Friday, August 10, 2012

CWT YATAMKA WALIMU KUENGULIWA KATIKA SENSA


Kabla ya kuanza kwa mgomo wa walimu, Mwenyekiti wa Tume ya Sensa na Makazi aliwatangazia watanzania kuwa jumla ya walimu 150,000 sawa na asilimia 75 ya walimu wote watashiriki katika zoezi la sensa ya watu na makazi.
 Kutokana na mgomo wa walimu baadhi ya wakuu wa mikoa na wilaya wamewaondoa walimu kwenye zoezi la sense kwa kile kinachoonekana kuwa ni maagizo kutoka ofisi ya Waziri Mkuu.
Kwa mujibu wa taarifa ya rais wa CWT Mwl. Gratian Mukoba, serikali iliorodhesha majina ya walimu waliogoma na viongozi wa CWT kwa maelekezo yanayodaiwa kutolewa na Kaimu Katibu Mkuu TAMISEMI Mwl. Jumanne Sagiti.
Kutokana na hatua hiyo, Chama kinawaomba wanachama wake waliogoma na kuondolewa kwenye sensa kutokata tamaa kwa kukosa pesa ambazo zingewasaidia kwa muda wa wiki moja tu.
Badala yake wajitambue kuwa uboreshaji wa maslahi yao utatokana na wao wenyewe.

0 comments:

Post a Comment