Mabingwa wa kombe la klabu Bingwa Afrika
Mshariki na kati kombe la Kagame, timu ya Young Africans Sports Club
leo imepongezwa na Wabunge wa Bunge la Jamhuri wa Muungano Tanzania kwa
kufanikiwa kutwaa Ubingwa huo.
Akiongea katika Ukumbi wa Bunge,
Spika wa Bunge la Jahmuri ya Muungano wa Tanzania mh, Anna Makinda
alisema anawapongeza wachezaji na viongozi wake wote, kwa kulilteta
Taifa ubingwa huo ambao timu 11 kutoka nchi wanachama zilishiriki.
Mh
Makinda alisema anafuraha siku ya leo, kwa kuwa Bunge limetembelewa na
wageni wengi, wakiwemo watu mashuhuri na wageni maalumu timu ya Young
Africans Sports Club.
Spika alianza kwa kuwatambulisha Bodi ya
Wadhamin wa klabu ya Young Africans wakiongozwa na mama mlezi wa klabu
hiyo, Mama Karume, Francis Kifukwe kisha akawatambulisha Mwenyekiti mpya
wa Young Africans Yusuph Manji na makamu mwenyekiti ndugu Clement
Sanga.
Baada ya hapo ilifuata zamu ya wachezaji na viongozi
wakiwa na wazee wa klabu hyo, makofi mengi mfululizo zaidi ya dakika
moja vilianza kupigwa kwenye meza baada ya Nahodha Nadir Haroub
Cannavaro kusimama na kuonyesha Kombe kwa watu wote na wabunge
waliokuwepo ndani ya bunge.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda pamoja na
baadhi ya wabunge na mawaziri baada ya utambulisho wa Young Africans
ndani ya bunge, walitoka nje kwa pamoja na kupiga picha na wachezaji na
viongozi wa yanga wakiwa na kombe hilo la Kagame.
Baada ya
utambulisho, wabunge wa wanachama wa Young Africans waliaaalika wageni
wao wote kupata kifungua kinywa katika mgahawa wa bunge.
Wabunge
wanachama wa Young Africans waliandaa kikao cha mda mfupi ndani ya
ukumbe wa bunge la zaman (Msekwa Hall) ambapo wabunge, viongozi na
wachezaji waliweza kufahamiana kwa undani zaidi.
Mwenyekiti Yusph
Manji alifungua rasmi tawi jipya katika eneo la Bunge ambapo mwenyekiti
wa Yanga tawi la bungeni ni mh. misanga, katibu mkuu wake akiwa ni Mh
Godfrey Zambi, mweka hazina mh.Martha Mlata huku Grace Kiwelu, Mwigulu
Nchemba, Faki Makame, na wengineo wakitajwa kama wajumbe katika uongozi
huo.
Mh Captain George Mkuchika ambaye jana aliteuliwa kuwa
mjumbe wa bodi ya wadhamin wa klabu, pia ndio aliyeteuliwa kuwa mlezi wa
tawi la Young Africans bungeni.
Dua za kubariki tawi hilo
zilisomwa kwa pande zote mbili za dini kisha wabunge na viongozi kupiga
picha za pamoja, ambapo pia jioni ya leo wabunge wameaanda futari kwa
ajili ya wageni hao.
Timu inatarajiwa kureje jijini Dar kesho
kuendelea na maaandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu nchini inayotazamiwa
kuanza septembe mosi.
Source: http://www.youngafricans.co.tz
MAMA SALMA KIKWETE ASHIRIKI ZOEZI LA KUPIGA KURA
6 hours ago
0 comments:
Post a Comment