache sana vinavyoendesha mijadala ya kuipinga”

MBUYI TWITE ATHIBITISHWA RASMI NA TFF KUJIUNGA NA YANGA


Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa wachezaji 11 wa nje kati ya 14 walioombea usajili na klabu mbalimbali za Ligi Kuu.
 
Wachezaji walioombewa usajili Yanga na tayari ITC zao zimepatikana ni Nizar Khalfan kutoka Vancouver Whitecaps ya Canada, Didier Kavumbagu (Atletico Olympic- Burundi) na Mbuyu Twite kutoka FC Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).
 
Kwa upande wa Simba ni Musa Mude (Sofapaka, Kenya) na Daniel Akuffor (Stella Abidjan, Ivory Coast) wakati Mtibwa Sugar ni Shabani Kisiga timu ya El Itihad ya Oman.
 
Waliopata ITC kwa upande wa Kagera Sugar ni Wilfred Ojodale Ame na Benjamin Efe Ofuyah wote kutoka FC Abuja ya Nigeria. Wengine ni Deangelis Silva kutoka New Road ya Nepal kwenda Coastal Union, George Odhiambo kutoka Randers FC ya Denmark kwenda Mtibwa Sugar na Jerry Santo kutoka Tusker, Kenya kwenda Coastal Union.
 
Wachezaji ambao wameombewa usajili na ITC zao bado hazijapatikana ni Salum Kinje na Pascal Ochieng wa AFC Leopards, Kenya kwenda Simba na Ayoub Hassan Isiko kutoka Bull FC, Uganda kwenda Mtibwa Sugar.
 
Bado klabu ambazo hazijakamilisha usajili na kupata ITC zina fursa ya kufanya hivyo hadi Septemba 4 mwaka huu ambapo dirisha litafungwa.
 
Pia TFF imetoa ITC kwa wachezaji wanane walioombewa kwenda kucheza mpira wa miguu katika nchi za Kenya na Msumbiji kutoka katika klabu mbalimbali za hapa nchini.
 
Wachezaji hao na klabu wanazokwenda katika mabano ni Abdallah Ally Abdallah (CD Madchegde, Msumbiji), Almasi Khatib Mkinda (Ferroviario da Beira, Msumbiji), David Naftali (Bandari, Kenya) na Hassan Hassan Mustafa (CD Madchegde, Msumbiji).
 
Wengine ni Meshack Abel (Bandari, Mombasa), Mohamed Banka (Bandari, Kenya), Thobias Davis Silas (CD Madchegde, Msumbiji) na Thomas Maurice (Bandari, Kenya).

Simba, Azam Zajiandaa Kwa Ajili Ya Ngao Ya Hisani Septemba 8

Kikosi cha Simba.


Kikosi cha Azam.


KATIKA kujiandaa na mechi ya Ngao ya Jamii, mabingwa wa Tanzania Bara, Simba SC, Jumamosi watacheza mechi ya kujipima nguvu na Mathare United ya Kenya kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha.

Simba itamenyana na Azam katika mechi ya Ngao ya Jamii ya kuashiria kufunguliwa kwa pazia la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Septemba 8, mwaka huu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.


Habari za ndani kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), zimesema kwamba, kuchelewa kwa mechi hiyo ambako kumeenda sambamba na kuchelewa kuanza kwa ligi hiyo, kumetokana na kuchelewa kufikiwa mwafaka mapema wa mkataba mpya wa udhamini wa Ligi Kuu.

Wakati huo huo, Mshindi wa pili wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Azam FC Jumamosi watamenyana na Transit Camp kwenye Uwanja wa Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Kihistoria hiyo itakuwa mechi ya tano ya Ngao ya Jamii kuchezwa nchini na ya pili kuishirikisha timu nje ya wapinzani wa jadi wa soka ya Tanzania, Simba na Yanga.
Mtibwa ilicheza na Yanga mwaka 2009, baada ya Simba kugoma na ikashinda mabao 2-1 na kutwaa Ngao, wakati kabla ya hapo, mwaka 2001, Ligi Kuu ya Tanzania ikiwa bado inadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia bia ya Safari Lager, ilichezwa mechi ya kwanza ya Ngao kihistoria.

Katika mechi hiyo, Yanga ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Simba na mwaka juzi Yanga iliifunga tena Simba kwa penali 3-1 kufuatia sare ya 0-0 na mwaka jana, Simba ilitwaa Ngao ya kwanza katika historia yake, kwa kuifunga Yanga mabao 2-0.


MABINGWA WA MECHI ZA NGAO YA JAMII:
Mwaka Mshindi Matokeo
2001 Yanga 2-1 Simba
2010 Yanga 0-0 Simba (3-1penalti)
2011 Simba 2-0 Yanga

Chanzo: http://bongostaz.blogspot.com

IJUMAA YA LEO KATIKA MAGAZETI











PAUL KAGAME ALIVYOWAKARIBISHA YANGA KWENYE IKULU YA RWANDA


Raisi wa Rwanda Paul Kagame akisalimiana na Mama Fatma Karume aliyeomgozana na Yanga kwenda nchini Rwanda.

Kocha wa Yanga Saintfield akisamiliana na Kagame

Mwenyekiti wa Yanga Yusuph Manji akisoma risala yake mbele ya Raisi Kagame

Wachezaji wa Yanga wakisikiliza kwa makini risala ya mwenyekiti wao

Nahodha wa Yanga na kocha wakimkabidhi kombel la Kagame - mdhamini mkuu wa kombe hilo Raisi wa Rwanda Paul Kagame.

Mama Karume na Seif Magari wakimkabidhi Kagame jezi ya Yanga

Paul Kagame akiongea na Wachezaji wa Yanga



Mchezaji Mbuyi Twite akiwa na wachezaji wenzie wa Yanga Ikulu ya Rwanda walipoalikwa na Raisi Paul Kagame.

PICHA ZOTE ZIMEPIGWA NA SALEHE ALLY WA CHAMPION

Israili na Afrikan Kusini yazozana


Rais jacob Zuma
Rais jacob Zuma
Israili imekasirishwa na uwamuzi wa serikali ya Afrika ya Kusini wa kupiga marufuku nembo zinazowekwa kwenye bidhaa ambazo zina nembo isemayo ''made in Israel'' il hali zimetengenezwa Ufuko wa magharibi.
Badala yake Afrika ya Kusini inataka bidhaa hizo zibainishwe kwa kuandikwa kuwa zimetengezwa katika ''maeneo yanayokaliwa''
Wizara ya mashauri ya nje ya Israil itaja hatua hiyo kama ya ubaguzi.
Makaazi, miji ya Israili iliyojengwa katika maeneo yanayozozaniwa ya wa Palestina ni kinyume cha sheria ya Kimataifa ingawa Israili inapinga hilo.
Afrika ya Kusini inaaminika kuwa nchi ya kwanza kujaribu kutimiza uamuzi huu kisheria ingawa serikali nyingine kama Uingereza, zimewahi kuyashauri maduka makubwa yabainishe bidhaa zitokazo kwenye makaazi ya walowezi wa Israili.
Lakini kuanzia leo nchini Afrika ya Kusini, bidhaa kutoka makaazi hayo ya Israili, hazitokubalika kuwa na nembo "made in Israel".
Wizara ya mashauri ya nje ya Israili, imeutaja uwamuzi huo kama wa Ubaguzi wa rangi na usiokubalika.
Wizara hiyo imemtaka Balozi wa Afrika ya kusini nchini Israili aeleze hatua ya serikali yake.
Kuna kampeni inayofanywa miongoni mwa wa Palestina na waungaji mkono wao ya kususia bidhaa zinazotengenezwa ndani ya maeneo yanayokaliwa na walowezi wa Kiyahudi pamoja na Israili kwa ujumla.
Msemaji wa vuguvugu la Afrika ya Kusini ameutaja uamuzi wa Afrika ya Kusini kama ishara tu lakini akaonyesha matumaini utakua chachu kwa wengine.
Raia wa Palestina wanaopendelea vikwazo mara kwa mara hutumia mfano wa juhudi za uhuru huko Afrika ya Kusini kama changamoto na kuishutumu Israili kuwa inaendesha sera ya ubaguzi na kuongoza dola la kiimla, Israili inapinga tuhuma hizo.

Taharuki nchini Kenya baada ya mauaji

Baadhi ya watu wamelazimika kutafuta hifadhi sokoni kwa kuhofia usalama wao.

Tana River, Kenya
Tana River, Kenya
Mauaji hayo yalitokea wakati watu wenye silaha kutoka jamii ya Pokomo waliposhambulia kijiji kimoja katika eneo la Reketa huku wakiteketeza makaazi ya watu.
Mmoja wa wale walioathiriwa ameelezea BBC kwamba walishambuliwa usiku, ''hata tumekimbia kutoka kijiji chetu sasa. Walikuja kwa kijiji cha Riketa, watu walikuwa wanalala hata hawana habari wakavamia akina mama, watoto wote wamekufa hapa hapa.''
Alisema shambulizi hilo limewashangaza kwa sababu hata wakati mifugo wao wameingia kwenye mashamba, kuna njia ya kufidia, ''sisi kawaida yetu, hiyo mifugo inashikwa kisha unalipishwa. Sio kukatakata mifugo au kumaliza wachungaji.''
Naibu kamanda wa polisi mjini Mombasa, Joseph Kitur amesema uchunguzi wa awali umebainisha kuwa shambulio hilo lilifanywa na watu kutoka jamii ya Pokomo.
Jamii za Pokomo na Orma zimekuwa zikizozania malisho na maji tangu mwezi uliopita lakini shambulizi hili ndilo mbaya zaidi kutokea kati yao.
Mwaka wa 2001, karibu watu 130 walifariki wakati mzozo kati ya jamii hizo mbili ulipozuka.
Jamii ya Pokomo ni wakulima na huwa inategemea sana mto wa Tana kwa shughuli zao.
Jamii ya Orma ni wafugaji.
Mauaji hayo yameleta kumbukumbu za ghasia za baada ya uchaguzi za mwaka wa 2007, ambapo watu 1,200 walifariki katika mapigano.

Uingereza yaibembeleza Ecuador

Uingereza imeandika barua kwa ubalozi wa Ecuador mjini London ikitaka kurejelea mazungumzo kuhusu hatma ya Julian Assange, mwanzilishi wa mtandao wa kufichua siri wa Wikileaks, aliyetorokea katika majengo ya ubalozi huo kuepuka kurejeshwa nchini Sweden kwa lazima.

Julian Assange katika ubalozi wa Ecuador
Uhusiano kati ya mataifa hayo mawili ulivurugika baada ya uamuzi wa Ecuador kumpa bwana Assange hifadhi ya kisiasa na Uingereza kutishia kuvamia ubalozi huo na kumkamata.
Afisi inayoshughulika na masuala ya kigeni haijasema chochote kuhusu ujumbe uliokop kwenye barua hiyo lakini afisa mmoja ameelezea kuwa inanuia kutuliza hali kati ya mataifa hayo mawili.
Rais Rafael Correa ameiambia BBC kuwa Uingereza ilifanya makosa makubwa kwa kutishia kuingia kwa nguvu kwenye ubalozi wa Equador,''Huu ni mvutano ambao ungeisha iwapo Uingereza ingetoa hakikisho ya kupita kwa usalama kwa Bwana Assange au unaweza kuendelea kwa miezi na hata miaka iwapo hataweza kutoka kwenye ubalozi wetu hapa London kuelekea Equador.''
Huenda mataifa ya Amerika Kusini yakamuunga mkono rais Rafael Correa.
Huku Uingereza ikisema kuwa inataka kurejelea mashauriano kuhusu hatma ya Julian Assange, Equador haikubaliani na msimamo huo na inataka kuhakikishiwa kuwa Assange hatakamatwa iwapo atatolewa kwenye ubalozi wao nchini Uingereza kuelekea Equador.
Equador inataka pia kuhakikishiwa kuwa mwanzilishi huyo wa mtandao wa Wiki Leaks hatawahi kupelekwa Marekani anakokabiliwa na tuhuma za kutoa taarifa muhimu na za siri kwenye mtandao wake.
Hata hivyo hakuna matumaini kwamba Marekani itakubali hilo.
Kwa hiyo ubalozi wa Equador umekiri kuwa huenda ukampa bwana Assange hifadhi kwa miaka mingi.

Chelsea 4-2 Reading: Hazard bags three assists as Blues come from behind to claim victory


Fernando Torres scored the decisive goal as Chelsea came from behind to beat Reading 4-2 at Stamford Bridge.
Frank Lampard opened the scoring with a powerful first-half penalty after Eden Hazard, who impressed once again, had been tripped by Chris Gunter.

Reading equalized shortly after through a thunderous Pavel Pogrebnyak header, before Petr Cech let a Danny Guthrie free kick squirm from his grasp and into his own net.

But Adam Federici followed suit, allowing a Gary Cahill shot to skid away from him, and with less than 10 minutes remaining, Torres was left with the simplest of finishes after good work by Juan Mata and Ashley Cole.

Branislav Ivanovic swept into an open goal in stoppage time, with Federici out of his area after attacking a corner.

Hazard, who had caught the eye in his Premier League debut against Wigan and had three assists against Reading, was involved inside two minutes, racing onto a pass from Mata on the left hand side, but the Belgian’s shot across goal failed to find the target and rolled wide.

Just five minutes later Chelsea went closer, as a lovely fluid passing move involving Torres and Branislav Ivanovic launched an attack for the returning Ramires, but the midfielder chose to test Adam Fedrici rather than play the Chelsea striker in with the goal at his mercy, and the Reading keeper palmed the ball away.

Reading launched a counterattack from Federici’s save, but lone striker Pavel Pogrebnyak flashed his shot wide, before Torres would get his first chance of the match.

The Spain international displayed some excellent trickery to deceive Jem Karacan and Kaspars Gorkss to make space in the penalty area, but his shot was blocked and flew to safety.

It was more Chelsea skill that would create the chance for the opening goal, as Hazard had his standing leg tripped in the box by Gunter, leaving match official Lee Mason with the easy decision to award the penalty.

Lampard stepped up and drilled low and powerfully to Federici’s right and, though the shot stopper dived the right way, he had little chance of keeping the spot kick out.

The home side’s lead lasted little more than five minutes though, as Pogrebnyak headed Reading level.

Garath McCleary exchanged a quick one-two with Danny Guthrie before finding the Russian, who showed expert movement to beat Gary Cahill and head into the top corner beyond Cech.

And, just before the half-hour mark, the visitors were in front after John Terry gave away a free kick for a foul on Jobi McAnuff around 20 yards from goal.

Guthrie blasted low and hard at Cech, but the 30-year old spilled a regulation save and could only watch the ball trickle into his net.

Chelsea had chances to equalize before the interval but Hazard fired over from distance before crossing for Torres, who nodded just wide, while Alex Pearce was inches away from extending the visitors’ lead, but could not connect with an Ian Harte free kick.

The Blues wasted no time in attempting to get back into the game after the break as Torres pulled back to the edge of the box for Ivanovic, but the defender’s shot sailed a long way over the bar.

But, with his side unable to break Reading down in the early stages of the second half, Roberto Di Matteo handed Oscar his Stamford Bridge debut, in place of compatriot Ramires.

Oscar was immediately among the action, nicking the ball away from Karacan, who upended the Brazilian and picked up a yellow card.

With over an hour played, Chelsea was finally able to carve out a second-half opening and after some pinball in the box following an Ivanovic pass, the ball fell to Hazard, but his shot was blocked by Pearce when Federici may well have been beaten.

Di Matteo was forced into another change as the hosts chased the elusive equalizer and replaced John Obi Mikel with Daniel Sturridge.

But it was a defender who would pull the scores level in the 70th minute, when Cahill’s speculative long-range effort bounced in front of the outstretched palms of Federici, who pushed the stinging shot into the bottom corner.

The equalizer appeared to have given Chelsea the impetus to press for a winner, with Juan Mata going close with a shot, beating Federici but curling wide.

And it was Mata again who went close with ten minutes remaining, scuffing wide after an Ivanovic cross cannoned into his path.

Just moments later though, Chelsea scored the winner as Ashley Cole darted onto a pass inside the box and squared for Torres, who got ahead of the resolute Reading backline and tapped into an empty net.

There were suspicions of offside surrounding the goal, but Chelsea took the three points in its first home game of the season as Federici came up for a corner and left his goal exposed, allowing the hosts to break through Hazard, who gifted Ivanovic an open goal