Monday, August 6, 2012
JOSE MOURINHO AFUNDISHA MAKOCHA 200 WA KIMAREKANI
Wakati Real Madrid wakiwa kwenye mazoezi huko UCLA, Jose Mourinho alikuwa akitoa darasa la masaa mawili aliloliita "Mourinho Way" katika chuo kikuu. Huku akisaidiwa na wasaidizi wake pamoja na program ya powerpoint, Mourinho alitoa darasa kwa makocha wa kimarekani 200.
"Hakuna sababu moja wa mbili kwa mafanikio yangu. Kuna vitu vingi sana na ambavyo vifanye kwa kazi kwa umoja," aliwaambia wanafunzi wake."
Mourinho pia akatoa mafunzo kuhusu namna anavyoongoza benchi la ufundi, kugawanya na kusambaza kazi miongoni mwa wasaidizi wake, namna anavyojua kucheza na akili za wapinzani na jinsi ya anavyowajenga kiakili wachezaji wake na vitu vingine vingi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment