Friday, August 17, 2012

President Kikwete Attends The 32nd Ordinary Summit Of Heads Of State And Government Of SADC In Maputo


Presiddent Dr.Jakaya Mrisho Kikwete left front row in a group photo with other SADC Heads of State and Government during the opening session of the 32rd Ordinary Summit of Heads of State and Government of SADC in Maputo today.
 President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete in conversation with the South African President Jacob Zuma  during the 32nd Ordinary Summit of Heads of State and Government of the Southern African Development Community(SADC) in Maputo

President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete together with Namibian President Hifikepunye Pohamba in intimate conversation during the opening ceremony of the 32nd Ordinary Summit of Heads of State and Government  of SADC in Maputo today.
                 
Photos by Freddy Maro

TANESCO WAZIDI KUKAMATA WEZI WA UMEME

Fundi wa Tanesco aking'oa moja ya mita iliyokutwa na ghost token katika jengo la Sophia Chang'ombe jijini Dar es Salaam.
 Mita za umeme ambazo zinatuhumiwa kuhusika na wizi huo
..............................
Huku shirika la umeme nchini TANESCO likielemewa na mzigo wa madeni na kashfa za vigogo kufuja fedha wateja nao wameanza kuliibia shirika hilo umeme hatua ambayo ilishawahi kumfanya aliyekuwa Mkurugenzi wa TANESCO wakati fulani kuingia mtaani kushuhudia mwenyewe jinsi wezi wa umeme wanavyoiba.
 
 TANESCO imekuwa kwenye kampeni ya kuwabana wezi wa Umeme unaweza kutembelea tovuti ya Shirika la Umeme Nchini kuweza kupata habari mbalimbali kuhusiana na Shirika hilo

Wizara Ya Nishati Na Madini Yakanusha Uchimbaji Wa Madini Ya URANI Kuanza



Tarehe 16 Agosti, 2012 gazeti la Rai Toleo Na.986 katika ukurasa wake wa kwanza na watatu lilichapisha taarifa yenye kichwa cha habari “UCHIMBAJI WA URANI SERIKALI YAONYWA” na kuwa kumezuka sakata lingine ambapo kampuni ya kigeni imeanza kuchimba madini hatari aina ya urani kwa kile wachunguzi wanasema ni kinyume cha sheria.

Gazeti hilo liliendelea kuandika kwamba Tanzania haina sera ya urani na kwamba hata kama Serikali imeruhusu uchimbaji huo, ni kinyume cha sheria kwa sababu hata Serikali yenyewe haijatunga sheria ya uchimbaji urani. Tunasema habari hii ina malengo ya kuupotosha umma.Mwandishi wa habari hii bila ya kutaja jina lake anaeleza kuwa hakuweza kuwasiliana na viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini licha ya yeye kuwaandikia ujumbe kitu ambacho hakina ukweli. Kutokana na unyeti wa habari yenyewe mwandishi alipaswa kuhakikisha anapata taarifa kamili kutoka Wizarani na siyo kutoa taarifa kwa matakwa binafsi.Habari hii imelenga zaidi katika kuupotosha umma badala ya kuuelimisha kama ambavyo mwandishi ameshindwa kueleza kwa ufasaha ni nini hasa kusudio lake.

Tunaheshimu Uhuru wa vyombo vya Habari na tungependa kama kuna suala lolote linalohitaji ufafanuzi, Wizara ipo tayari muda wowote kutoa maelezo badala ya kukimbilia kuandika habari zinazojichanganya na kusababisha usumbufu kwa wananchi.

Tunatumia fursa hii kwa mara nyingine kuufahamisha umma kuwa kama Mheshimiwa Waziri wa Nishati na Madini Mhe: Prof Sospeter Muhongo alivyosema kwenye hotuba ya bajeti ya mwaka huu kuwa pamoja na kuwepo kwa maeneo mbalimbali hapa nchini yenye madini ya urani ni maeneo mawili yaani Wilaya ya Namtumbo na Manyoni ndiyo yaliyothibitishwa kuwa na kiasi cha kutosha kuweza kuchimbwa kibiashara na si kweli kuwa uchimbaji umeanza.

Eneo la Namtumbo lipo ndani ya Hifadhi ya Taifa na Serikali iliwasilisha maombi UNESCO ya kurekebisha mipaka ya eneo la hifadhi ya Dunia ili kuongeza eneo la mradi, ombi liliridhiwa katika kikao cha UNESCO cha tarehe 02/Julai, 2012 kilichofanyika Saint Petersburg (Urusi).Aidha, Sera ya Madini ya Mwaka 2009 na Kanuni za Madini ya Mionzi Ayonisha za Mwaka 2010 - the Mining (Radioactive Minerals) Regulations, 2010 chini ya Sheria ya Madini, 2010 zinatumika katika kusimamia shughuli za utafutaji na uchimbaji wa madini ya urani nchini. 

Sheria na Kanuni zote zilizotungwa na zitakazoendelea kutungwa zinazohusiana na usimamizi wa madini ya urani pamoja na mambo mengine zinalenga kuzingatia miongozo/taratibu za Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki (IAEA) za usimamizi wa madini hayo zinazohakikisha kuwa uchimbaji hauleti athari kwa binadamu na mazingira.Tunaendelea kuwashauri waandishi wa habari kuwa sisi kama wizara na chombo cha Serikali tunawajibu wa kuelimisha umma juu ya shughuli mbalimbali za wizara hivyo tunawashauri kuwa tushirikiane kwa maslahi ya Taifa badala ya kutoa habari zenye malengo binafsi.

Imetolewa na:Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Nishati na Madini

Lowassa Awataka Viongozi Wa Morogoro Kushughulikia Tatizo La Uchomaji Moto Misitu


  Mh.Lowassa akiangalia madawati yaliyokabidhiwa kwa shule hiyo na benki ya KCB hivi karibuni.
Waziri Mkuu mstaafu Mh Edward Lowassa akiwasalimia wanafunzi wa shule ya msingi ujirani katika eneo la wafungaji wa jamii ya wamasai kata ya mkundi wilaya ya Morogoro alikokwenda kukagua na kukabidhi harambe za wafugaji hao kwa ajili ya ujenzi wa shule yao hiyo Waziri mkuu mstaafu mh Edward Lowassa ameuomba uongozi wa mkoa wa Morogoro kulishughulikia tatizo la uchomaji moto misitu.
 Waziri Mkuu mstaafu Mh Edward Lowassa akikabidhiwa kibuyu na mama wa kimasai kata ya Mkundi wilaya ya Morogoro.

Akizungumza mapema leo kwenye kijiji cha Kiegea mjini Morogoro,Mh.Lowassa  ametoa wito huo alipokuwa akikabidhi michango ya harambee ya wafugaji wa jamii ya  Wamasai,kusaidia ujenzi wa shule ya msingi kijijini hapo.Mh Lowassa alialikwa kufanya kazi hiyo akiwa ni kiongozi wa jamii ya wamasai nchini.

Mh.Lowassa pia aligusia suala la baadhi ya wanchi kuwa na tabia ya kuchoma moto misitu hovyo hasa mkoa wa Morogoro,hali inayopelekea uharibifu mkubwa wa Mazingira,Lowassa amebainisha kuwa kila anapopita mkoani morogoro amekuwa akishuhudia misitu ikichomwa moto,hali iliyokuwa ikimhudhunisha sana.

''Nimekuwa nikishuhudia maeneo kadhaa ya misitu yakichomwa moto,kwa hivyo ndugu zanguni naomba tuachane na tabia hii pamoja na kuwa kilimo ni muhimu katika maisha yetu ya kila siku,lakini kwa njia hii tutaufanya mkoa huu wa Morogoro ugeuke jangwa'' alionya Lowassa na kuongeza kuwa iwapo mwanamuziki maarufu wa mkoa huo, Marehemu Mbaraka Mwinshehe angefufuka angesikitika sana.

''Mara nyingi nikikutana na hali hii,huwa naukumbuka wimbo wa Mbaraka Mwinshehe unaosema kuwa Morogoro maji yatiririka milimani, kama akifufuka atalia'' alisema Lowassa na kuuomba uongozi wa mkoa kushirikiana kwa pamoja kutafuta suluhisho la tatizo hilo ambalo limekuwa likikithiri siku hadi siku.''Mh DC wa Morogoro nawaombeni mtafute suluhisho la tatizo hili, tusipoangalia mkoa huu utakuwa jangwa''alisema.

Aidha Mh.Lowassa amesema kuwa suala la elimu ni muhimu zaidi kabla ya kilimo kwanza,akaongeza kuwa Elimu kabla baadaye kilimo kwanza.Mh Lowassa pia ametoa changamoto kwa wananchi wa kata mpya ya mkundi ya jamii hiyo ya wafugaji kuanza ujenzi wa shule ya sekondari ya kata.

''Ni aibu kata hii kutokuwa na shule ya sekondari wakati kila kata nchini ina shule ya sekondari ,ambako hivi sasa angalau kuna usawa kwa watoto kugusa elimu ya sekondari'' alisema na kuongeza kuwa atakuwa tayari kuja kwenye kata hiyo Januari mwakani kuongoza harambee ya kuchangisha fedha za ujenzi wa sekondari.Mh.Lowassa ndiye aliyeongoza operesheni ya ujenzi wa shule za kata kote nchini wakati alipokuwa waziri mkuu.

''Niko tayari kuja January kuongoza harambe ya kuchangisha fedha, ni aibu kwakweli sijafurahishwa na hali yenu hapa mnatakiwa nyinyi wenyewe msimame kidete kujiletea maendeleo, njooni Monduli mjifunze jinsi wafugaji wenzenu walivyoweza kutumia mifugo yao kujenga shule na nyumba za waalimu'' alisema Lowassa.

Mh.Lowassa amemtaka kila mfugaji kutoa ng'ombe au mbuzi mmoja kwa ajili ya kuchangia elimu kwenye kata yao na kumuomba mkuu wa wilaya kutumia sheria zilizopo kumkamata na kumtia ndani yeyote atakayekaidi wito huo.

Mh Lowassa alichangia mabati 500 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa madarasa ya shule hiyo ya msingi ya Ujirani yenye wanafunzi 414 ,lakini yenye upungufu mkubwa wa Waalimu, wawili tu mmoja wa kuajiriwa na mwingine wa kujitolea.

Katika harambee ya wananchi wa eneo hilo walichanga ng'ombe watano kwa ajili ya kuendeleza shule hiyo, idadi ambayo mh Lowassa aliipinga,akidai kuwa ni Wanachi hao wana idadi kubwa ya mifugo hivyo walipaswa  kujitolea zaidi.

Wabunge CCM Wahaha Kujikosha Na Ufisadi


TUHUMA za rushwa dhidi ya wabunge juzi zilitawala kikao cha Kamati ya Wabunge wa CCM, ambapo Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliombwa kuingilia kati ili ‘kuwasafisha’ wenye tuhuma hizo mbele ya jamii. Kikao hicho kiliitishwa pamoja na mambo mengine, kuzungumzia nafasi ya wabunge wa CCM katika kuhamasisha umma kushiriki katika Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika Agosti 26, mwaka huu na utoaji wa maoni kwa Tume ya Katiba Mpya.

Habari kutoka ndani ya kikao hicho, zimesema pamoja na kwamba haikuwa moja ya agenda za mkutano huo, Mbunge wa Bukene, Seleman Zedi alisimama na kuibua kilio cha wabunge wanaotuhumiwa kwa rushwa. Mbunge huyo ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini iliyovunjwa na Spika wa Bunge, Anne Makinda alimweleza Waziri Mkuu kwamba baadhi ya wabunge, hasa wa iliyokuwa kamati yake, wangekwendaje kuhamasisha Sensa majimboni wakati wamechafuka kwa tuhuma za rushwa?

Mtoa taarifa wetu anasema, mbunge huyo akiungwa mkono na Mbunge wa Viti Maalumu, Munde Tambwe, walimwomba Waziri Mkuu ambaye ni mwenyekiti
wa kikao hicho, amweleze Spika awasafishe kwa kutangaza bungeni kwa madai kuwa tuhuma dhidi yao hazikuthibitika.

Alisema kauli hiyo ya Spika ingewasaidia kurudi majimboni wakiwa wasafi na wenye mamlaka ya kimaadili kuungana na wenzao kuhamasisha Sensa na utoaji wa maoni ya Katiba Mpya. Hata hivyo, vyanzo vyetu vya habari vimetofautiana kuhusu kauli ya Pinda baada ya kupokea malalamiko hayo, kimoja kikisema alikaa kimya na kingine kikisema alijibu kuwa asingeweza kuingilia kati suala hilo kwa kuwa bado linachunguzwa na Kamati ndogo ya Bunge. Mambo mengine yaliyoibuka kwenye kikao hicho ni mjadala wa Muswada wa Fedha.

Wabunge wa CCM walipinga ongezeko la kodi kwenye maji ya kunywa na msamaha wa Kodi ya Ongezeko la Thamani (Vat) kwa kampuni za kuchimba madini. Kwa zaidi ya wiki sasa, Kamati ndogo ya Bunge iliyoundwa na Spika Makinda imekuwa inaendelea kuwahoji baadhi ya wabunge ama wanaotuhumiwa au wenye ushahidi wa tuhuma hizo. Baadhi ya wabunge wamekuwa wakiitwa mmoja baada ya mwingine na kuhojiwa na wajumbe hao faragha kuhusu ama madai ya rushwa dhidi yao au mambo waliyoeleza kuhusu tuhuma hizo. Tuhuma hizo zilisababisha Spika Makinda kuvunja Kamati ya Nishati na Madini iliyodaiwa kukithiri kwa rushwa.

MABANGO YA WAGANGA WA KIENYEJI HATIMAYE YAHOJIWA BUNGENI

 Mabango ya matangazo ya waganga yaliyotapakaa kila kona ya Jiji la Dar es Salaam wakitangaza kazi zao katika jamii hatimaye yameaanza kuhojiwa huko Bungeni pale MBUNGE wa Viti Maalumu, Bety Machangu (CCM)alipouliza swali Bungeni “Je, serikali inaruhusu matangazo hayo? Na ni kweli kwamba waganga hao wanatibu magonjwa hayo ama wanawadanganya wananchi tu?” alihoji mbunge huyo.
Hili ni mojawapo ya mabango hayo yanayohojiwa  huyu yeye akiorodhesha vile anavyotibu  huku UKIMWI akionekana kuutilia msisitizo wakati  wanasayansi wa Taasisi ya Magonjwa ya Kuambukiza na Mzio (Niaida) ya Marekani, akisema kuwa tiba hiyo inaweza kutibu ugonjwa huo hatari kwa asilimia 90  mwezi mei walitangaza kupata tiba hiyo hatujui Dr.Ngulumo aligundua lini tiba hiyo ? Ukweli ni kwamba Dawa ya UKIMWI-Huu ndi ukweli soma upate maarifa zaidi la sivyo utapotea.


 Hayo ndio mabangozz..!! yaliyoja kila kona ya Jiji la Dar es Salaam.

PICHA 11 ZA RVP AKIWA KWENYE SIKU YA KWANZA YA MAZOEZI NA MAN UTD!












CHADEMA YAZIDI KUJIKUSANYIA WANACHAMA - Kilosa


Vuguvugu la M4C linaloongozwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA limeonekana kutikisa chama cha wananchi CUF wilayani Kilosa ambapo mbali ya wanachama wengi sana wa CUF kujiunga CHADEMA pia Mjumbe wa mkutano Mkuu CUF Taifa Bwana Wille Lemi alijitoa rasmi katika CUF na kukabidhiwa kadi na Kiongozi wa upinzani nchini ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa.

Katika mkutano huo Dr Slaa aliwataka wananchi wa vyama vyote kuunganisha nguvu kwa pamoja chini ya vuguvugu la M4C ili kuhakikisha katika uchaguzi mkuu ujao wananchi wanapata serikali itakayojali maslahi yao chini ya CHADEMA.

Dr Slaa pia alishukuru mwitikio wa wanakilosa kutokana na mkutano huo kufurika umati mkubwa wa watu.Mbali na CUF kupoteza wanachama wengi pia mamia ya wanaCCM walikihama chama chao na kujiunga rasmi CHADEMA kuunganisha nguvu katika vuguvugu la M4C.Idadi ya wanachama wapya waliojiunga CDM katika mkutano wa Kilosa ulikuwa zaidi ya elfu moja.
Kilosa ilikuwa ni mojawapo ya maeneo yenye wanachama wengi wa CUF lakini inaonekana ziara ya Dr Slaa imesimika rasmi CHADEMA kama chama kinachopendwa zaidi Kilosa.
Kutoka Chademablog

Mkuu Wa Mkoa Wa DSM Ahimiza Sensa Ya Watu Na Makazi



Na. Aron Msigwa -MAELEZO.
Zikiwa zimebaki siku chache kabla ya kuanza kwa zoezi la Sensa ya watu na makazi nchini, mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki ametoa wito kwa wakazi wa mkoa huo kutoa ushirikiano kwa makarani wa sensa watakaoendesha zoezi hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam amesema maandalizi ya ukamilishaji wa zoezi hilo yanaendelea vizuri na kuongeza kuwa Waziri mkuu Mizengo Pinda anatarajia kuzindua kampeni ya uhamasishaji wa watu kushiriki katika zoezi hilo kesho (17/8/2012) katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.

Ametoa onyo na kuvitaka vikundi vya baadhi ya viongozi wa dini na wananchi wanaowahamasisha wananchi kutoshiriki katika zoezi hilo katika maeneo yao kuacha mara moja kwani zoezi hilo lipo kwa mujibu wa sheria namba 1 ya mwaka 2002.

"Natoa onyo kwa kikundi chochote kinachoendesha kampeni ya kuwahamasisha wananchi kutoshiriki kwenye zoezi la Sensa ya watu na makazi katika mkoa wa Dar es salaam kuacha mara moja kwani zoezi hilo lipo kwa mujibu wa sheria na yeyote atakayekaidi au kukwamisha zoezi hilo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake" amesema.

Amesema kuwa Zoezi la Sensa sio la mtu mmoja mmoja wala kikundi fulani bali ni suala la watanzania wote bila kujali dini, rangi wala kabila, hivyo watu wanaopinga zoezi hilo wanavunja sheria za nchi.

Naye mratibu wa zoezi la Sensa kwa mkoa wa Dar es salaam Bi. Magreth Stephen Mganda amesema mpaka sasa mkoa wa una jumla ya makarani na wasimamizi 18,993 watakaoshiriki zoezi la kuhesabu watu wakiwemo 90 wa akiba.

Amesema kati ya hao 644 wanatoka wilaya ya Kinondoni,365 wanatoka Ilala na 530 kutoka wilaya ya Temeke.

Katika hatua nyingine mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Bw. Saidi Meck Sadiki ametoa ufafanuzi wa vitendo vya vurugu,uharibifu na uporaji wa mali za wanachi katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Dar es salaam hususan wilaya ya Temeke na Kinondoni.

Amesema kuwa vitendo hivyo vilivyotokea ni kinyume cha sheria na kutoa onyo kwa wale wote waliohusika kuvamia maeneo na kuchukua ardhi kwa nguvu pasipo kufuata utaratibu kuacha mara moja.

Amesema kuwa wale waliovamia maeneo hayo bila kufuata utaratibu waondoke wenyewe na kukubali kutii sheria bila shuruti kwa kuwa serikali haitamvumilia mtu yeyote anayevunja sheria.

"Wale wote waliovamia maeneo hayo katika mkoa wa Dar es salaam katika maeneo yote yenye vurugu waondoke wenyewe , watii sheria kwa sababu vitendo vya namna hii ni vya kiharifu na kamwe serikali haiwezi kuvivumilia" amesisitiza.

Ameongeza kuwa tayari mahakama imeshatoa mwongozo kuhusu maeneo hayo na kubainisha kuwa wote waliohusika na watakaoendelea kuvunja sheria katika maeneo hayo watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

HABARI NDIO HIYO...!


The first picture - Robin van Persie signs for Manchester United -
Habari ndio hiyo Robin Van Persie akisaini mkataba wake Man U akiwa na Sir.Alex Ferguson
ni mkataba wa miaka mi nne.
all the best RVP.

Kipengele Cha Dini Chakataliwa Rasmi Sensa


Waziri mkuu anahutubia sasa hivi mnazi mmoja juu ya sensa.ameorodhesha maswali yatakayohojiwa lakini kipengele cha dini hakitakuwepo

Rufaa Ya Lema Tarehe 20 Sept



RUFAA ya kupinga kuvuliwa ubunge ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA), imepangwa kusikilizwa Septemba 20, mwaka huu, mbele ya majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa; Natalia Kimaro, Mbarouk Salim Mbarouk na Salumu Massati.
Kwa mujibu taarifa za kikao cha Mahakama ya Rufaa cha Arusha, rufaa hiyo iliyofunguliwa na Lema akipinga uamuzi uliotengua ubunge wake kufuatia shauri lililofunguliwa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, inatarajiwa kusikilizwa kwa siku moja ambapo baada ya hapo itapangwa tarehe kwa ajili ya kutoa uamuzi.

Awali, Lema kupitia wakili wake, Method Kimomogoro, aliwasilisha kwenye mahakama hiyo hoja 18 za madai akipinga kutenguliwa kwa ubunge wake na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Aprili 5, mwaka huu.

Kwenye baadhi ya madai hayo, Lema aliiomba Mahakama ya Rufaa kutengua uamuzi wa Mahakama Kuu, uliotengua ubunge wake, huku akiitaka imtangaze kuwa mbunge halali wa Jimbo la Arusha Mjini.

Aidha, aliitaka mahakama hiyo ya juu, iwaamuru walalamikiwa katika shauri hilo walipe gharama za rufaa hiyo pamoja na zile za kesi iliyomalizika kwenye Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.

Katika madai mengine, Lema anamlalamikia, Jaji Gabriel Rwakibarila, aliyesikiliza kesi hiyo kuwa, alitoa uamuzi wake kwa kuzingatia maneno ya uvumi, huku akipuuza ushahidi uliotolewa mahakamani hapo.

Lema anadai kuwa, Jaji alikosea wakati alipoamua kuwa mpiga kura yeyote anaruhusiwa kupinga matokeo ya uchaguzi hata kama haki zake za msingi hazijaguswa.

Kesi hiyo iliyotengua ubunge wa Lema, ilifunguliwa na wanachama watatu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM); Mussa Mkanga, Agness Mollel na Happy Kivuyo, wakidai kuwa wakati wa kampeni mbunge huyo alimdhalilisha mgombea mwezake, Dk. Batilda Burian kwa kutumia lugha za matusi.

ANGALIZO
Jaji Mbarouk Salim Mbarouk ni yule aliyeonekana kutajwa kwa namna isiyo nzuri kwenye utetezi wa Tundu Lisu au ni mwingine? na kama ni yeye hiyo haitaleta tena kutoridhika iwapo maamuzi hayatakuwa upande wa Lema na Chadema? nini mawazo yenu katika hili? 
Bush Lawayer

KATUNI: BEI YA NGUO YAZIDI KUPANDA MITAANI


JIONEE MWENYEWE: TANGU SIKU YA KWANZA ALIPOSAJILIWA MPAKA ANAPOONDOKA ARSENAL - ROBIN VAN PERSIE


Siku akiwa anatambulishwa katika uwanja wa zamani wa Arsenal Highbury

Mazoezini siku ya kwanza

Akisherehekea moja ya makombe yake ya kwanza kabisa kushinda akiwa na Arsenal - kombe la FA Cup baada ya kuifunga Manchester United kwa penati 5-4



Majeruhi yalipoanza kumuandama

Moja ya magoli bora kabisa akiwa na Arsenal - hapa akiwatungua Charlton

Aliposhea uwanja na Thierry Henry katika awamu ya kwanza

Hapa ni baada ya kwenda kumsalimu golikipa wa Edwin Van Persie.

Hapa ni baada ya kuwafunga mabao mawili Chelsea kwenye uwanja Stamford Bridge.

Hapa ni baada ya kufungwa na Bolton kwenye mchezo wa fainali.

Kadi yake nyekundu aliyopewa kwa maamuzi ya utata dhidi ya Barcelona.

Akiombwa asiondoke

Akiwafunga mahasimu wao wakubwa Tottenham

Akishangilia magoli yake mawili aliyoyafunga dhidi ya Chelsea kwenye uwanja


Hapa ndipo Majeruhi yalipoanza kushikakasi

Siku ya mwisho aliyoyafanya mazoezi  na Arsenal huko Ujerumani.
Akiwa na viongozi wake wapya wa MAN UTD

CRISTIANO RONALDO KWA TIMU INAYOMTAKA INATAKIWA KULIPA €1 BILLION


Kila mchezaji anayo bei yake, ingawa vilabu vimekuwa vikijaribu kila njia kuweza kukaa na  wachezaji wao muhimu, lakini siku zote inakuwa ngumu jambo lililopelekea kuwa zinawawekea vipengele vya beighali ikiwa kuna klabu itakuja kuwataka kuwanunua wakiwa bado kwenye mkataba husika.  
 Kupitia utafiti mdogo uliofanyika tumeweza kugundua na kupata kujua ni wachezaji  gani wanaongoza kwa kuwekewa vipengele vya kuuzwa fedha nyingi kuliko wenigne.


Cristiano Ronaldo
€1bn
 

Lionel Messi
€250m
 

Fernando Torres
€127m
 

Hulk
€100m
 

Thiago Alcantara
€100m