Waziri wa Ujenzi, Dk Harryson Mwakyembe
WAZIRI
wa Ujenzi, Dk Harryson Mwakyembe amesema serikali itabeba jukumu la
kulipa mishahara ya wafanyakazi Shirika la Reli Tanzania na Zambia
(TAZARA, baada ya wafanyakazi hao kucheleweshewa mshahara yao kwa
kipindi cha miezi mitatu.
Kauli
hiyo imekuja baada ya wafanyakazi wa shirika hilo kufikisha kilio chao
kwa Waziri huyo kuwa wamekuwa wakiishi maisha ya kubangaiza kutoakana
ucheleweshwaji wa mishahara yao.
Akizungumza
na wafanyakazi hao, kwenye ofisi za Shirika hilo (TAZARA), jijini Dar
es salaam jana, Dk Mwakyembe alisema akiwa waziri wa wizara hiyo
anawaahidi hatakubali kuona wanaishi bila kulipwa mishahara huku
wakifanya kazikwa juhudi.
Dk
Mwakyembe alibainisha kuwa serikali imepokea kilio chao hivyo italipa
sh bilioni1.3 kama mshahara wa miezi miwili kati ya miezi hiyo mitatu
wanayodai kuanzia leo (jana).
Aliitaja
miezihiyo itakayolipwa kuwa ni pamoja na Juni na Julai ambapo amewataka
viongozi wa Shirika hilo kutoa maelezo kuwa ni kwanini hadi sasa
hawajalipa mishahara wafanyakazi hao.
Akizungumzia
madai ya wafanyakazi hao ya kutaka kung’olewa madarakani kwa
Mkurugenzi Mkuu,Mbegusita Akashambatwa na Naibu wake, Damus Ndumbalo,
alisema shirika hili ni la kimataifa linalohusisha nchi mbili hivyo
maamuzi yake ni lazima ya husishe viongozi wa pande zote mbili.
Aidha,
alitoa onyo kuhusu vitendo vya hujuma ikiwa ni pamoja na wizi kuwa wale
wote wanaojihusisha watambuwe kuwa dawa yao iko jikoni inachemka.
Katika
hatua nyingine amesema amesikitishwa sana kuona kuwa wafanyakazi wa
Mradi wa Ukarabati wa Train Mijini, hadi leo hawjalipwa mishahara ya
miezi miwili,fedha hizo lilikwishatengwa.
“Nilisikitika
sana kumkuta yule dada Mwanamisi akiwa amevaa overrol lake huku
akiunganisha vyuma tena amefunga mfungo wa Ramadhani ambapo aliniambia
tunafanyakazi lakini hatujalipwa mishahara inishangaza sana nataka
walipwe haraka”alisema Dk Mwakyembe.
Awali
Katibu Mkuu wa chama cha wafanyakazi shirika hilo, Ernest Kiwele,
alisema wamechoshwa na tabia za viongozi hao kuwa wamekuwa chanzo cha
matatizo yote yanayowakabili wafanyakazi hao.
0 comments:
Post a Comment