Monday, August 6, 2012
SIMBA YAMSAJILI REDONDO KWA MIL 30 ASAINI MKATABA WA MIAKA 2
Klabu ya Simba imeendelea kufungua makucha yake katika soko la usajili, baada ya wiki iliyopita kumtwaa Mbuyi Twite na Mrisho Ngassa, leo hii klabu hiyo imefanikiwa kumsajili kiungo wake wa zamani aliyekuwa akiichezea Azam Ramadhan Chombo Redondo.
Kwa taarifa rasmi nilizozipata kutoka kwa Redondo mwenyewe ni kweli amesaini mkataba na Simba akitokea Azam baada ya mkataba wake kumalizika. "Nimesaini mkataba wa miaka miwili na Simba nikiwa mchezaji huru baada ya mkataba wangu na mwajiri wangu wa zamani Azam kumalizika"
Redondo ambaye aliondoka Simba takribani miaka 3 iliyopita, amesaini Simba kwa ada ya millioni 30, leo pekee wakati akisaini amepewa shilingi millioni 20, na millioni 10 zilizobaki atamaliziwa baadae.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment