Friday, August 17, 2012

CHADEMA YAZIDI KUJIKUSANYIA WANACHAMA - Kilosa


Vuguvugu la M4C linaloongozwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA limeonekana kutikisa chama cha wananchi CUF wilayani Kilosa ambapo mbali ya wanachama wengi sana wa CUF kujiunga CHADEMA pia Mjumbe wa mkutano Mkuu CUF Taifa Bwana Wille Lemi alijitoa rasmi katika CUF na kukabidhiwa kadi na Kiongozi wa upinzani nchini ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa.

Katika mkutano huo Dr Slaa aliwataka wananchi wa vyama vyote kuunganisha nguvu kwa pamoja chini ya vuguvugu la M4C ili kuhakikisha katika uchaguzi mkuu ujao wananchi wanapata serikali itakayojali maslahi yao chini ya CHADEMA.

Dr Slaa pia alishukuru mwitikio wa wanakilosa kutokana na mkutano huo kufurika umati mkubwa wa watu.Mbali na CUF kupoteza wanachama wengi pia mamia ya wanaCCM walikihama chama chao na kujiunga rasmi CHADEMA kuunganisha nguvu katika vuguvugu la M4C.Idadi ya wanachama wapya waliojiunga CDM katika mkutano wa Kilosa ulikuwa zaidi ya elfu moja.
Kilosa ilikuwa ni mojawapo ya maeneo yenye wanachama wengi wa CUF lakini inaonekana ziara ya Dr Slaa imesimika rasmi CHADEMA kama chama kinachopendwa zaidi Kilosa.
Kutoka Chademablog

0 comments:

Post a Comment