Tuesday, August 14, 2012

Wanafunzi 3074 Walioomba Mikopo Waenguliwa Na Bodi Ya Mikopo-TCU


                  Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo, George Nyatogo.


Na Joachim Mushi, Thehabari.com

BODI ya Mikopo ya Elimu ya Juu nchini pamoja na Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) imewaengua zaidi ya wanafunzi 3074 walioomba vyuo na mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka 2012/13.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na taasisi hizo kupitia mitandao yao (website) Agosti 10 na 12, 2012 zaidi ya wanafunzi 3074 wameenguliwa katika maombi yao kwa kuwa na dosari mbalimbali.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) pekee imeorodhesha zaidi ya wanafunzi 2,649 ambao imebaini kuwa na mapungufu kadhaa katika maombi yao ya kupewa mikopo ya vyuo.

Miongoni mwa makosa ama dosari ambazo bodi imezibaini kwa walioenguliwa kwa sasa ni pamoja kukosekana kwa vyeti vya kuzaliwa kwa muombaji, sahihi ya mdhamini/muombaji, kukosekana kwa picha ndogo ya muombaji/mdhamini, kukosekana kwa sahihi za viongozi wa Serikali za mitaa/vijiji kwa waombaji na nyaraka nyingine muhimu kwa waombaji.

Kwa upande wake TCU imewaengua jumla ya waombaji 425 kwa dosari na makosa mbalimbali, ambayo imeyabainisha katika taarifa yake.

Miongoni mwa dosari ambazo zimetajwa na TCU kwa wanafunzi hao ni pamoja na baadhi yao kukosea namba za vyeti vya masomo kwa vidato vya nne na tano (O’ level na A’ level Index number), miaka ya kumaliza masomo (year of completion), mawasiliano sahihi kwa muombaji (Contact information e.g. Mobile phone number, email address and postal address) pamoja na uchaguzi wa masomo (Programme selected).

Waweza kuingia katika linki hii hapo chini na kuona majina ya waliobainika kuwa na dosari anuai katika maombi yao kwa TCU http://www.tcu.go.tz

Pia waweza kutembelea linki zifuatazo na kushuhudia majina ya waliobainika kuwa na dosari hizo katika maombi yao kwa bodi ya mikopo;-http://www.heslb.go.tz

Hata hivyo taasisi hizo mbili zimetoa muda kwa walioenguliwa sasa kutokana na dosari hizo kurekebisha na kutuma tena maombi yao kupitia mitandao kwa mujibu wa maelekezo waliyotoa.

MWANAFUNZI ABAKWA, ANYONGWA, AZIKWA



Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Bw. Zelothe Sephen.
MWANAFUNZI wa darasa la saba Shule ya Msingi Hogolo, wa umri wa miaka 14 (jina limehifadhiwa) ambaye ni Mkazi wa Mtaa wa Ikulu Kijiji cha Hogolo wilayani Kongwa, mkoani Dodoma ameuawa kwa kunyongwa na kuzikwa kwenye shimo nyuma ya nyumba yao karibu na choo baada ya kubakwa.
Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa chanzo cha mauaji hayo yaliyofanyika Jumamosi iliyopita ni wivu wa kimapenzi kwani marehemu enzi za uhai wake, anadaiwa alikuwa amevunja uhusiano na mpenzi wake wa muda mrefu, Heri Aboubakar na kuanzisha uhusiano mpya na Wilfredy Muhaha maarufu Kabo.
Hata hivyo bado haijafahamika muuaji halisi wa marehemu huyo licha ya polisi kuwashikilia watu kadhaa kwa tuhuma za kuhusika na tukio hilo akiwemo mpenzi wake wa sasa, Muhaha.
Mbali na Muhaha wengine wanaoshikiliwa Polisi ni Ashad Jafari ambaye ni mkulima na mkazi wa Mtaa wa Nyerere Hogolo ambaye ni rafiki wa marehemu na Rino Mazoea, mkulima na mkazi wa Ikulu Hogolo wilayani Kongwa ambaye ni kaka wa marehemu.
Kamanda Zelothe Steven alisema wanamtafuta Aboubakar ambaye amekimbia kijijini hapo na hajulikani alipo mpaka sasa. Katika tukio hilo, kaka wa marehemu ambaye pia anashikiliwa Polisi, katika maelezo yake ya awali alidai kusikia purukushani zikitokea usiku wa tukio hilo la mauaji lakini hakutoka usiku huo kushuhudia nini kinaendelea.
Marehemu alikuwa akiishi na babu na bibi yake hapo kijijini na siku ya tukio , walezi hao, walikuwa wameondoka kwenda katika vijiji vya jirani, ambapo bibi yake alikuwa amekwenda Kongwa kwa ajili ya kujengea makaburi na babu yake alikwenda Kijiji cha Banyi Banyi kutembelea wagonjwa.

TCU ANNOUNCEMENT to the prospective applicants on the second round of application

Tanzania Commission for Universities (TCU) informs all prospective applicants that, applications for admission into higher learning institutions for the second round of application, will start on 13th August 2012. The second round of application will involve:




a)    New applicants (Form 6, Teachers, FTC, NTA Level 6 and applicants with foreign certificates) who did not have the opportunity to apply during the first round of application; or
b)   Applicants who were not selected during the first round of application due to various reasons and whose names will be published on the TCU website or have been notified through their individual accounts of this fact.

NOTE:
i)          Applicants who applied but for some reasons they were not selected, are not required to pay another application fee instead they will only be required to choose another program by logging into their accounts.
ii)        The list of applicants who were not selected and hence are required to re-apply will be on TCU website on Tuesday 14th August 2012.
How to apply

Applicants will apply through the Central Admissions System and applications will be treated on the first-come first-served basis this means the applicant is required to choose only one program he/she qualifies basing on program requirements given in the ‘Students Guidebook’ available on TCU website. Each programme is tied to an institution and that means the process involves one programme at a particular institution only.
Application fee for new applicants

·       Tanzanians will be required to pay an application a non-refundable fee of TSHS.30,000/- payable through NBC branches country wide,
·       Non-Tanzanians will be required to pay US$60 through CAS Account at any NBC bank countrywide (TCU-CAS Acc. No.074139000021), and
·       Non-Tanzanians residing outside Tanzania will be required to pay US$60 through CAS account number (TCU-CAS Acc.No.074139000021). The swift code: NLCBTZTX.
Deadline for application 
The deadline for applications for all categories will be on 25rd August 2012.

Cristiano Ronaldo, Iniesta and Messi shortlisted for UEFA Best Player in Europe award

The Primera Division stars are still in the running to win the second edition of the individual award after receiving the most points in a vote among sports journalists.

Cristiano Ronaldo Lionel Messi

Real Madrid forward Cristiano Ronaldo and Barcelona duo Lionel Messi and Andres Iniesta have been shortlisted for the UEFA Best Player in Europe award.

The trio gained the most points in a vote among 53 sports journalists representing each of the European football governing body's member associations.

Juventus playmaker Andrea Pirlo came in fourth in the election, while Barcelona's Xavi, who finished second in last year's edition of the award, completed the top five.

The remaining three players will now go into a deciding vote in Monaco during the Champions League group stage draw on August 30.

The individual award, created in partnership with European Sports Media (ESM), recognizes the best player, irrespective of his nationality, playing for a club within the territory of a UEFA member association during the previous season.

WASOMI UDSM WAIKOSOA BAJETI YA ELIMU


                        Baadhi ya maofisa kutoka taasisi ya HakiElimu
Kutoka kushoto ni Meneja Kitengo cha Habari wa HakiElimu, Nyanda Shuli, Mhadhiri Adolf Mkenda kutoka Idara ya Uchumi ya UDSM Mhadhiri wa UDSM, Dk. Kitila Mkumbo

Na Joachim Mushi, Thehabari.com

TAASISI ya HakiElimu leo jijini Dar es Salaam imewakutanisha baadhi ya wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), walimu pamoja na wadau mbalimbali wa elimu ambapo waliishuhudia bajeti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Elimu ikiwasilishwa ‘live’ mjini bungeni mjini Dodoma kabla ya kutoa maoni yao.

Wadau hao wa elimu kwa pamoja waliishuhudia kupitia king’amuzi bajeti ya Wizara ta Elimu na Mafunzo ya Ufundi ikiwasilishwa ‘live’ wakiwa kwenye mkutano kisha baadaye kutoa maoni yao jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mara baada ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Elimu, Dk. Shukuru Kawambwa kuwasilisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka 2012/13, Mhadhiri wa UDSM, Dk. Kitila Mkumbo alisema ameshangaa bajeti hiyo kutouona mgomo wa walimu wa juzi pamoja na migomo ya wanafunzi wa vyuo vikuu kama ni tatizo kwa elimu na kuiingiza kama changamoto.

“Binafsi kati ya vitu ambavyo vimenishangaza ni bajeti hiyo kutotaja mgomo wa walimu katika bajeti iliyopita kuwa ni miongoni mwa changamoto za wizara hiyo…na hata migomo ya vyuo vikuu,” alisema Dk. Mkumbo alipokuwa akijadili katika mkutano huo.

Alisema wizara imetaja kufanya vizuri katika elimu upande wa msingi na sekondari kwa kidato, lakini imekwepa kutoa mafanikio kwa kidato cha tano na sita eneo ambalo limefanya vibaya kwa matokeo ya hivi karibuni. Alikosoa kiwango cha uwiano kati ya wanafunzi na walimu kilichotatolewa kwa sasa (1:46) kwani idadi kubwa ya walimu wapo shule za mjini huku hali mbaya ikiwa vijijini.

Aidha aliongeza kuwa wizara pia imeshindwa kuona migomo ya wanafunzi wa vyuo vikuu ya mara kwa mara ni changamoto hivyo kushindwa kueleza katika bajeti yake. “…karibu asilimia 80 ya migomo ya wanafunzi wa vyuo vikuu imesababishwa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, lakini hili halikutajwa katika bajeti ya waziri,” alisema msomi huyo.
Kwa upande wake Mhadhiri Adolf Mkenda kutoka Idara ya Uchumi ya UDSM akizungumza katika mkutano huo alisema bajeti iliyowasilishwa ni ya kawaida hivyo ni vigumu kumaliza changamoto lukuki za elimu zinazoikabili wizara hiyo.
Alisema bajeti imejivunia ongezeko la idadi ya vyuo vikuu lakini imeshindwa kuonesha ubora wa vyuo hivyo jambo ambalo ni hatari endapo litaachwa, bila udhibiti. “…Twaweza kuwa na vyuo vingi lakini suala la ubora ni tatizo lingine. Pia uandikishaji wa idadi kubwa ya wanafunzi unatakiwa kulinganishwa na waliokusudiwa kuandikishwa…maana twaweza jivunia kiwango kinapanda kumbe tunadanganywa na ongezeko la idadi ya watu,” alisema msomi huyo.

Akizungumza kwenye mjadala Meneja wa Kitengo cha Habari wa HakiElimu, Nyanda Shuli alisema Serikali haiwezi kufanikisha elimu bora bila kuaandaa walimu bora katika utoaji wa elimu husika. “Huwezi kutegemea elimu bora pasipo na walimu bora, binafsi sijaona mkakati wowote mahususi wa kuboresha elimu,” alisema Shuli.
Ameishauri wizara ya elimu kujiandaa vizuri kimipango kabla ya kutekeleza mpango wa kuwa na shule ya kidato cha tano na sita kwa kila tarafa ili kuepuka madudu yaliojitokeza katika mpango wa uanzishwaji shule za kata.

Hata hivyo kabla ya kuishuhudia bajeti hiyo ikiwasilishwa Dk. Mkumbo na Mkenda wakiongozwa na mhadhiri mwenzao kutoka Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano, Ayoub Rioba waliwasilisha mada zilizokuwa zikiiangalia elimu ya Tanzania na majaliwa yake.

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Elimu tayari imewasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2012/13 ambapo jumla ya sh. 724,471,937,000 ili zitumike kuiwezesha Wizara kutekeleza majukumu yake. Huku sh. 18,561,689,000 zikiwa ni fedha za ndani na sh. 74,019,627,000 kutoka kwa washirika wa maendeleo

Jumanne Ya leo katika magazeti

















Mabondia wagoma kurudi Afrika, Waomba hifadhi London!


Blaise Yepmou Mendouo
Wanamichezo watano waliohudhuria miechezo ya Olympic jijini London Uingereza kutoka nchini Cameroon, wanasema wanataka ukimbizi kuendelea kubaki nchi Uingereza baada ya kutoweka katika kijiji cha Olympic wiki iliyopita.
Wanamichezo hao wanaume watano wote wakiwa ni mabondia wameiambia BBC kuwa waliondoka katika kijiji cha mashindano ya Olympic mashariki mwa London baada ya kutishiwa na maafisa wa juu wa timu ya Olympic ya Camerron, kuwa wangeadhibiwa iwapo wangeshindwa katika mashindano hayo.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake mmoja wa mabondia hao amesema wanataka kubaki nchini Uingereza ili kuendeleza taaluma yao ya kimichezo katika ndondi.
Hata hivyo mkuu wa msafara wa timu ya wanamichezo wa Cameroon David Ojong, amesema mabondia hao wamedanganya na kuwa hakuna yeyote aliyewatishia.
Amesema mabondia wote walipata mafunzo ya kutosha pamoja na kulipwa vizuri na sababu hiyo huenda ni kuhalalisha kurotoka kwao.
Mmoja wa mabondia hao Thomas Essomba amesema viongozi wa msafara wao waliwatisha kwa kuanza kuwaamuru wale waliokuwa tayari wameshiriki michezo mingine na kushindwa kusalimisha hati zao za kusafiria.
Naye bondia mwingine Blaise Yepmouo, amesema kamwe hawataki kurejea nchini mwao kwani taaluma yao ya kimichezo itakufa.
''Tunataka kuwa mabondia wa kulipwa na hatuwezi kurudi Camroon.'' Anasema. ''Na hata ikiwa tutarudi hatuwezi tena kuendelea na ngumi. Watano waliopo hapa wanataka kuwa mabondia wa kulipwa na ndiyo maana tunaomba udhamini.''
Wamesema kuwa kubaki kwao Uingereza kutawawezesha kupata udhamini na hivyo kuendeleza vipaji vyao katika mchezo huo.

Helikopta za kivita za Uganda zapatikana

Msemaji wa Jeshi Uganda ,Kanali Felix Kulaigye
Jeshi la Uganda limesema kuwa helikopta zake nne zilizokuwa zime ripotiwa kutoweka zikiwa njiani kuelekea nchini Somalia sasa zimepatikana na marubani wake wote wako salama.
Akizungumza na BBC msemaji wa jeshi hilo Kanali Felix Kulaigye hakuweza kusema ndege hizo ziko wapi kwa sasa.
Naye msemaji wa jeshi la Kenya, Bogita Ongeri ameiambia BBC kwamba operesheni ya kutafuta ndege hizo ilikuwa imevurugwa na hali mbaya ya hewa na kuongeza kuwa helikopta hizo nne zilikuwa kwenye safari hiyo kutoka nchini Uganda.
Moja ya helikopta hizo ilitua katika mji wa Garissa.
Rubani aliyekuwa kwenye helikopta ya pili alizungumza na mamlaka za kenya akisema yuko katika eneo la mlima kenya lakini hakukukuwa na mawasiliano na helikopta nyingine mbili.
Helikopta hizo za Uganda hutumiwa kusindikiza misafara kutoka angani, katika opereresheni za utafutaji na uokoaji pamoja na kushambulia wanamgambo wa kiislamu wa Al Shabaab nchini Somalia.
Helikpta hizo ni miongoni mwa ndege ambazo zilikuwa zikielekea Somalia kukipa nguvu kikosi cha Umoja wa Afrika .
Awali msemaji wa jeshi la Uganda Kanali Felix Kulayigye alikuwa amesema kuwa walikuwa wakizitafuta ndege zao mbili aina ya Mi-24 . Alisema ndege hizo ni zile za kufanya mashambulizi.

Dk. Ulimboka Awekwa Mafichoni



WINGU limegubika sakata la kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari Nchini, Dk Steven Ulimboka siku moja baada ya kurejea nchini, huku watu wake wa karibu akiwamo baba mzazi, wakigoma kusema chochote kumhusu.Dk Ulimboka alirejea nchini juzi akitokea Afrika Kusini alikokuwa amelazwa kwa ajili ya matibabu kwa takriban mwezi mmoja na nusu, baada ya kutekwa, kuteswa na kutupwa kwenye Msitu wa Pande nje kidogo na Jiji la Dar es Salaam usiku wa kuamkia Juni 26 mwaka huu.

Ingawa wakati wa ugonjwa wake baadhi ya watu wake wa karibu walikuwa wakitoa maelezo mbalimbali, jana wote waligoma kusema chochote, huku jitihada za gazeti hili kumpata nyumbani kwake zikigonga mwamba.Baba mzazi wa Dk Ulimboka, Stephen Mwaitenda aliweka wazi kuwa ni vigumu kumwona daktari huyo jana.Takriban watu wote waliofika nyumbani kwa Mzee Mwaitenda jana kumjulia hali Dk Ulimboka waliambiwa kuwa hayupo nyumbani.

Mwaitenda alilieleza gazeti hili kuwa ana furaha kuwa mtoto wake alirejea nchini salama licha ya kupelekwa Afrika Kusini akiwa taabani kutokana na kipigo.
Alipotakiwa kueleza juu ya kile kilichompata, mtoto wake huyo alisema: "Mungu na Steven mwenyewe (Dk Ulimboka) ndio wanaojua kilichotokea."Aliongeza: “Kweli nimefurahi kwamba mwanangu amerudi, lakini siwezi kuelezea nini kilimtokea alipotekwa," alisema Mwaitenda.Alisema Dk Ulimboka hayupo nyumbani na hajui kwamba angerudi wakati gani. "Hata kama angekuwapo, ni vigumu kumwona," alisema.

Kauli ya Katibu wa Madaktari
Katibu wa Jumuiya ya Madaktari, Dk Edwin Chitage alisema madaktari walikuwa hawajaamua nini kingefuata baada ya Dk Ulimboka kurejea nchini.Alisema hata hivyo, daktari huyo anahitaji muda wa kupumzika kwanza na familia yake.“Aliporudi jana (juzi) alitumia muda wake kukaa na familia yake, mpaka sasa hatujajua hatua inayofuata. Dk Ulimboka atazungumza wakati mwafaka ukifika,” alisema Dk Chitage.
Rais wa Chama cha Madaktari (MAT), Dk Namala Mkopi hakutaka kuzungumzia suala hilo akieleza kuwa alikuwa mkutanoni.

Dk Mkopi alitoa kauli hiyo baada ya daktari aliyemtibu Dk Ulimboka wakati wa tukio la kutekwa, Profesa Joseph Kahamba akiwa amesema yeye (Mkopi) ndiye angesaidia kupatikana kwa Dk Ulimboka ili azungumze na waandishi wa habari.

Dk Chitage alipoulizwa nini kinaendelea baada ya Dk Ulimboka kurejea nchini alijibu, "Hakuna kinachoendelea."

Aliendelea, "Leo hakuna kitu, tumepumzika na hata yeye tumemwacha apumzike na familia yake," alisema Dk Chitage.

Alisema Jumuiya hiyo na familia yake wanaandaa mazingira yatakayowezesha Dk Ulimboka kuzungumza na umma kupitia vyombo vya habari.

"Kuhusu hatua zitakazofuata tutaandaa utaratibu na tutawaarifu, juu ya hatua zipi tutachukua ikiwamo hili linaloumiza vichwa vya wengi la mazingira ya kutekwa kwake," alisema Dk Chitage.

Katibu wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Rodrick Kabangila alipoulizwa kuhusu suala hilo alisema yuko safarini na hajui kinachoendelea.

"Nipo Mwanza, nimesafiri na sijui kinachoendelea," alisema.

Alisema MAT itakutana kujadili suala hilo wakati wowote na kwamba utaratibu utaandaliwa kwa Dk Ulimboka kuzungumza na vyombo vya habari.

"Unajua sisi tuliomba kibali cha kuandamana kushinikiza Serikali kuunda tume huru kuchunguza tukio hilo na kuwabaini waliohusika tukakataliwa. Lakini sasa yeye amerudi na anawajua waliomdhuru. Tutaandaa utaratibu, atazungumza nanyi ili watu wote wajue," alisema Dk Kabangila.

Mkurugenzi wa Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake (Tamwa), Ananilea Nkya, alisema hakuwa na mawasiliano yoyote na Dk Ulimboka wala hajui kinachoendelea baada ya kuachana naye juzi Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere.

Polisi wazungumza

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova akizungumza kupitia msaidizi wake, alisema kuwa suala la Dk Ulimboka limefungwa na hawezi kulizungumzia tena kwa kuwa lipo mahakamani.

"Kamanda alikwishasema kuwa suala hilo lipo mahakamani hivyo hawezi kulizungumzia," alisema msaidizi huyo.Alipoulizwa iwapo polisi ilikubali maombi ya madaktari kutaka tume hiyo ivunjwe na iundwe nyingine huru alijibu, "Tume inaendelea na kazi.""Tume inafanya kazi yake na polisi pia wapo katika kazi zao," alisema na kukata simu.

Wanasiasa watoa wito

NCCR-Mageuzi, CUF na Democratic (DP) vimemtaka Dk Ulimboka kuwataja watu waliomteka na kumpiga.Wito huo ulitolewa jana kwa nyakati tofauti na Katibu Mkuu wa NCCR-, Samwel Ruhuza, Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro na Mwenyekiti wa DP, Mchungaji Christopher Mtikila.“Atumie roho yake na dhamira yake kuwataja watu waliomfanyia unyama ule ili jamii ijue na pengine ndio utakuwa mwisho wa watu kufanyiwa vitu vya aina hii,” alisema Ruhuza.

Ruhuza alisema kuwa kiongozi huyo wa madaktari amerejea huku akiwa na afya njema, lakini bado ana deni kwa watu wasiopenda vitendo vya unyanyasaji.“Ndiyo maana nikasema azungumze jambo hili kutoka ndani ya moyo wake,” alisema Ruhuza.Mtikila alisema licha ya kwamba Dk Ulimboka anatakiwa kuwataja waliomfanyia vitendo hivyo, yaliyomkuta yanatakiwa kupelekwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki za Binadamu.“Nimeshazungumza na mtu mmoja kutoka mjini London, Uingereza amesema kuwa jambo hilo linawezekana,” alisema Mtikila.Alifafanua kwamba, atafanya kila njia ili akutane na Dk Ulimboka na kumshawishi akafungue kesi katika mahakama hiyo ili liwe fundisho kwa wanaopenda kuwanyanyasa Watanzania wanaodai haki zao.

“Nitafanya kila njia ili nionane na Ulimboka, hili jambo ni lazima lifike katika mahakama ya kimataifa ya haki za binadamu…, pia anatakiwa kuwataja waliomfanyia unyama huu,” alisema Mtikila.

Kwa upande wake, Mtatiro alisema kuwa Ulimboka anatakiwa kukutana na vyombo vya habari na kueleza mambo yote ili kufichua yaliyokuwa yakifichwa na vyombo vya usalama.

“Ukweli utamweka huru na utawaweka huru watu wengi ambao wanaweza kufanyiwa unyama siku zijazo. Ikiwezekana afungue kesi ili haki itendeke,” alisema Mtatiro na kuongeza:“Ulimboka anatakiwa kufahamu kwamba Watanzania hawakukubaliana na mateso aliyopewa, unyama aliofanyiwa unalaaniwa na kila mtu,” alisema Mtatiro.

Habari hii imeandikwa na Fidelis Butahe, Aidan Mhando, Joseph Zablon, Geofrey Nyang’oro, Boniface Meena na Leon Bahati.

Serikali Imewafukuza Kazi Watumishi Watatu Wa Wizara Ya Maliasili Na Utalii Kufatia Sakata La Usafirishaji Wa Wanyama Pori


Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu uamuzi wa Serikali wa kuwafukuza kazi watumishi watatu wa wizara hiyo kutoka na ukiukaji wa sheria na utekelezaji wa majukumu yao ya kazi kufuatia sakata la usafirishaji wa wanyama pori kupitia Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro kwenda Quatar.

Wizara ya Maliasili na Utalii imechukua hatua za kinidhamu kwa watumishi wake tisa (9) kufuatia kadhia ya utoroshaji wa Wanyamapori Hai katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na masuala mengine yanayohusu Wanyamapori. Watumishi hao wamechukuliwa hatua husika kufuatia kukamilika kwa uchunguzi wa tuhuma zilizokuwa zikiwakabili.

(1) Waliofukuzwa kazi kutokana na ukiukaji wa sheria katika utekelezaji wa majukumu yao ni:

- Bw. Obeid F. Mbangwa - Mkurugenzi wa Wanyamapori. Wakati wa kadhia hiyo alikuwa Mkurugenzi Msaidizi Matumizi ya Wanyamapori,

- Bw. Simon Charles Gwera – Ofisi ya Uwindaji wa Kitalii – CITES na Utalii wa Picha Arusha,

- Bw Frank Mremi - Ofisi ya Uwindaji wa Kitalii – CITES na Utalii wa Picha Arusha.

(2) Aliyeondolewa Cheo cha Madaraka kutokana na kutochukua hatua kamilifu za ulinzi ambazo zingeweza kuzuia kutokea kwa tukio la utoroshwaji wa wanyama ni:

- Bw. Bonaventura M.C. Midala – Mkurugenzi Msaidizi, Undelezaji Wanyamapori. Wakati wa tukio alikuwa Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Kuzuia Ujangili.

(3) Wafuatao ni Maafisa Wanyamapori Daraja la II waliotekeleza maelekezo ya Wakuu wao wa kazi yaliyo kinyume cha Sheria ambao wamepewa Onyo Kali la Maandishi:

- Bibi Martha P. Msemo - Afisa Leseni, Ofisi ya Uwindaji wa Kitalii, CITES na Utalii wa Picha Arusha.

- Bibi Anthonia Anthony – Afisa Leseni, Ofisi ya Uwindaji wa Kitalii, CITES na Utalii wa Picha Dar es Salaam.

(4) Bw. Silvanus Atete Okudo ni Mkuu wa Kituo cha Uwindaji wa Kitalii, CITES na Utalii wa Picha Arusha aliyeshindwa kufuatilia kupata maelekezo ya Mkurungezi wa Wanyamapori kuhusu mtumishi wake aliyekiuka Sheria katika utoaji wa vibali. Aidha, alishindwa kupeleka kwa Katibu Mkuu taarifa kuhusu mtumishi huyo ili achukuliwe hatua za nidhamu.

- Silvanus Atete Okudo – amepewa Onyo Kali la Maandishi.

(5) Wafuatao ni Maafisa ambao uchunguzi dhidi yao unaendelea:

- Bw. Mohamed Madehele – Ofisi ya Matumizi Endelevu ya Wanyamapori

- Bibi Mariam Nyallu – Kituo cha Uwindaji wa Kitalii, CITES na Utalii wa Picha – Arusha.

Wahusika wengine katika kadhia hiyo wasiokuwa waajiriwa wa Wizara ya Maliasili na Utalii watachukiliwa hatua na mamlaka nyingine husika.

Mhe. Khamis Suedi Kagasheki
WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII
13 Agosti 2012
Imetolewa kwenye Press Conference iliyofanyika Katika Viwanja vya Bunge Dodoma tarehe 13 Agosti 2012)