Monday, August 13, 2012

KUMEKUCHA JIJI LA MWANZA BARABARA ZAZIDI KUKARABATIWA

Mafundi wa kampuni ya Jasco wakiendelea na ujenzi wa barabara ya Libert jijini Mwanza.

Barabara ya Libert kutokea barabara ya Uhuru inavyoonekana sasa kufuatia kuendelea kwa ujenzi wake unaofanywa na kampuni ya Jasco ya jijiniMwanza.

Eneo la barabara ya Uhuru kuelekea Mlango mmoja jijini Mwanza, ambalo limekuwa ni sehemu korofi ambapo kwa sasa inakarabatiwa kutokana na kuwa kero kubwa wakati wa mvua zinaponyesha.

Mafundi wakitandaza nondo ili kumwaga zege kudhibiti eneo hilo katika barabara ya Uhuru jijini Mwanza ambalo limekuwa kero kupitika wakati wa mvua zinaponyesha.

WEMA: HUYO WEMA WA FACEBOOK NI TAPELI


 
Na Gladness Mallya

STAA wa filamu nchini, Wema Sepetu ameamua kufunguka kwa kusema kuwa anakerwa na watu wanaotumia jina lake katika mitandao mbalimbali ya kijamii ukiwemo wa Facebook, kwani wanamuharibia mambo yake mengi.

Wema ameliambia gazeti hili kuwa ana zaidi ya miezi 12 tangu alipojitoa…kwenye mtandao wa Facebook, lakini bado kuna mtu anatumia jina lake vibaya kwa kuomba fedha kwa watu jambo ambalo linamkera kupita kiasi kwani amekuwa akipigiwa simu na watu wakimuuliza kulikoni.
“Yaani nakerwa sana na watu wanaotumia jina langu kutapeli au kuomba fedha kwenye mtandao,
“Mashabiki wangu wakiona mtu anatumia jina langu kwenye Facebook wajue huyo ni tapeli na siyo mimi,” alisema Wema.

Mrwanda, Mbiyavanga watemwa


 
Danny Mrwanda.
Khatimu Naheka na Wilbert Moland

WACHEZAJI wawili wa Simba, Danny Mrwanda na Kanu Mbiyavanga wametemwa kwenye kikosi hicho.

Simba iliwasajili wachezaji wote wawili kwenye usajili huu, lakini baada ya kuwapa nafasi kwenye michezo kadhaa na…

Tegete, Shamte safari imeiva Toto


 
Jerry Tegete.
Na Lucy Mgina

MAJINA ya wachezaji watano wa Yanga likiwemo la mshambuliaji Jerry Tegete (pichani), yamewasilishwa kwenye dawati la Toto African tayari kwa kujiunga na timu hiyo kwa mkopo.

Ukiacha Tegete, wachezaji…

NAVIJUA VITU TISA KUHUSU WEWE


Navijua vitu 9 kuhusu wewe
1. Unasoma hii habari.
2. Wewe ni binadamu hai kabisa.
3. Huna jeuri ya kusema PIPI bila kufungua mdomo
4. Hahaha nakuona umejaribu kusema PIPI...
6. Unajicheka ujinga.
Nimeyaona meno yako
7. Unatabasamu umeruka Na.5
8. Hahaha unacheki kama kuna namba 5
9. Umetabasamu

Okwi: Sijasaini Simba, naondoka


Emmanuel Okwi.
Na Wilbert Molandi

SIKU chache baada ya kujiunga na klabu yake ya Simba akitokea kwenye majaribio nchini Austria, kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Emmanuel Okwi, amesema bado hajaongeza mkataba wa timu hiyo na pia anatarajiwa kuondoka tena kwa ajili ya kufanya majaribio ya kucheza soka…

Mbowe;- Siongozi Genge La Wasaka Vyeo

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA Freemaan Mbowe amesema kamwe haongozi kundi au genge la wasaka vyeo na madaraka ndani ya chama chake bali anaongoza kundi la watu wanaopenda mabadiliko.Kiongozi huyo amesema binafsi hawezi kwa sasa kusema atagombea Urais au Ubunge kwa sababu huu si muda wake hata kidogo.

Mbowe amesema mwanachama yeyote makini wa Chadema kwa sasa ni muda wa kuwaunganisha wanachama na watanzania kwa ujumla na wala si muda wa kuwagawa kukimbilia madaraka. Kiongozi huyo amesema ndiyo maana makamanda wote wakiongozwa na Dr Slaa wamejichimbia vijijini kwa kazi moja tu ya kueneza vuguvugu la mabadiliko-M4C.

Chanzo: Tanzania Daima.

Chelsea 2-3 Manchester City: Tevez, Yaya Toure and Nasri down 10-man Blues



The Premier League champion was in fine form at Villa Park on Sunday and produced the first psychological blow of the new season by coming from behind to secure victory.

Roberto Mancini may believe Manchester United is the favorite to win the league this season, but his City side was in fine form at Villa Park and dominated this feisty match despite falling behind to Fernando Torres’ 40th minute strike.

Yaya Toure, Carlos Tevez and Samir Nasri struck three superb goals after the break as City took advantage of space in the Chelsea defense created by the red card shown to Branislav Ivanovic in the 42nd minute for a horrible studs-up challenge on Aleksandar Kolarov.

Ryan Bertrand grabbed a late goal back for Chelsea but City held on comfortably to complete a successful day following the news that the club had agreed a fee with Everton to sign Jack Rodwell.

There was certainly nothing charitable about the traditional season curtain raiser as fierce challenges flew in with almost the same ferocity as the rain pounding down in the west Midlands.

Nigel De Jong set the tone with a lunging foul on Frank Lampard, while City defender Stefan Savic was booked as he took out his frustration on Eden Hazard’s ankle.

Thousands of supporters arrived late due to traffic on the M6, but they missed little action of note in the early stages as the champions of England and Europe cancelled each other out in a congested midfield.

In the third minute, Tevez forced the first save of note from Petr Cech with a free kick from the corner of the penalty area that curled over the wall but lacked the power to beat the Chelsea goalkeeper at his near post.

City looked rather uncomfortable defensively with the 3-5-2 formation deployed by Mancini, but they began to take control of proceedings, Nasri coming close but seeing his effort from a tight angle smothered by Cech.

Hazard, the only summer signing to start the match for either side, showed glimpses of his quality, taking the ball under pressure and using his skill to move the City defenders.

The 32 million pound Belgian is certainly confident in his own ability - but his first game on English soil is likely to be remembered for the moment in the first half when he fell flat on his face when attempting a back heel.

On 28 minutes, it was Hazard who drifted inside and fizzed a low shot towards the bottom corner of Costel Pantilmon’s goal, the first shot in anger from a Chelsea player.

Against the run of play, however, the Blues took the lead in the 40th minute, with Torres making a clear statement of his intent for the new season after winning the Golden Boot at Euro 2012.

Ramires did all of the hard work for the Spaniard, taking the ball on the edge of the penalty area and executing a neat reverse pass. Torres’ finish was masterly, a perfect first touch with his right foot and a deadly clipped finish with his left from eight yards.

Yet Chelsea’s celebrations were short-lived as Roberto Di Matteo’s side was reduced to 10 men less than two minutes later as Ivanovic was sent off. The Serbian’s studs-up lunge on Aleksandar Kolarov was dangerous, reckless and completely unnecessary and the fullback will now be suspended for three matches.

The extra man told as City dominated from the whistle after the re-start and drew level eight minutes into the second half. Yaya Toure, always the man for the occasion, collected a poor clearance from John Terry and swept the ball low into the corner from 20 yards, making the difficult look simple.

In the 58th minute, City took the lead with a goal that was as inevitable as it was brilliant. There seemed little danger when Tevez collected the ball on the left of the Chelsea box, but he cut across, past the dangling leg of David Luiz, before smashing a missile into the top corner.

Cech could only stand motionless as the striker wheeled away in celebration, the man who spent most of last season in Argentina dedicating his goal to the Fuerte Apache area where he grew up in Buenos Aires.

By now, there was no doubt of the outcome of the match, but Nasri added the finishing touch with a first-time volley on his left foot to turn in Kolarov’s cross following a sweeping move.

Chelsea substitute Ryan Bertrand grabbed a goal back for the Londoners in the 78th minute as he turned in a rebound from close range when Pantilimon made a mess of his attempt to save Daniel Sturridge’s shot.

But it was not enough and City deservedly saw the game out to land a psychological blow more telling than any of the physical combat on the pitch.

MAGAZETI LEO JUMATATU

















Familia Ya Mafisango Yatimuliwa Katika Nyumba Waliyokuwa Wakiishi...!

Baadhi ya vyombo vya ndani vya aliyekuwa kiungo mahiri wa Simba, marehemu Patrick Mafisango vikiwa nje ya nyumba aliyokuwa akiishi katika eneo la Keko Bora jijini Dar es Salaam, baada ya mwenye nyumba kuvitoa nje kutokana na deni la pango.
Orly Ilemba, akiwa nje ya nyumba aliyokuwa akiishi na marehemu kaka yake, Patrick Mafisango baada ya mwenye nyumba kutoa nje vyombo vya ndani kutokana na deni la pango.
Na: Andrew Chale
FAMILIA ya aliyekuwa kiungo mahiri wa mabingwa wa soka Tanzania Bara, Simba, marehemu Patrick Mutesa Mafisango iko katika wakati mgumu baada ya kutimuliwa katika nyumba waliyokuwa wakiishi, Keko Bora jijini Dar es Salaam.

Familia hiyo, ilitolewa nje vifaa katika nyumba hiyo na mmiliki wake, kutokana na kudaiwa kodi ya pango aliyokuwa akiudai kwa muda mrefu uongozi wa Simba.

Akizungumza kwa masikitiko makubwa, mdogo wa marehemu Mafisango, Orly Ilemba, alisema, mwenye nyumba huyo, Chingweni Mtoro, aliwafuata asubuhi na kutaka chumba chake kabla ya kutoa vitu hivyo nje ya chumba na kuweka kufuli jipya.
“Nipo nje tokea asubuhi, hatujafanya lolote, zaidi nalinda vitu vya marehemu, viongozi wa Simba kila nikijaribu kuwapigia simu hawapokei mpaka sasa sina la kufanya,” alisema Ilemba.

Alifafanua kuwa, viongozi hao wa Simba walijua mwisho wa kukaa humo, lakini wameshindwa kushughulikia suala hilo mapema mpaka wanakutwa na aibu hiyo.

“Lakini mwenye nyumba huyu, alisema mkataba huo ulitakiwa kufika mwisho Agosti 8, kama walivyokubaliana na viongozi wa Simba, lakini viongozi hao hawakuweza kumalizana naye ndio maana kaamua kufikia hatua hii,” alisema kwa masikitiko.

Mdogo huyo wa marehemu Mafisango, yupo nchini kwa ajili ya kusubiria rambirambi, ambazo klabu ya Simba iliahidi kuzitoa.

Juhudi za kuupata uongozi wa klabu ya Simba, kujua wana taarifa na wanachukua hatua gani, zilishindwa kuzaa matunda kwani wahusika, hawakupatikana.

Mafisango kati ya nyota mahiri waliochangia kwa kiasi kikubwa timu hiyo kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu msimu uliopita iliyofikia tamati Mei 6, alifariki dunia Mei 17, 2012 kwa ajali ya gari, eneo la Keko, jijini Dar es Salaam.

Juhudi za kuupata uongozi wa Simba kuzungumzia hali hiyo ilishindikana baada ya baada ya simu msemaji wa klabu hiyo, Ezekiel Kamwaga kutopatikana kwa siku ya jana.

 Picha kwa hisani ya http://francisdande.blogspot.com

Shangwe Na Majonzi Kwenye Mapokezi Ya Dr Ulimboka Alipowasili Nyumbani Jana!


Na, Waandishi wa Globalpublishers

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini Tanzania, Dkt. Ulimboka Stephen, amerejea salama nchini jana mchana na kutoa shukrani za dhati kwa Watanzania kwa dua na michango yao kuinusuru afya yake na kuahidi kuendeleza mapambano dhidi ya huduma bora za afya na maslahi kwa Madaktari.

Dkt. Ulimboka, aliwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere, saa 8:00 mchana na ndege ya Shirika la SA Airways, akitokea nchini Afrika Kusini, alipokwenda kwa matibabu.

Madaktari wenzake, ndugu, jamaa, marafiki, Wanaharakati na wananchi wengine, walimlaki kwa shangwe, hoihoi, nderemo huku wakiwa na mabango yenye ujumbe ambao GlobalPublishers.info imenukuu kuwa ulisomeka:

“DR. Ulimboka karibu nyumbani.”
“DR. Ulimboka, damu yako iliyomwagika inaamsha ari ya wananchi kudai haki ya afya.”
“DR. Ulimboka wewe ni mpigania haki ya afya bora kwa wananchi wote. Mungu na Watanzania wote tuko nawe.”

Kwa upande mwingine, Dkt. Ulimboka baada ya kukuta umati mkubwa uwanjani, alishindwa kujizuia, hivyo akatoa machozi kisha akasema: “Nawashukuru sana Watanzania kwa kuwa pamoja na mimi kwa maombi, sasa nimerejea nikiwa na afya njema, mapambano yanaendelea,” na kuongeza: “Watu wacheze na watu lakini wasicheze na Mungu, hasa Mungu wangu mimi.”

Serikali Kulipa Mishahara Ya Wafanyakazi TAZARA


Waziri wa Ujenzi, Dk Harryson Mwakyembe

WAZIRI wa Ujenzi, Dk Harryson Mwakyembe amesema serikali itabeba jukumu la kulipa mishahara ya wafanyakazi Shirika la Reli Tanzania na Zambia (TAZARA, baada ya wafanyakazi hao kucheleweshewa mshahara yao kwa kipindi cha miezi mitatu.

Kauli hiyo imekuja baada ya wafanyakazi wa shirika hilo kufikisha kilio chao kwa Waziri huyo kuwa wamekuwa wakiishi maisha ya kubangaiza kutoakana ucheleweshwaji wa mishahara yao.

Akizungumza na wafanyakazi hao, kwenye ofisi za Shirika hilo (TAZARA), jijini Dar es salaam jana, Dk Mwakyembe alisema akiwa waziri wa wizara hiyo anawaahidi hatakubali kuona wanaishi bila kulipwa mishahara huku wakifanya kazikwa juhudi.

Dk Mwakyembe alibainisha kuwa serikali imepokea kilio chao hivyo italipa sh bilioni1.3 kama mshahara wa miezi miwili kati ya miezi hiyo mitatu wanayodai kuanzia leo (jana).

Aliitaja miezihiyo itakayolipwa kuwa ni pamoja na Juni na Julai ambapo amewataka viongozi wa Shirika hilo kutoa maelezo kuwa ni kwanini hadi sasa hawajalipa mishahara wafanyakazi hao. 

Akizungumzia madai ya wafanyakazi hao ya kutaka kung’olewa madarakani kwa Mkurugenzi Mkuu,Mbegusita Akashambatwa na Naibu wake, Damus Ndumbalo, alisema shirika hili ni la kimataifa linalohusisha nchi mbili hivyo maamuzi yake ni lazima ya husishe viongozi wa pande zote mbili.

Aidha, alitoa onyo kuhusu vitendo vya hujuma ikiwa ni pamoja na wizi kuwa wale wote wanaojihusisha watambuwe kuwa dawa yao iko jikoni inachemka.


Katika hatua nyingine amesema amesikitishwa sana kuona kuwa wafanyakazi wa Mradi wa Ukarabati wa Train Mijini, hadi leo hawjalipwa mishahara ya miezi miwili,fedha hizo lilikwishatengwa.

“Nilisikitika sana kumkuta yule dada Mwanamisi akiwa amevaa overrol lake huku akiunganisha vyuma tena amefunga mfungo wa Ramadhani ambapo aliniambia tunafanyakazi lakini hatujalipwa mishahara inishangaza sana nataka walipwe haraka”alisema Dk Mwakyembe.
Awali Katibu Mkuu wa chama cha wafanyakazi shirika hilo, Ernest Kiwele, alisema wamechoshwa na tabia za viongozi hao kuwa wamekuwa chanzo cha matatizo yote yanayowakabili wafanyakazi hao.

Alisema Mkurugenzi Mkuu na Naibu wake wamekuwa wakiendesha Shirika hilo kwa kujali zaidi maslahi yao na jamaa zao hata wale waliosimamishwa kazi kwa kuwalipa mishahara.