Thursday, August 16, 2012

Majambazi wapora Sh. milioni 65 Dar

 
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela
Watu wanne wanaodaiwa kuwa ni majambazi wamepora Sh. milioni 65 kwenye kiwanda cha kutengeneza kinywaji cha Sayona, kilichopo eneo la Mwenge, jijini Dar es Salaam.
Tukio hilo lilitokea saa 8:00 machana baada ya majambazi hao kufyatua  risasi mara tatu hewani mfululizo kwa wakiwa wamesimama mbele gari la kiwanda  kiwanda hicho lililokuwa likitoka nje kupeleka pesa hizo kwa mhasibu wa kampuni ya M.M inayoshughulika na utengenezaji wa vifaa vya ujenzi.
Meneja masoko wa kampuni hiyo, Ragu Gadabi, alisema walinzi wake walimfungulia geti na kutoka nje ili kuwahisha pesa hizo. Alisema kuwa hatua chache nje ya geti, gari lenye  namba T640 MBZ aina ya RAV4 lilisimama mbele yake na kisha mtu mmoja alishuka na kugonga dirisha la gari lake.
“Sikuweza kufungua dirisha, lakini nilisikia milio ya risasi ikishambulia gari hilo, nilifanikiwa kutoka kwenye gari na kurudi kiwandani, lakini pesa na Laptop zote zimechukuliwa,” alisema na kuongeza: “Nilirudi kiwandani haraka kunusuru maisha yangu la sivyo wangepoteza uhai wangu, kitendo kilikuwa cha haraka mno yaani kufumba na kufumbua,” alisema Ragu.
Shuhuda ambaye hakupenda kutaja jina lake liandikwe gazetini, alisema majambazi hao walitokea barabara ya ITV na mara walipofika karibu na kiwanda hicho walisimama. Alisema muda mfupi baadaye aliliona gari likitoka kiwandani na kisha gari lililokuwa limesimama likalikinga gari hilo na kuanza kufyatua risasi na kufanikiwa kuchukua pesa na kompyuta ndogo.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwa Jeshi la Polisi linaedelea kulifanyia kazi.
“Nimepata taarifa hizo, lakini kwa sasa nipo nyumbani kwani hali yangu siyo nzuri kiafya, lakini vijana wangu wa kazi wanaedelea kuifanyakazi hiyo,” alisema.
CHANZO: NIPASHE

Benki Ya KCB Yatoa Msaada Wa Madawati Kwa Shule Ya msingi Ujirani Manispaa Ya Morogoro



Meneja wa Benki ya KCB Tanzania tawi la Morogoro, Carlos akiteta jambo na wazazi wa wanafunzi wa  shule ya msingi Ujirani iliyopo kijiji cha  Kienge B katika Kata ya Mkundi Manispaa ya Morogoro,baada ya kukabidhiwa msaada wa madawati 80 yenye thamani ya shilingi milioni 4.8.

Meneja wa Benki ya KCB Tanzania tawi la Morogoro, Carlos akiteta jambo na wazazi wa wanafunzi wa  shule ya msingi Ujirani iliyopo kijiji cha  Kienge B katika Kata ya Mkundi Manispaa ya Morogoro,baada ya kukabidhiwa msaada wa madawati 80 yenye thamani ya shilingi milioni 4.8.
Meneja wa Benki ya KCB Tanzania tawi la Morogoro, Carlos Msigwa wa pili kutoka (kulia) akipongezwa na Mkuu wa shule ya msingi ya Ujirani Philemon Kibuja, iliyopo kijiji cha  Kienge B katika Kata ya Mkundi Manispaa ya Morogoro,baada ya kukabidhiwa msaada wa madawati 80 yenye thamani ya shilingi milioni4.8. na benki ya KCB Tanzania,wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Mshauri wa shule Godfrey Tairo na Mwalimu wa kujitolea Lazaro Isondo.

Meneja wa Benki ya KCB Tanzania tawi la Morogoro, Carlos Msigwa akisalimiana na mmoja wa wanafunzi wa wanafunzi wa shule ya msingi ya Ujirani iliyopo kijiji cha  Kienge B katika Kata ya Mkundi, Manispaa ya Morogoro,baada ya kukabidhi msaada wa madawati 80 yenyethamani ya shilingi milioni4.8 kwa shule hiyo.
Meneja wa Benki ya KCB Tanzania tawi la Morogoro Tanzania , Carlos Msigwa akipongezwa na Diwani wa kata ya Mkundi Emelda Chambo, baada ya kumkabidhi  msaada wa madawati 80 yenye thamani ya shilingi milioni 4,8  kwa ajiri ya shule ya msingi ya Ujirani iliyopo kijiji cha  Kienge B, Manispaa ya Morogoro.
Afisa Masoko wa Benki ya KCB Tanzania tawi la Morogoro,Herieth Mwakifulefule akimsaidia kumvisha kiatu Kulwa Mussa, ambaye ni Mwanafunzi wa darasa la Tatu katika shule ya msingi ya Ujirani ya jamii ya wamasai iliyopo katika kijiji cha Kienge B, baada ya benki hiyo kutoa msaada wa madawati 80 yenye thamani ya shilingi milioni4.8. mtoto huyo tangu darasa la kwanza amekuwa akishika nafasi ya kwanza katika darasa lao.

BENKI ya KCB Tanzania imetoa msaada wa madawati 80 yenye thamani ya shilingi milioni nne na laki nane (4.8m) kwa shule ya msingi Ujirani iliyopo katika kata ya Mkundi manispaa ya Morogoro.

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya madawati hayo, Meneja wa KCB Tawi la Morogoro Carlos Msigwa alisema kuwa lengo la msaada huo lilikuwa kusaidia upungufu wa madawati katika shule hiyo na hivyo kuwawezesha wanafunzi kusoma vizuri

Meneja huo alisema kuwa Benki ya KCB inatambua umuhimu wa elimu bora katika maendeleo ya taifa na ndiyo maana haikusita kuelekeza msaada huo katika sekta ya elimu.

Akipokea msaada huo, diwani wa kata ya Mkundi Emelda Chambo aliishukuru Banki ya KCB kwa kutoa msaada na kusema kuwa utakuwa chachu kubwa katika maendeleo ya elimu katika shule hiyo ambayo inakabiliwa na upungufu mkubwa wa madawati.

Tuaishukuru sana KCB kwani wamekuwa kama walezi kwa shule yetu. Hii ni mara ya tatu kupokea msaada baada ya ule wa miti ya kivuli pamoja na vitabu.Tunaahidi kuyatunza madawati haya ili mtakaporudi tena myakute katika hali nzuri.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo Philemon Kibuja shule hiyo yenye wanafunzi 400 imekuwa ikikabiliwa na changamoto nyingi ikiwamo ukosefu mkubwa wa madawati.

“Mimi ndiyo mwalimu mkuu na mwalimu pekee katika shule hii. Nafundisha kuanzia darasa la kwanza hadi la saba. Shule hii kabla ya kupata msaada huu kutoka KCB haikuwa na dawati hata moja. Wanafunzi walilazimika kukaa chini, kwenye magogo na kwenye mabenchi,’ alisema

Mwalimu huyo aliishukuru Benki ya KCB na kuomba serikali pamoja na makampuni binafsi kuidia shule hiyo ambayo wanafunzi wengi wanatoka katika jamii za wafugaji.

“Shule hii yenye wanafunzi 400 ina madarasa matatu tu na mwalimu ni mimi peke yangu. Pamoja na jitihada kubwa ya kuomba msaada serikalini, serikali haijaweza kutusaidia. Tunaomba mashirika mbalimbali kujitikeza kutusaidia,” alisema
chanzo: Mjengwa

Bus La Muhamed Trans Lapata Ajali Km 15 Kutoka Bukoba Mjini


RPC Kelenge kulia akijadili jambo na RTO  Willy eneo la tukio
     Bus la muhamed trans lenye nambari  T884 likiwa limepinduka
Lori lenye nambari  T814 liliokua baada ya kugongwa na bus kwa kutokea nyuma.


Ajali hii imetokea asubuhi ya leo majira ya saa moja kasoro ni eneo la kyetema km 5 kabla ya kifika kemondo na ni umbali wa km 15 kutoka bukob mjini. Baada kwa kuligonga lori la mchanga  bus hilo lilikua likisafiri kutoka bukoba mjini kuelekea Mwanza, na abiria wote wamenusurika!

Picha kwa hisani ya:-
Bukobawadau
P. O.Box 316,
Bukoba – TANZANIA
Mobile:MC BARAKA GALIATANO +255 715 505043,
 SIR.LOOM   GALIATANO   +255 768 397241

WAPENZI WA ARSENAL WAKILIA NA KUSAGA MENO, KWA HASIRA WAFANYA HAYA


Muda mchache baada ya vilabu vya Arsenal na Man United kuthibitisha kwamba vimekubalina ada ya uhamisho wa mchezaji RobinVan Persie kujiunga na mashetani wekundu - baadhi ya mashabiki wa Arsenal wamekuwa wakipost picha mitandaoni kuonyesha namna walivyopokea taarifa za nahodha wao kwenda Old Traford. Wapenzi wa Arsenal vipi? KAMA YOYOTE AMBAYE ANATAKA KUONYESHA HASIRA ZAKE KAMA HAWA ATUME PICHA AU MAONI KWENYE EMAIL HII - shaffidauda@gmail.com

Chanjo ya Ebola huenda isipatikane


Virusi vya Ebola

Virusi vya Ebola
Wanasayansi wanaoendesha utafiti kuhusu virusi vinavyosababisha ugonga wa Ebola, wameiambia BBC kuwa, chanjo inayoweza kutumiwa kuzuia maambukizi ya virusi hivyo huenda isifumbuliwe.
Wiki chahche zilizopita idara ya ulinzi ya Marekani, Pentagon, ilisitisha ufadhili wake kwa kampuni mbili ambazo zilikuwa zikiendesha utafiti huo.
Mmoja wa wataalamu katika jopo hilo amesema kuna uwezekano mkubwa wa chanjo hiyo itakayotumiwa kuzuia mkurupuko wa ugonjwa wa Ebola haitatumika.
Ugonjwa wa Ebola umetajwa kama moja ya magonjwa hatari na ya kuogofya zaidi ulimwenguni.
Virusi hivyo vinasababisha homa kali ambayo hufanya mtu kuvuja damu katika viungo vya ndani na hata kupitia sehemu zingine kama vile masikio, mapua na hata ngozi.
Wataalamu wanasema virusi hivyo ambavyo hushambulia chembe chembe nyeupe na mishipa ya damu na kusababisha mwasho wa ngozi, macho mekundu, kutapika na mauimivu ya viungo.
Katika miezi ya hivi karibuni watu 16, waliaga dunia Magharibi mwa Uganda, kutokana na ugonjwa huo.
Kufikia sasa hakuna tiba kamili ya ugonjwa huo ambao unaweza kusababisha vifo kwa asilimia 90 ya watu walioambukizwa virusi hivyo.
Mikakati ya kujaribu kufumbua chanjo ya kutibu na kuzuia virusi vya Ebola imefadhiliwa na Idara ya Ulinzi na Taasisi ya Kitaifa ya Afya nchini Marekani NIH.
Idara hizo mbili zimewekeza mamilioni ya dola kwa utafiti huku zikiwa na wasi wasi kuwa virusi hivyo vinaweza kutumiwa kama silaha za kibiolojia.
Kutokana na ufadhili huo, chanjo kadhaa zimefumbuliwa na tayari zimefanyiwa majaribio kwa wanyama na matokeo yake yamekuwa ya kuridhisha.
Kampuni mbili Sarepta na Tekmira tayari zimeanzisha majaribio ya tiba hiyo kwa binadamu.
Lakini kampuni hizo zimefahamaishwa na Idara ya Ulinzi ya Marekani kusitisha utafiti huo mwa muda kutokana na ukosefu wa fedha.
Uamuzi wa mwisho kuhusu ikiwa ufadhili huo utarejelewa tena utatolewa mwezi ujao.

Syria yaondolewa kama mwanachama wa OIC


Ekmeledin Ihsanoglu wa OIC

Ekmeledin Ihsanoglu wa OIC
Jumuiya ya muungano wa nchi za Kiislamu (OIC) imesimamisha uanachama wa Syria katika muungano huo.
Baada ya kumalizika kwa mkutano wa viongozi wa Kiislamu uliofanyika mjini Mecca, katibu mkuu wa Muungano huo, Ekmeleddin Ihsa-noglu, alisema muungano huo wa mataifa ya kiislamu hauna nafasi kwa taifa ambalo serikali yake inawaua raia wake.
Hatua hiyo imesababisha kutengwa zaidi kwa Rais Bashar al-Assad baada ya jumuiya ya mataifa ya ki-arabu kuitimua mnamo mwezi Novemba.

Koffi Olomide ashitakiwa kwa kupigana



Koffi Olomide ashitakiwa kwa kupigana
Koffi Olomide, ambaye ni mwanamuziki mashuhuri barani Afrika ameshitakiwa kwa kumpiga Mtayarishaji wake wa muziki.
Mwanamuziki huyo alikamatwa na kufungiwa katika kituo cha polisi na kufikishwa mahakamani jumatano.
Koffi alikamatwa kufuatia vurugu katika hoteli moja mjini Kinshasa.
Waandishi wa habari wanasema mahakama hiyo ya Kinishasa ilifurika kutokana na watu wengi kuja kumuona kiongozi huyo wa bendi ya Quartier Latin akiwa kizimbani.
Kesi hiyo iliharishwa hadi Alhamisi asubuhi wakati atakaposhitakiwa rasmi.
Wakati wa kesi hiyo hapo jana Koffi Olomide aliwakilishwa na mawakili 10.
Ugomvi kati ya mwanamuziki huyo na mtayarishi wake Bwana , Diego Lubaki, ni kuhusu pesa dola $3,680.
Hakimu alimfahamisha mwanamuziki huyo ikiwa atapatikana na hatia huenda akafungwa jela miezi sita.
Olomide ni gwiji wa muziki aina ya "soukous", mtindo ulitokana na jina la kifaransa "secouer", lenye maana ya kujitikisa au kujinengua ,na wachezaji wake vile vile wanatambulika kwa kunengua maungo.

Mafuriko yasababisha vifo Nigeria


Mafuriko katika eneo la Jos

Mafuriko katika eneo la Jos
Takriban watu 33 wameuawa kufuatia mafuriko makubwa kati kati mwa jimbo la Plateau nchini Nigeria.
Afisa mmoja wa shirika la kutoa misaada, Abdussalam Muhammad ameiambia BBC, kuwa maelfu ya watu wameachwa bila makao baada ya makaazi yao kusombwa na maji.
Amesema usafiri umetatizika baada ya barabara kadhaa na daraja kusombwa na maji na hivyo kuvuruga shughuli za kutoa misaaada.
Zaidi ya watu elfu kumi na mbili wameathiriwa na mafuriko hayo yaliyokumba wilaya sita ikiwemo wilaya ya Shendam.
Mwezi uliopita watu thelathini na tisa waliuawa karibu na makao makuu ya jimbo hilo Jos.
Maafisa wa serikali wamewaonya raia katika maeneo hayo kuwa huenda kukatokea mafuriko zaidi katika siku za hivi karibuni.
Msimu wa mvua nchini Nigeria huanza mwezi Machi hadi Septemba Kila mwaka.
Bwana Muhammad, ambaye ni mshirikishi wa kutoa misaada ya dharurua wa shirika la kitaifa la kukabiliana na majanga katika eneo la kati nchini Nigeria, amesema waathiriwa hao wanahitaji misaada ya vyakula, maji, mavazi, blanketi na dawa.
Wilaya ya Shendam ni miongoni mwa sehemu zilizoathiriwa pakubwa na mafuriko nchini Nigeria.
Sehemu zingine ni pamoja na wilaya za Wase na Kanam.

Mzozo wa ziwa Nyasi kujadiliwa leo


Rais wa Tanzania

Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete
Rais wa Malawi Joyce Banda hii leo anaelekea jijini Maputo, nchini Msumbiji, kuhudhuria mkutano wa Jumuiya ya maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC, ambako anatazamiwa kukutana na Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete, ili kuzungumzia utata unaozunguka umiliki wa ziwa Nyasa katika mpaka wa mataifa ya Malawi na Tanzania.
Wakati hayo yakisubiriwa serikali ya Tanzania, imeendelea kusisitiza kuwa ni lazima mzozo uliopo kati yake na Malawi kuhusu umiliki wa ziwa hilo umalizwe kwa mazungumzo na sio kutumia nguvu.
Lakini kwa upande wake serikali ya Malawi imepuuuza wito huo wa serikali ya Tanzania na kusisitiza kuwa, ziwa hilo lote ni la Malawi hivyo utafiti wa mafuta utaendelea.

ALHAMISI YA LEO KATIKA MAGAZETI















Robin van Persie: Man Utd agree £24m deal with Arsenal for striker, Robin Van Persie (RVP)



Robin van Persie


Manchester United have agreed a £24m deal to sign Arsenal striker Robin van Persie on a four-year contract.
The 29-year-old will meet with United in the next 48 hours to discuss personal terms and have a medical.
Arsenal captain Van Persie announced in July he would not extend his current deal, which expires in June 2013.
"Manchester United is pleased to announce it has reached agreement for the transfer of Robin Van Persie," the club said in a statement. 
"The deal is subject to a medical and the agreement of personal terms. A further announcement will be made in due course."

Arsenal career in numbers

Joined: 2004
Transfer fee: £2.75m
Appearances: 278
Goals scored: 132
Goals scored last season: 37
Trophies won: Two (2004 Community Shield & 2004-05 FA Cup)
Consecutive seasons without a trophy: Seven
United will pay £22.5m, with a further £1.5m one-off bonus to follow if they win a Premier League or Champions League title in the next four years.
It is understood Arsenal were willing to make Van Persie their highest paid player ever, but never actually offered him a new contract.
The Netherlands international, who scored 44 goals in 57 games for club and country last season, maintained he would not discuss his future until after Arsenal's final match at West Brom on 12 May.
Three days later, he opened dialogue with Gunners boss Arsene Wenger and chief executive Ivan Gazidis at Wenger's house.
Wenger and Van Persie disagreed on their vision for the club, transfer activity and the team's performance in the 2011-12 campaign.
No contract was discussed and Van Persie joined the Dutch squad on 17 May to begin their preparations for Euro 2012.
He announced he would not be extending his contract on 4 July and returned to training on 17 July, the same week he was the subject of bids from United, Manchester City and Juventus.
All three offers fell short of Arsenal's valuation - they were reluctant to enter formal negotiations until a bid exceeded £20m, and hoped to hold out for £25-30m.
United, City and Juventus increased their offers but, of the three, United were the only side Van Persie would consider joining.

Past transfer dealings

Transfers between Arsenal and Man Utd are rare - Viv Anderson was the last to make the move, in 1987, although Mikael Silvestre did go in the other direction in 2008.
He was not part of the Gunners squad that left on 21 July for a pre-season tour to Asia but did travel with them on 6 August for a week-long training camp in Germany.
It is understood Van Persie was encouraged by the arrivals of Germany forward Lukas Podolski, France striker Olivier Giroud and Spain midfielder Cazorla - to the point where he was open to the idea of staying with or without a new contract.
But Wenger pulled him aside shortly before Sunday's friendly victory over Cologne,  told him he would be sold if a deal could be reached and informed the Dutchman he was no longer part of his plans.
Formal discussions between Arsenal and United began immediately, with Gazidis and United chief executive David Gill agreeing a fee of £22.5m on Tuesday, only for it to be vetoed by Wenger as he held out for £25m.
On Wednesday morning, United boss Sir Alex Ferguson called Wenger to offer £23m and Wenger quoted him £24m.
But a compromise was finally reached on Wednesday evening and Van Persie will travel to Manchester on Thursday to discuss terms and begin his medical.
Van Persie was named Professional Footballers' Association and Football Writers' player of the year but scored only once as the Netherlands were eliminated at the group stage of Euro 2012. 

Source: bbc.co.uk

PAMOJA NA KUFANYIWA OPERATION YA MOYO - MADAKATARI WAMWAMBIA MUAMBA HAWEZI KUCHEZA SOKA TENA - ATANGAZA KUSTAAFU




Hatimaye mchezaji wa Bolton Fabrice Muamba ametangaza kuachana na soka leo hii kutokana na ushauri wa daktari.

Mchezaji huyo mwenye asili ya Congo, alipata mshtuko wa moyo wakati wa mechi ya FA Cup dhidi ya Tottenham, amesema ana uchungu mkubwa kuachana na kucheza soka lakini hana budi zaidi ya kuweka mbele afya yake.

Muamba ameishukuru sana timu ya madaktari kwa kuokoa maisha yake na ameshukuru kwa maombi na sapoti kubwa aliyoipata kutoka kwa wapenzi wote wa soka duniani.

Moyo wa Muamba ulisimama kwa saa 78 baada ya kudondoka kwenye dimba la White Hart Lane baada ya kupatwa mshtuko wa moyo hali iliyopelekea kufanyiwa matibabu na kuweza kuokoa maisha yake.

Alikaa mwezi mzima Hosptali lakini aliwashangaza madaktari kwa jinsi alivyopata nafuu kwa haraka huku akisistiza anataka urudi kwenye dimba aendelee kucheza soka.

Kiungo huyo wa Bolton na England alienda mpaka nchini Ubelgiji wiki iliyopita kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji mdogo ili kuweza kuwa fiti kwa ajili kurudi uwanjani.


Mchumba wake Shauna ali-tweet kuwaambia mashabiki wa Muamba kwamba operation imeenda vizuri na atarudi kucheza soka kwa nguvu kuliko ilivyokuwa mwanzoni, lakini siku moja baadae madaktari wakampa taarifa mbaya kwamba kurudi kucheza soka kutahatarisha maisha yake kwa kuwa moyo wake hauwezi kuhimili.

Kabla ya kutangaza kustaafu Mumba aliwaambia mashabiki wake waendelee kutabasamu na kila kitu kitakuwa poa.

Historia yake ya soka na kuanza kujulikana ilianzia katika academy ya soka ya Arsenal mwaka 2002 kabla ya kuhamia Birmingham na baadae akaenda Bolton mwaka 2008.


chanzo: Shaffih Dauda

SIMBA B YALIPA KISASI KWA AZAM FC NA KUTINGA FAINALI SUPER8 CUP




Timu ya soka ya Simba B imeifunga timu ya Azam katika mchezo wa nusu fainali wa kombe la Super 8 katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

Magoli ya Simba yalifungwa na wachezaji Rashid Ismial na Haroun Athumani wakati goli la kufutia machozi la Azam lilifungwa na beki wake wa kutumainiwa Saidi Morad.

Kwa ushindi huo Simba itacheza fainali ya Super 8 siku ya Jumamosi dhidi ya wakata miwa wa manungu Mtibwa Sugar ambao mapema leo waliwafunga Jamhuri ya Pemba mabao 5-1.

Simba leo waliwakilishwa na kikosi cha Abuu Hashimu(18), Miraj Adam (19), Omary Salum (11)/William Lucian ‘Gallas’, Hassan Isihaka (5), Hassan Hatibu (15) Said Ndemla (13), Haroun Athumani (7), Abdallah Seseme (17), Rashid Ismail (8), Edward Christopher (9)/Ramadhan Mzee na Frank Sekule (4)Ibrahim Ajibu.
Benchi; Saleh Malande (1), Ramadhan Mzee (2), William Lucian ‘Gallas’(3), Kenny Alex (12), Mohamed Salum (16), Ibrahim Ajibu (20) na Jesse Nyambo (14).
Makocha: Suleiman Matola. Msaidizi; Amri Said.

Azam FC - Wandwi Jackson (18), Ibrahim Shikanda (21), Samir Hajji Nuhu (11), Said Mourad (15), Luckson Kakolaki (5), Abdulhalim Humud (24), Sunday Frank (12), Jabir Aziz (25)/Khamis Mcha, Gaudence Mwaikimba (17)/Zahor Pazi, Abdi Kassim (20) na Kipre Herman Tcheche (27)Hamisi Mcha.

Benchi; Aishi Mfula (1), Omary Mtaki (2), Himid Mao (23), Khamis Mcha (22), Kelvin Friday (28). Abdulghani Gullam (14) na Zahor Pazi (9).
Makocha: Boris Bunjak (Serbia). Msaidizi; Vivek Nagul (India).

VIFAA VIPYA VYATUA SIMBA SPORTS CLUB!


Mohamed Nassor (kushoto) akimshuhudia mshambuliaji  wa klabu ya Simba, Daniel Akuffo akisaini mkataba wa kuichezea klabu hiyo. 

 
Mohamed Nassor (kushoto) akimshuhudia beki mpya ,Paschal Ochieng akisaini mkataba wa kuichezea klabu hiyo.
Ochieng kulia na Akuffo kushoto

Mawaziri Watajwa Kuficha Mabilioni Benki Za Uswisi

ZITTO ASEMA YUMO KIONGOZI WA JUU WA SERIKALI YA SASA,WENGINE NI WA AWAMU YA MKAPA, ATISHIA KUWAANIKA

TUHUMA kwamba baadhi ya vigogo Serikali wameficha mabilioni ya fedha nchini Uswisi jana ziliibuka tena bungeni, huku Kambi ya Upinzani ikidai kwamba inawafahamu wahusika wa ufisadi huo na kutishia kuwataja ikiwa Serikali haitawataja.

Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe aliitaka Serikali kuwataja kwa majina viongozi na wafanyabiashara wakubwa walioficha Sh315.5 bilioni nchini Uswisi, akisema kwamba watu hao “wanafahamika”.

Juni mwaka huu, Benki Kuu ya Uswisi ilitoa taarifa inayoonyesha kuwapo kwa kiasi cha Sh315.5 bilioni zilizotoroshwa Tanzania na kufichwa nchini humo na vigogo ambao ni wanasiasa pamoja na wafanyabiashara.

Akiwasilisha hotuba ya kambi yake kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Fedha na Uchumi bungeni jana, Zitto ambaye pia ni Waziri Kivuli wa wizara hiyo alisema mmoja wa viongozi wa juu wa Tanzania na baadhi ya mawaziri wa Serikali za awamu zilizopita ni miongoni mwa wamiliki wa fedha hizo.

“Kambi ya Upinzani bungeni imepata taarifa kuwa mmoja wa viongozi wa juu kabisa wa Tanzania na baadhi ya mawaziri wa awamu zilizopita ni miongoni mwa fedha hizi,” alisema Zitto.

Pia aliitaka Serikali kuliambia taifa ni hatua gani itakazochukua kurejesha fedha hizo pia kuwataka wamiliki wake na kama ikishindwa, wao watawataja.

“Tunaitaka Serikali kutoa taarifa rasmi ya hatua gani imechukua mara baada ya taarifa ile kutoka Benki ya Taifa ya Uswisi ilipotolewa,” alisema Zitto na kuongeza:

“Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni italazimika kuweka wazi taarifa na majina ya watu wenye umiliki wa fedha hizo iwapo Serikali haitatoa taarifa rasmi,” alisisitiza.

Fedha hizo zinadaiwa kutokana na biashara (deals) zilizofanywa na watendaji wa Serikali na wafanyabiashara kwenye Sekta za Nishati na Madini na kwamba sehemu kubwa ya fedha zililipwa na kampuni za utafutaji mafuta na gesi katika pwani ya Mkoa wa Mtwara zilizopewa mikataba kati ya mwaka 2004 na 2006.

Baada ya Zitto kumaliza kuwasilisha hotuba yake, Mbunge wa Simanjiro (CCM), Christopher Ole-Sendeka aliomba mwongozo wa Spika kuhusu suala hilo.

Sendeka alisema Zitto alisema miongoni mwa walioficha fedha hizo ni kiongozi wa juu wa Tanzania, lakini akashangaa Serikali kutohoji juu ya kauli hiyo.

“Mheshimiwa Naibu Spika, mheshimiwa Zitto amewatuhumu viongozi wa Serikali na kiongozi wa juu kabisa kuwa wameficha fedha Uswisi,” alisema.

Alisema, lakini pamoja na tuhuma hizo, hakuna kiongozi wa Serikali aliyesimama na kutolea ufafanuzi hivyo akaomba mwongozi ili Zitto aruhusiwe kuwataja.

Sendeka alisema tuhuma hizo ni nzito na zimeichafua sura ya Serikali hivyo ni vyema ijulikane ni nani kati ya Serikali na Zitto atabeba mzigo wa kuwataja.
Naibu Spika, Job Ndugai alisema angetoa mwongozo huo baada ya kuipitia hotuba hiyo ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na kuona kama ina matatizo. Hata hivyo, hakutoa mwongozo huo.

Mbio Za Mwenge Wa Uhuru Mkoani Arusha



Wasichana wa jamii ya Wadzabe wakiwa kwenye pozi kuulaki Mwenge wilayani Ngorongoro.

Baadhi ya wananchi waliopata bahati ya kushika Mwenge wa Uhuru kwenye kituo cha Polisi Ngorongoro kilichokarabatiwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro(NCAA).
Mkuu wa mkoa wa Arusha,Magesa Mulongo akiwa ameshika Mwenge wa Uhuru kabla ya kuukabidhi kwa mkuu wa mkoa wa Mara kwenye lango la Hifadhi ya Taifa Serengeti

Mkuu wa wilaya ya Karatu,Felix Ntibenda(kulia)akiwa na wakimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa na askari wa kutuliza ghasia mkoa wa Arusha wakiwa katika hali ya hamasa na ukakamavu