Saturday, August 18, 2012

JUMAMOSI YA LEO KATIKA MAGAZETI














Ferdinand atozwa faini



Rio Ferdinand
Beki wa Manchester United Rio Ferdinand ametozwa faini ya pauni za Uingereza 45,000 sawa na dola za kimarekani $71,000 na chama cha mpira cha England baada ya kupatikana na hatia ya kutumia lugha mbovu kuhusu beki wa Chelsea Ashley Cole.
Halmashauri huru imempata na hatia kwa kumkashifu Cole akitumia lugha inayopdhalilisha ukoo na kabila la mpinzani kwa msemo wa maneno 'Choc ice' kwa maana mtu mweusi nje na ndani mzungu.
Ferdinand alikanusha kua sivyo hivyo ila ni kwamba maanake ni mtu feki, au mnafiki.

Ashley Cole
Matamshi yaliyopeperushwa kwa mtandao wa Twitter yalitokea baada ya Ashley Cole kutoa ushahidi mahakamani dhidi ya mdogo wake Rio aliyedai kua alitukanwa na John Terry. Terry hakupatikana na hatia.

Wajumbe: " Mwenyekiti, Gazeti La Kisiwa Lituombe Radhi Wasomaji"



Ndugu Mwenyekiti, 
Gazeti la KISIWA la Ijumaa ya tar; 17 August lenye kichwa cha habari: MFUNGO WAISHA NA MIUJIZA MIKUBWA.
Mwanzo kabisa baada ya kuziangalia picha hizo nilidhani ni gazeti la Aprili Mosi ile siku ya wajinga, la hasha ni la leo na ni habari kama habari zingine za kina.
Mwenyekiti naomba uiweke hii kwenye ukurasa wako wa mbele kwa faida ya wengi - maana si wote wanaosoma maoni, ila ikiwa hapo juu mbele watu wote wataona uozo huu wa kuweka habari bila chunguzi za kina.
Maoni yangu kwa wizara ya habari isiishie tu kufungia magazeti yanayowachachafya wanasiasa, hata haya yanayopotosha umma kwa malengo ya kuuza kupitia imani za watu ni kebehi na hayatufai. Watuombe radhi ukurasa wa mbele kama yalivyoweka habari katika ukurasa huo, nina imani watauza pia.
Picha iliyopo ni ya mtindo unaoitwa wa "multimedia", hivyo ni ya kutengeneza.
Tafakari;
(1) watu waliouwawa na joka hili la kutisha ni wengi kiasi cha kuashiria uwepo wa watu wengi katika eneo hilo, lakini cha kushangaza hakuna watu wa kulishangaa na kusherehea kuuwawa kwaa joka katika mji huu uliopoteza watu wengi. Pata picha sawaka limeuwawa Nyeregete kule kijijini kwa Mwenyekiti halafu umeamua kupiga picha, sidhani kama kutakosa watu wa kulishangaa.

(2) Hili ni joka kubwa sana, la miujiza ya kipekee, limepoteza maisha ya watu wengi sana, haiingii akilini kwamba walimuua hawakuwa na shauku ya kuweka kumbukumbu kwa kupiga picha ya pamoja na joka hili tutakaloliingiza kwenye kitabu cha rekodi za dunia cha Guinnes, kama zipo mtuzodoe kwa kuziweka hewani tuzione, naahidi kuomba radhi, kufuta kauli na kuwasifu kwa kazi nzuri.

Picha yenyewe;
(1) Angalia kwa umakini gari lilobeba nyoka, kwa waliokuwa na wazazi wenye nafuu walipata kuendesha magari haya wakati wa kuchezea ya plastiki, nakumbuka jirani yangu walikuwa na tipa la kubinua mchanga, la njano kwa kumbukumbu nzuri, sisi tulindesha ya mbao yakiwa na matairi tulikata kwenye malapa ya umoja, wengine waliendesha ya mabati ya korie na wengine ya kukata maboksi ya biskuti. Hata askari aliyekalia nyoka naye ni wa plastiki.

Yaani iko hivi, nyoka wa kweli kwenye gari la plastiki (trick of the eye), halafu ikafanyiwa editing kidogo kwa kompyuta kuongezea background.


Kiufupi ni kwamba, habari ni ya kutengeneza na picha ni ya kutengeneza kwa ufundi mbovu.


Ndugu zangu wa gazeti la KISIWA mtuombe radhi, hapa hakuna Elimu, hakuna Maarifa wala Habari.


Mwenyekiti nitakushukuru kama hautaiweka hii nyuma ya pazia la "comments" na badala yake uiweke usoni ili wengi wapate kuiona na kuisoma ili wachangie katika hili.


Inakera kuona baadhi ya wanataaluma ya habari kutofanya tafiti za kina kabla kutujuza vinavyojiri kama habari.


Mdau - Hussein


Mungu Ibariki Tanzania na watu wake.

Mjumbe mwingine: Mfungo waisha na miujiza mikubwa, gazeti KISIWA.
Maoni yangu kwa wizara ya habari isiishie tu kufungia magazeti yanayowachachafya wanasiasa, hata haya yanayopotosha umma kwa malengo ya kuuza kupitia imani za watu ni kebehi na hayatufai mtaani. Watuombe radhi ukurasa wa mbele kama yalivyoweka habari katika ukurasa huo, watauza pia.
Picha iliyopo ni ya mtindo wa "multimedia",hivyo ni ya kutengeneza.
Tafakari; (1) watu waliouwawa na joka hili la kutisha ni wengi kiasi cha kuashiria uwepo wa watu wengi katika eneo hili, lakini cha kushangaza hakuna watu wa kulishangaa katika mji wa watu wengi. Pata picha sawaka limeuwawa Nyeregete kule kijijini kwa Mwenyekiti halafu umeamua kupiga picha, sidhani kama kutakosa watu wa kulishangaa. (2) Hili ni joka kubwa sana, la miujiza ya kipekee, limepoteza maisha ya watu wengi sana, haiingii akilini kwamba walimuua hawakuwa na shauku ya kuweka kumbukumbu kwa kupiga picha joka hili, kama zipo mtuzodoe kwa kuziweka hewani tuzione na tuwasifu kwa kazi nzuri.
Picha yenyewe; (1) Angalia kwa umakini gari lilobeba nyoka, kwa waliokuwa na wazazi wenye nafuu walipata kuendesha magari haya wakati wa kucheza, sisi tulindesha ya mbao, mabati na ya kukata maboksi. Hata askari aliyekalia nyoka naye ni wa plastiki. Yaani iko hivi, nyoka wa kweli kwenye gari la plastiki (trick of the eye), halafu ikafanyiwa editing kwa kompyuta POORLY.
Kiufupi ni kwamba, habari ni ya kutengeneza na picha ni ya kutengeneza kwa ufundi mbovu.
Ndugu zangu wa gazeti la KISIWA mtuombe radhi, hapa hakuna Elimu, hakuna Maarifa wala Habari.
 Source: Mjengwa