JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUWEPO KWA MGONJWA WA EBOLA, WILAYA YA KARAGWE MKOA WA KAGERA, TANZANIA
Utangulizi
Wizara
ya Afya na Ustawi wa Jamii inapenda kutoa taarifa kwa umma, kuhusu
tetesi zilizokuwa zimeenea hapa nchini kutoka kwenye vyombo mbali mbali
vya habari kuhusu kuwepo kwa mgonjwa wa Ebola,wilayani Karagwe mkoa wa
Kagera.
Mnamo
tarehe 3 Agosti 2012, Wizara ya Afya na Ustawi Wa Jamii ilipokea
taarifa kutoka kwa mganga mkuu wa wilaya ya Karagwe ya kuwepo kwa
mgonjwa aliyekuwa anahisiwa kuwa na dalili za ugonjwa wa Ebola, katika
hospitali ya Wilaya ya Nyakahanga. Aidha,taarifa hiyo ilibainisha kuwa
mgonjwa huyo alikuwa ni mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka (6|) kutoka
katika kijiji cha Nyakatundu wilayani Karagwe. Mgonjwa huyu alikuwa na
dalili za homa kali, kulegea, kutokwa damu puani, kutapika damu, na
kukojoa damu.Maelezo kutoka kwa mama mzazi zilieleza kuwa mtoto huyu
alianza kuugua kuanzia tarehe 30 Agosti 2012, ambapo alipatiwa dawa ya
Septrin baada ya hospitali binafsi kuonyesha kuwa ana ugonjwa
wa“Typhoid”.
Uchunguzi
wa awali katika hospitali ya Nyakahanga ulionyesha kuwa mtoto huyu
alikuwa anasumbuliwa na uambukizo kwenye haja ndogo (Urinary Tract
Infection).Vile vile alifanyiwa uchunguzi wa kimaabara na Vipimo vya
malaria, Hepatitis na Typhoid havikuonyesha kuwepo kwa magonjwa haya.
Hospitali inaendelea kumpatia matibabu mtoto huyu na imewaweka mgonjwa
na mama yake anayemtunza kwenye chumba maalum (Isolatiom room) kwa ajili
ya uangalizi zaidi.
Aidha
mnamo tarehe 4 Agosti 2012, timu za wataalamu kutoka Wizara ya Afya na
Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na timu ya mkoa wa Kagera imeweza
kufika na kumfanyia uchunguzi wa kina pamoja na kuchukua sampuli za damu
kwa ajili ya uchunguzi zaidi katika maabara ya Taifa ya uchunguzi wa
magonjwa na Maabara za nje ya nchi, ili kubaini kama ameathirika na
ugonjwa wa Ebola. Timu hiyo ya wataalamu imetoa taarifa kuwa hali ya
mgonjwa huyu kwa sasa imeimarika ikiwa pamoja na kutokuwa na homa,
kutapika na kukojoa damu kumekoma pia, uchunguzi uliofanywa kwa mama wa
mtoto umeonyesha kuwa hana dalili zozote za ugonjwa wa Ebola.Vile vile
hakuna taarifa ya mtu mwingine yeyote kwenye familia hiyo au kwenye
maeneo ya kijiji hicho au cha jirani kuwa na dalili za ugonjwa huo.
Kufuatia taarifa hii, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na Mkoa wa Kagera imechukua hatua zifuatazo;
•
Imepeleka timu ya wataalamu mbali mbali kutoka Wizarani na mkoa kwa
lengo la kwenda kufuatilia na kutoa taarifa kuhusu kuwepo kwa ugonjwa
huo.
•
Imetoa elimu ya Afya kuhusu njia za kuzuia kuenea ugonjwa wa Ebola
pamoja na dalili za ugonjwa huu, kwa wananchi na watumishi wa afya
katika hospitali ya Nyakahanga
• Kupeleka vifaa kinga katika hospitali ya Nyakahanga pamoja na maeneo ya mipakani
•
Kutoa matangazo kwa jamii kwa kutumia vipaaza sauti na kupitia radioni
(Radio Karagwe) kuhusu ugonjwa huu. Aidha, vipeperushi pia vimetolewa.
Hitimisho
Wizara
inapenda kuufahamisha umma kuwa mpaka sasa hakuna mgonjwa yeyote
aliyethibitishwa kuwa na ugonjwa wa Ebola hapa nchini.Aidha, Wizara ya
Afya imejiaanda kikamilifu kukabiliana na ugonjwa huu iwapo utatokea
hapa nchini.
Kwa
sasa timu za wataalum zipo katika mikoa ya Mara, Mwanza, Kagera,
Kigoma, Kilimanjaro na Arusha, kutoa elimu juu ya ugonjwa huu kwa
wataalamu na kwa wananchi na vilevile kufuatilia ugonjwa huu sehemu za
mipakani.
Wizara
inaendelea kutoa wito kwa wananchi kutoa taarifa haraka kwenye kituo
chochote cha kutolea huduma za afya, mara wanapoona dalili za ugonjwa
huu.
0 comments:
Post a Comment