Rais wa Malawi Joyce Banda hii
leo anaelekea jijini Maputo, nchini Msumbiji, kuhudhuria mkutano wa
Jumuiya ya maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC, ambako
anatazamiwa kukutana na Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete, ili kuzungumzia
utata unaozunguka umiliki wa ziwa Nyasa katika mpaka wa mataifa ya
Malawi na Tanzania.
Wakati hayo yakisubiriwa serikali ya Tanzania,
imeendelea kusisitiza kuwa ni lazima mzozo uliopo kati yake na Malawi
kuhusu umiliki wa ziwa hilo umalizwe kwa mazungumzo na sio kutumia
nguvu.Lakini kwa upande wake serikali ya Malawi imepuuuza wito huo wa serikali ya Tanzania na kusisitiza kuwa, ziwa hilo lote ni la Malawi hivyo utafiti wa mafuta utaendelea.
0 comments:
Post a Comment